Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

mimi ni mmoja wa wanafunzi nimesoma apo FEZA o-level na high-level. shule za FEZA hazina mtaala wowote unaofundisha ugaidi.

shule ina walimu mchanganyiko waturuki na watanzania. wanafunzi wengine niliosoma nao sasa hivi ni walimu apo FEZA. kwa mfano mkuu wa shule ya FEZA boys alisoma apo O-level baadae akafanya bachelor Uturuki na masters kafanya UDSM.

miaka yote iyo tumesoma mpaka sasa kila mtu anafanya maisha yake sijawahi kusikia ata siku moja mwanafunzi yeyote wa FEZA ambaye amefanya tukio la kigaidi. wengi wetu tumekua watu wema kutokana na mafunzo mazuri tuliyopata pale shuleni.

nimewahi kua moja wa kiongozi wa wanafunzi ila hakuna ata siku moja ambayo tumeelekezwa tufanye tukio la ovyo. shule ziko serious na elimu pekee. shule za FEZA zinajiendesha kutoakana na ada wanazolipa wazazi wa wanafunzi matajiri pia wanafunzi maskini wanasomeshwa kutokana na michango ya wazazi matajiri na baadhi ya wanafunzi waliosoma apo ambao asilimia kubwa wamefanikiwa kimaisha.

ivyo basi kwa mimi binafsi naweza kusema kuwa shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule na ugaidi. Uturuki raisi Erdogan amevurugwa tu kutokana na sera zake za ovyo za kuminya demokrasia na ndio maana mpaka leo umoja wa ulaya (EU) wameshindwa kuiruhusu uturuki kujiunga na umoja huo kutokana na uvunjifu mkubwa wa demokrasia.

Waturuki ni watu wanapenda sana biashara na wamesambaa kila kona ya dunia na wamechangia kukua kwa uchumi kwa nchi mbalimbali duniani kwa kutoa ajira kwa wazawa wa mataifa ambayo wanawekeza. kwa mfano ukienda Poland, Germany na mataifa mengi tu ya ulaya jamaa wametoa ajira kwa mamilioni ya watu.

kwa mfano rafiki zangu wengi tu hapa bongo na ata nje ya nchi wanafanya kazi na waturuki na wako vizuri tu. Fethullah Gullen yeye sio mmiliki wa shule za FEZA ila yeye alitoa idea kwa waturuki kuanzisha mashule nje ya uturuki ili kutoa elimu bora kwa mataifa mbalimbali duniani.

Hachangii na wala hapewi ata senti kutoka kwenye shule. uwekezaji hapa bongo wote umefanywa kutokana na ada na michango ya watanzania wachache ambao wameshawishika kuchangia shule.

rafiki yangu mmoja baba yake mzazi ametoa tiles za shule nzima for free. mimi pamoja na wanafunzi wengine tumeshapiga rangi sana shule za FEZA kwa kujitolea. ivyo basi naweza sema shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule ayo mambo yao ya ndani ya uturuki wajaribu kumalizana nayo wenyewe.

huo ubalozi kama unajua kuhusu iyo michango ya kigaidi basi wafungie hizo account ambazo zinapewa iyo misaada. Nigeria wamemgomea Erdogan na serikali yake kuhusu kufunga shule za aina ya FEZA ambazo zipo Uturuki ivyo serikali yetu isiyumbishwe kutokana na uyo Erdogan.

shule hizi zinazalisha wataalamu wakutosha ambao wana mchango mkubwa tu kwa taifa ili. rafiki zangu wengi tu sasa hivi ni madiktar katika hospitali za hapahapa nchini, wengine mainjia wazuri tu na wanasaidia mambo mbalimbali.


ata>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hata

apo>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hapo

ayo>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hayo

iyo>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hiyo

ili>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hili

ivyo>>>>>>>>>>>>>>>>>>hivyo

nimwahi kua moja wa.................nimewahi kuwa mmoja wa

Naona kweli hapo FEZA msisitizo ulikuwa ni English zaidi......lakini pamoja na hayo nimelipenda andiko lako...Hata hivyo kumbuka kwa maeneo mengi duniani mafunzo ya kigaidi huwa hayatolewi wazi wazi, ila points zako nyingi katika andiko hili ni za msingi....
 
hoja zote sawa lakini ajira ya walimu imenikwaza. wawekezaji wanatakiwa kuleta wataalamu ambao hatuna hapa nchini. kumbe hata walimu hatuna mpaka wanaletwa toka uturuki? na vibali vya ajira wanavyo au wana visa za utalii?
 
