Waziri Makamba ana "traits" za kuwa Rais baada ya Samia. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Waziri Makamba ana "traits" za kuwa Rais baada ya Samia. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Ni sifa njema kufananishwa na January,ni dhahiri ana uwezo ambao wewe na unadhani anao mnahofia.

Ndio maana hamna hoja mna vioja vya matusi.
Nje ya mada kidogo:

Mimi naamini kundi kubwa la watanzania "tuna uwezo mdogo".

Tuna uwezo mdogo wa kiakili.
Tuna uwezo mdogo wa kifedha.
Tuna uwezo mdogo kwenye mambo mengine meeengi sana.

Hali hiyo inatupelekea tuwe watu wa "jumla jumla" na "juu juu".

Tunakosa ufanisi na ubobevu katika karibia kila tunalolitenda.

Hatuna ufanisi na ubobevu kwenye kilimo, biashara, uchimbaji, uvuvi, ufugaji, elimu, mijadala na mambo mengine "chungunzima".

Tazama kama hapa JF, ni members wachache sana wanaweza kujadili jambo (lolote lile) kwa hoja. Iwe ni kwenye Michezo, Mahusiano, Biashara, Siasa, n.k

Nimefuatilia uzi wako tangu mwanzo, naona ni wachache sana au hakuna kabisa anayeweka hoja mezani kukupinga katika mawasilisho yako.

Wengi wetu "tumejikita" katika "jumla jumla na juu juu" tu....

Mara oooh uwaziri umemshinda, mara aliiba mtihani, mara awe Rais wa wasafi, mara wewe chawa wake, mara ooh bora tumpe huo Urais Steve Nyerere, mara tunataka Mkristo, n.k .....
Hivi vitu wewe umeviita "Nonsense".

Mimi nitaviita ndio utanzania wenyewe.

Safari ni ndefu sana.
 
Duh kwa hiyo wewe ndo kipimo Cha kuona nani anafaa kuwa rais!
 
Hili ni tatizo kubwa Sana la Watanzania,na ni matokeo ya mfumo uliotulea.

Na watu wenye uwezo wanakuwa wahanga wa hili kundi kubwa la wajinga.

Ona hapa jukwaani unamwambia mtu apinge kwa hoja analeta hisia binafsi za chuki kwa sababu ambazo hazieleweki..

Kwa Tanzania hii watu wengi wenye uwezo wanashindwa kuonyesha talent zao kwa sababu jamii kubwa ni ya wajinga na wapuuzi..
 
utapigwa mawe balaa....lakini ukweli ni kwamba dogo kichwa iko vizuri, amelelewa vizuri na inaonekana mamentor wake walikuwa wazuri..huwezi kumfananisha na vijana wengi wa umri wake walio kwenye mfumo au nje ya mfumo..

Mapungufu kila binadamu anayo...
Hebu tueleze uzuri wa makamba upo kwenye nini, wengi mnazungumza jumlajumla tu hamsemi kichwa kipo vizuri wapi.
Lakini huyuhuyu makamba mnaesema yupo vizuri kichwani alifutiwa matokeo galanos kwa kashfa ya kuiba mitihani.
 
Mkuu, waziri kutahadharisha hivyo ndilo hilo linakua ni kosa la January Makamba ?

Huwa naona serikali nyingi duniani huwa zinawatahadharisha wananchi wake kwenye mambo mbalimbali. Kumbe ni kosa.
Huna uwezo wa kuelewa nilichoandika hapo.Serikali kazi yake ni kutatua changamoto za wananchi na wala siyo kuwatahadharisha wananchi kuwa wakae tayari kuumizwa na changamoto.
 
Huna uwezo wa kuelewa nilichoandika hapo.Serikali kazi yake ni kutatua changamoto za wananchi na wala siyo kuwatahadharisha wananchi kuwa wakae tayari kuumizwa na changamoto.
Kumbe "sina uwezo" wa kuelewa ulichokiandika, ooooh okay basi sawa.

Inaelekea mkuu umeandika kitu kigumu sana kueleweka.

Lakini pia hapo chini umesema "sio jukumu la serikali kuwatahadharisha wananchi"

Kwahiyo hilo lilipaswa kuwa ni "siri ya serikali" ?

Maoni yangu ya jumla, pamoja na kwamba umenituhumu kwamba siwezi kuelewa "jambo gumu" uliloliandika, ni kwamba, serikali inapaswa kuwaeleza wananchi juu ya hatari zinazokuja.
Wakati huo huo inatakiwa kuendelea na majukumu yake ya kuzikabili changamoto hizo.

Serikali inapaswa kuwaambia wananchi wake kwamba kuna tishio la kupanda kwa bei ya mafuta, lakini pia kuwaambia (watu hao) inachukua hatua gani ili kukabiliana na hali hiyo.

Inatakiwa kufanya hivyo kwenye matishio ya usalama, milipuko ya magonjwa, hali mbaya ya hewa (ukame, mafuriko, vimbunga, n.k) pamoja na madhila mengineyo mengi.

Kama kweli tunaamini katika "uwazi" kama kiambata muhimu cha "utawala bora", tunapaswa kuwa na serikali ya namna hiyo.

Vinginevyo, labda uthibitishe kwamba serikali ikisema kwamba kutakua na ongezeko la bei ya mafuta, kauli inakua imemaanisha kwamba serikali kamwe haitojihusisha na juhudi zozote za kuhakikisha inapunguza makali ya athari za kupanda kwa bei ya mafuta.

NB:
In the meantime, tuendelee kuamini kwamba "sisi" tunaandika vitu vigumu sana ambavyo "wengine" hawawezi kabisa kuelewa.
 
Serikali inapaswa kuwaambia wananchi wake kwamba kuna tishio la kupanda kwa bei ya mafuta, lakini pia kuwaambia (watu hao) inachukua hatua gani ili kukabiliana na hali hiyo.
Sasa ulivyopinga kuwa nisimkandie Makamba,ni wapi ametueleza hatua ambazo Serikali itachukua ili kukabiliana na changamoto aliyotutahadharisha?
 
Kuwa rais wa kitu gani?
Rais wa chama cha wasanii; kwani kuna tatizo.

Yeyote anayeandaliwa kuwa rais wa serikali yoyote huwa anavurunda sana awapo madarakani kwani huwa ni mtu asiye na uwezo, ndiyo maana nguvu inatumika kumuandaa. Wenye uwezo huwa hawaandaliwi bali huwa wanajiandaa automatically.

Chema chajiuza, na kibaya chajitemebeza!!

Kwenye list ya cabinet ya mama, bado sijaona presidential material hasa; labda Kassim Majaliwa tu. Najua kuna wasiomwona hivyo, lakini ni mchapa kazi na mfuatiliaji mzuri sana asiye na makundi wala wa kujikweza kuliko hao wanaojiita wenye chama chao.
 
Kitendo cha kutumia hii style ya propoganda zilizo muweka madarakani JK mwaka 2005 tayari inaonesha sio smart hata kidogo. Tanzania imekuwa na watu wenye ufahamu wa hali ya juu zaidi sana miaka hii kuliko hiyo.

Ili uwe Rais wa JMT kwa sasa lazima ujitenge na JK kwa maana ya baadhi ya mambo yaliyo fanyika kwenye utawala wake haijalishi ushindi kwenye sanduku la kura unapatikana vipi? Hata JPM alilijua hilo na alilifanyia kazi. Ndio yale maneno "mijizi."

Bahati mbaya huyu mwenzetu na wengine wa aina yake ile mbereko inawabeba na wanaitegemea mpaka leo. Hawawezi kusimama wenyewe wahesabiwe na Watanzania. Wataambulia huo uwaziri na nafasi nyengine za miaka miwili mitatu. Ushauri wangu watumie vizuri urefu wa kamba walizo pewa na kwa uangalifu wasiache nyayo. Historia huwa inajuriduia atatokea JPM mwingine chaguzi si nyingi zijazo.
 