ata>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hata

apo>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hapo

ayo>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hayo

iyo>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hiyo

ili>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>hili

ivyo>>>>>>>>>>>>>>>>>>hivyo

nimwahi kua moja wa.................nimewahi kuwa mmoja wa

Naona kweli hapo FEZA msisitizo ulikuwa ni English zaidi......lakini pamoja na hayo nimelipenda andiko lako...Hata hivyo kumbuka kwa maeneo mengi duniani mafunzo ya kigaidi huwa hayatolewi wazi wazi, ila points zako nyingi katika andiko hili ni za msingi....
kwani sheria mojawapo humu jf ktk kuandika comments lazima uandike kwa kiswahil fasaha?? Mstake kutuzingua si mngekuwa bas maprofesa wa kiswaili au tuki
 
Najua Shule imekupiga chenga lakini basi hata kudodosa huwezi? Tafsiri na tafakuri hili aliosema mkatoliki mwenzako, Mahiga "walimu wa shule za FEZA ambao ni raia wa Uturuki wamekuwa wakitumia mbinu za kigaidi kufundisha wanafunzi".


Mkuu Barghash bin sayyid ametopea kwenye ujinga, think outside the box,binafsi siamini kama Feza schools zinafundisha ugaidi no way hizi body binafsi za Erdogan na mdhamini wake wa siku nyingi Imani Fetullah Guleh ,kama file ni ugaidi basi Erdogan ni ugaidi pia haiwezekan miaka yote washirikiane mpaka 2013 alarm Guleh uanze kuwa ugaidi uzeeni.mwisho soon kama kuwa na ushindani,wa shule ni jambo uwe ya Kanisa au msikiti,hizo shule za Kanisa unazoponda ndiyo wanao wanasoma
 
Ilisadikika lile.Zoez la mapinduz aliliandaa huyo hyo raisi aliepo mafalakan.Kama njia ya kuaminisha umma kuhusisha na hawa wamirik.Ambao wanamirik shule na vyuo.Zaid ya 200/dunian sioni mantik yake
 
Mambo yao ya ndani wasiyalete kwetu

emalau;
Wameyaleta kwetu kivipi mkuu?? Wamekosea kutushtua kuwa tuwe macho?? Hujui ni rahisi zaidi kuuimarisha huo ugaidi kwa kutumia lango la biashara?? Hujui ni rahisi zaidi kuwapata mamluki tena wachanga kabisa kwa kutumia darasa??
Nadhani tumuunge mkono mh. Mahiga kuwa kama ushahidi upo, tusichelewe kuchukua hatua. Mh JPM aliwahi kusema kuwa, Kama ushahidi upo wazi nini kinangojewa hatua isichukuliwe??
Namuunga mh Mahiga mkono. Waturuki, leteni ushahidi, mficha maradhi mauti itamuumbua. Hata zipasishe Div. I wooote, ka ni magaidi ni hatari kwa kizazi chetu. Umaskini wetu usituuzie mauti.
 
Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone

Kama ni kweli basi Serikali ya Uturuki inafadhili ugaidi duniani. Siku zote hizo mbona hawakutufahamisha kwamba walimu kutoka Uturuki wanafundisha watoto wetu ugaidi?

Na kiongozi wa mapinduzi yaliyoshindwa huko Uturuki yuko Marekani, nchi ambayo ipo mstari wa mbele kupigana na ugaidi duniani. Mbona Marekani haijamshughulikia kiongozi huyo siku zote hizo alipokuwa Marekani kama kweli ni kiongozi wa ugaidi?
 
Haya mambo yanataka utaalamu kuya prove wrong or right. Kuna mplalestina mmoja alifanya PhD ya jinsi katuni zinavyotumika kujenga mitazamo ya watoto huko Gaza na West bank nilichoka. Kwa juu juu huwezi ku sense kitu chochote. Kuna katuni za west na za wale sijui wanamgambo ni shida
Nadhani Ni Wanafunzi Waliosoma FEZA tu pekeyao Ndiyo Wenye Haki Kamili Hapa Ya Kuja Kututhibitishia Hayo Madai Yaliyotolewa Ya Kuwa Walimu Wanatumia Njia Za Kigaidi Kufundishia Je Ni Kweli? Njooni Mutupe Ushuhuda...
 