Kwa jamii kama ya tz tunahitaji kiongozi wa juu awe anti establishment... Makamba anaonekana kuelemea kwa tabaka fulani hivi less popular. Kwa mtanzania wa kawaida hafai. Interest groups zitamwendesha.
 
Bila kupoteza muda.

Ni hivi ukiangalia Baraza lote la Mawaziri la sasa mwanasiasa pekee mwenye ushawishi na mwenye traits za kuwa Rais ni January Makamba.

He seems to be well informed,anajiamiji,interactive na kichwani ni smart na anajua kuongea na kupangilia mambo.Kiufupi yuko smart na ana exposure ya kutosha.

Sio mtu wa mihemko wala kuendeshwa kirahisi rahisi na pressure za kisiasa.

Nimekuja kufuatilia kwa nini watu wanamshambulia nimegundua ni vile anaonekana ni tishio kwa walio wengi kwenye Urais baada ya Samia.

Jana alikuwa live kwenye kipindi cha mwaka mmja wa Rais akielezea mafanikio, changamoto na dira ya Wizara ya Nishati.

Maswali yote yanayoulizwaga humu jukwaani Kuhusu kukatika kwa umeme,sijui kuchelewesha Bwawa and such nonsense ameyajibu kwa weledi na evidences kabisa ndio maana hadi saizi huwezi akina Msukuma na genge lake wakiwa na hoja.

Swala la kwa nini awamu iliyopita umeme ulikuwa haukatiki uje kukatika sasa amelijibu vyema kabisa tena akaja na Takwimu na history ya masuala ya umeme.

Kwa jinsi nilivyomtathmini ni wazi anafaa kumrithi Samia,sijaona mtu mwingine yeyote wa kumzidi labda kwa mbali Mwigulu anaweza kumsogelea but Mwigulu ana ego na majivuno Sana.

Ngoja tuone mda utasema.

Katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM mwaka 2015, walijitokeza wagombea wengi sana. January Makamba aliweza kuingia katika orodha ya tano bora huku majina makubwa ya makada wazoefu yakienguliwa kabla yake.

Jambo hili linadhihirisha jambo moja, pamoja na uchanga wake kwa wakati ule ndani ya chama chake, January bado alikuwa na ushawishi mkubwa. Kwa sasa bado anazidi kujijenga na kujiimarisha zaidi.

Licha ya kupata dhoruba ya kisiasa wakati ule wa JPM, pale alipodukuliwa akimteta kwa kumbagaza aliyekuwa bosi wake na hatimaye kuondolewa katika baraza la mawaziri. Lakini jambo hilo halikuweza kumtoa na kumtupa nje wa wigo wa siasa ndani ya chama chake.

Wote tunaiona "come back" yake, pale alipoitwa tena na Rais SSH kuhudumu katika wizara nyeti ya nishati. January si yule tena wa mwaka 2015, kwa sasa ni mwenye kujiamini, uthubutu, ubunifu, sifa ya mchapa kazi, sifa za ukweli na uwazi, mjengaji mzuri wa hoja, kutafuta kujifunza, kutokuishi kwa mazoea, sifa ya kuchukua hatua pale panapostahili ikiwemo kuwawajibisha wabadhirifu wa mali za umma na sifa nyingine za kadhaa.

January anaungwa mkono na viongozi wengi wastaafu, wazee wa chama na hata mfumo uliopo. Hii ndiyo sababu kubwa ya chuki za mahasimu wake dhidi yake. Huyu na Dr. Emmanuel Nchimbi ndiyo vipenzi wa mfumo, lakini January ana sifa ya ziada ya kuwa ni mzao wa baba ambaye ni Muislamu - BAKWATA na mama amvaye ni Mkristu - Mkatoliki.

But all in all, CDM ipo tayari kutwaa na kushika dola mwaka 2025. Hayo ya ngoswe tunawaachia ngoswe wenyewe.
 
Sasa ulivyopinga kuwa nisimkandie Makamba,ni wapi ametueleza hatua ambazo Serikali itachukua ili kukabiliana na changamoto aliyotutahadharisha?
Mkuu, haki ya kutoa maoni hasi kwa kiongozi wa nchi yako ni ya kwako na hakuna anayeweza kuichukua haki hii.

Comment yangu haiathiri kabisa msimamo wako, ila nilikua "nahoji tu" kwamba je, haumkubali kiongozi huyo kwa sababu tu alitoa hiyo tahadhari ?

Nikafika mbali kwa kutanabaisha kwamba mbona duniani kuna viongozi wengi tu huwa wanatoa tahadhari kwa wananchi wao juu ya kadhia kadha wa kadha ? Je, hili kwako linabaki kuwa ni kosa as simple as that, au ni kwa huyu waziri tu ?

Mimi sifahamu hiyo habari umeitoa kwenye source gani na sijui kwa undani wake kama ilijumuisha maneno ya waziri juu ya je, kuna mikakati gani juu ya suluhu ya changamoto hiyo au hakuligusia kabisa hilo.

Kamwe siwezi kuupinga "msimamo" wako, ila ninaweza "kuhoji au kupinga hoja zako".
 
Katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM mwaka 2015, walijitokeza wagombea wengi sana. January Makamba aliweza kuingia katika orodha ya tano bora huku majina makubwa ya makada wazoefu yakienguliwa kabla yake.

Jambo hili linadhihirisha jambo moja, pamoja na uchanga wake kwa wakati ule ndani ya chama chake, January bado alikuwa na ushawishi mkubwa. Kwa sasa bado anazidi kujijenga na kujiimarisha zaidi.

Licha ya kupata dhoruba ya kisiasa wakati ule wa JPM, pale alipodukuliwa akimteta kwa kumbagaza aliyekuwa bosi wake na hatimaye kuondolewa katika baraza la mawaziri. Lakini jambo hilo halikuweza kumtoa na kumtupa nje wa wigo wa siasa ndani ya chama chake.

Wote tunaiona "come back" yake, pale alipoitwa tena na Rais SSH kuhudumu katika wizara nyeti ya nishati. January si yule tena wa mwaka 2015, kwa sasa ni mwenye kujiamini, uthubutu, ubunifu, sifa ya mchapa kazi, sifa za ukweli na uwazi, mjengaji mzuri wa hoja, kutafuta kujifunza, kutokuishi kwa mazoea, sifa ya kuchukua hatua pale panapostahili ikiwemo kuwawajibisha wabadhirifu wa mali za umma na sifa nyingine za kadhaa.

January anaungwa mkono na viongozi wengi wastaafu, wazee wa chama na hata mfumo uliopo. Hii ndiyo sababu kubwa ya chuki za mahasimu wake dhidi yake. Huyu na Dr. Emmanuel Nchimbi ndiyo vipenzi wa mfumo, lakini January ana sifa ya ziada ya kuwa ni mzao wa baba ambaye ni Muislamu - BAKWATA na mama amvaye ni Mkristu - Mkatoliki.

But all in all, CDM ipo tayari kutwaa na kushika dola mwaka 2025. Hayo ya ngoswe tunawaachia ngoswe wenyewe.
Wenye wivu na chuki watapinga.
 
Kwanza akatafute ile Crane...., Hayo Mengine Baadaye
 
Hebu tueleze uzuri wa makamba upo kwenye nini, wengi mnazungumza jumlajumla tu hamsemi kichwa kipo vizuri wapi.
Lakini huyuhuyu makamba mnaesema yupo vizuri kichwani alifutiwa matokeo galanos kwa kashfa ya kuiba mitihani.

Kila aliyevizuri kichwani lazima afanye vizuri darasani kwa kufaulu mtihani..!
 
Back
Top Bottom