Hizi shule nimesikia ni za mtu mmoja mturuki aishie US. US wamewaambia uturuki kama kuna ushaidi amehusika kwenye jaribio la mapinduzi watamkabidhi uturuki. But naelewa kwa nini shule zake zinakuwa attacked. Watoto ni zana nzuri ya mabadiliko. Watakuwa na woga kuwa ana preach chuki mashuleni
 
Hizi shule nimesikia ni za mtu mmoja mturuki aishie US. US wamewaambia uturuki kama kuna ushaidi amehusika kwenye jaribio la mapinduzi watamkabidhi uturuki. But naelewa kwa nini shule zake zinakuwa attacked. Watoto ni zana nzuri ya mabadiliko. Watakuwa na woga kuwa ana preach chuki mashuleni
Hizi shule sio za mmiliki mmoja ila wamiliki wame be inspired na movement ya huyo Sheikh katika kutoa huduma(hizmet), anaamini katika kutoa huduma for the sake of God na akaanzia kuwaambia wafuasi wake wawekeze kwenye elimu, afya, na huduma nyingine za kijamii.
Huyu mtu anaishi uhamishoni tangu 97 na hana hata haja ya kujua shule hizo zinaingiza faida au la
 
Ugomvi wa gullen na endorgan ulianza mwaka 2013 hasa baada ya wafuasi wa gullen kuibua scandal ya rushwa dhidi ya baadhi ya mawaziri wa endorgan na pia mtoto wa endorgan,hiyo scandal ikapelekea mawaziri wa endorgan kupigwa chini,endorgan akamshutumu gullen kuwa ndo amechochea hiyo scandal ili kumwangusha yeye endorgan.
Scandal ilihusika na baadhi ya maofisa kuvikiuka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya iran,vilivyowekwa na marekani,
iligundulika hao maofisa akiwemo mtoto wa endorgan wakifanya biashara na iran kwa siri,kwa kubadilishana mafuta na gase toka iran kwa dhahabu,inawezekana gulen alipewa siri na wamarekani ili alisanue,toka hapo ndo gullen akaitwa ni gaidi wa kuiba siri nyeti na kuzianika hadharani kwa lengo la kumpindua Endorgan.
Gülen was once an ally of President Recep Tayyip Erdoğan, but the relationship fell apart when the latter accused the cleric of “ trying to topple him” in December 2013. Gülen has lived in the U.S. since 1999, when he fled the then-government on “charges of anti-secular activities.”
Reuters readthe indictment, which states the cleric “is the number one suspect among 69 people accused of running a ‘terrorist group’ behind 2013 corruption investigations.” Authorities targeted Erdoğan’s inner circle and led to their dismissal.
All of the suspects face life imprisonment, but Gülen faces a number of additional charges, since authorities believe him to be the mastermind of the alleged terrorist group. The indictment sayshe formed and led the group and obtained “secret information for the aim of political espionage.”
“We have gone into their lairs, and we will go into them again,” Erdoğan declared last year. “Whoever is beside them and behind them, we will bring down this network and bring it to account.”
Authorities have targeted anyone connected to Gülen, which led to failing businesses and people losing their jobs. One of the largest banks in Turkey lost its prominence. Critics of Erdoğan, not necessarily connected to Gülen, accused him of using the controversy “to reshuffle the judiciary system in his favor and crack down on dissent.” Erdoğan has a history of shutting down anyone, including kids, who dares insultor questionhis motives.
Erdoğan man[emoji27]
 
inaonekana kuwa Gullen ni plan B ya obama,baada ya arab spring kushindikana,
ukiangalia uislamu wa huyu Gullen ni ule unahimiza elimu,yaani kujenga mashule,inovation,business na ni pro west,
sasa wamarekani walikuwa wanaanda huyu mtu akamate madaraka uturuki baada yua kuona endorgan ni too radical.
Na kutoka uturuki taratibu ushawishi wa uturuki ungeenda unaenea taratibu syria,iraq,yemen,lebanon etc,ambao ungekuwa friendly to west.

Sasa naona deal limefail vibaya sana
Source please
 
Unamaanisha Waturuki wazushi
Huyu uelewa wake ni mdogo, akili yake imemtuma dini fulani inaonewa hapa, ili hali sisi (Tz) ndio tumewataka ushahidi, kwa maana ingine tumenusa uzushi juu ya madai yao, sasa kaibuka huyo wa upande moja kutokuwa na haki, sijui kala maharage ya wapi huyu, tumsamehe, uwezo wake umeishia hapo
 
Back
Top Bottom