Waziri Makamba ana "traits" za kuwa Rais baada ya Samia. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Waziri Makamba ana "traits" za kuwa Rais baada ya Samia. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

"nahoji tu" kwamba je, haumkubali kiongozi huyo kwa sababu tu alitoa hiyo tahadhari ?
Nimemkataa kwa sababu ya kutoa tahadhari bila hatua.

Kwetu sisi wananchi hatua ni muhimu kuliko tahadhari ndiyo maana tunalipa kodi kwa ajili ya changamoto zetu zitatuliwe,kwa hiyo nilitegemea nione hatua kabla ya tahadhari.
 
Katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM mwaka 2015, walijitokeza wagombea wengi sana. January Makamba aliweza kuingia katika orodha ya tano bora huku majina makubwa ya makada wazoefu yakienguliwa kabla yake.

Jambo hili linadhihirisha jambo moja, pamoja na uchanga wake kwa wakati ule ndani ya chama chake, January bado alikuwa na ushawishi mkubwa. Kwa sasa bado anazidi kujijenga na kujiimarisha zaidi.

Licha ya kupata dhoruba ya kisiasa wakati ule wa JPM, pale alipodukuliwa akimteta kwa kumbagaza aliyekuwa bosi wake na hatimaye kuondolewa katika baraza la mawaziri. Lakini jambo hilo halikuweza kumtoa na kumtupa nje wa wigo wa siasa ndani ya chama chake.

Wote tunaiona "come back" yake, pale alipoitwa tena na Rais SSH kuhudumu katika wizara nyeti ya nishati. January si yule tena wa mwaka 2015, kwa sasa ni mwenye kujiamini, uthubutu, ubunifu, sifa ya mchapa kazi, sifa za ukweli na uwazi, mjengaji mzuri wa hoja, kutafuta kujifunza, kutokuishi kwa mazoea, sifa ya kuchukua hatua pale panapostahili ikiwemo kuwawajibisha wabadhirifu wa mali za umma na sifa nyingine za kadhaa.

January anaungwa mkono na viongozi wengi wastaafu, wazee wa chama na hata mfumo uliopo. Hii ndiyo sababu kubwa ya chuki za mahasimu wake dhidi yake. Huyu na Dr. Emmanuel Nchimbi ndiyo vipenzi wa mfumo, lakini January ana sifa ya ziada ya kuwa ni mzao wa baba ambaye ni Muislamu - BAKWATA na mama amvaye ni Mkristu - Mkatoliki.

But all in all, CDM ipo tayari kutwaa na kushika dola mwaka 2025. Hayo ya ngoswe tunawaachia ngoswe wenyewe.

Wewe ndio umefafanua neno mbereko vizuri sana na kwa mukhtaza huu wengi watalielewa vizuri sasa.

JPM alisimama akahesabiwa na wengi kwa utendaji wake kazi ule ambao marehemu Kingunge aliouita nyapara na Watanzania walimuhesabu na kumuelewa hivyo. Ndio maana si Kingunge mwenyewe na EL wake ama Makamba na mbereko yake walio weza kuishinda thamani kubwa ya sifa hii ya nyapara. Makamba na wengine wanao utamani Urais wa JMT wasimame wahesabiwe wakijua kuwa hata wawezeshaji wa ushindi watakuwa wakifanya kwa tahadhari akilini mwao ya msamiati huu mpya sabaya kwenye koridozi zao.
 
Hii zero ikija pewa urais wa JMT ndio siku sitataka tena kujulikana ni mbongo.. hii ni seti tupu iliojaa kiburi na majigambo, na inalindwa na msoga otherwise ingekua huko jalalani sasa hivi. Jimbo lake lipo hoi bin taaban, uje wizara sasa ndio hio umeme wa mgawo na huyo hangaya hana la kufanya maana remote ya kuongoza nchi ipo msoga. Bila figisu figisu kwenye uchaguzi wa 2025 , Mbowe akigombea urais Chadema inachukua kiulaini sana watu wamewachoka CCM ni basi tu.
 
vice versa is true...ni bogus sema mfumo unamfanya aonekane ni smart and visionary...
Inawezekana ni disposition yake ndo inamfanya aonekane au ku act smart.......siwezi jua, labda wakubwa wanaomfuatilia kwa karibu wanaweza judge.
 
Huyu jamaa namuona anakiburi na majivuno sana
Inawezekana wewe una low self-esteem ndiyo maana unamuona January kama mjivuni...ukiulizwa ni wapi na wapi ameonyesha kiburi na ujivuni pengine ukashindwa kutoa mfano....

Kuna mtu nilimuuliza somewhere kwa nini anamtuhumu January kujiona kama Obama....akabaki ana unyaunya tu...nikamuuliza au ni clothing style ya kukunja mashati, who says kwamba that style belongs to Obama pekee, wengine wasifanye...alikosa hoja....

Tuache tabia ya kuchukia watu bila sababu za msingi, ni aina flani ya uchawi, sadly...
 
Wakati flani Mh VP Mpango akilalama kuwa Mh Rais SSH anachoshwa anapelekewa mafaili yaliyo kiuka utaratibu ooh sijui wako wanao lala hata kukiuka taratibu za protokali ya ratiba, nk. Kwa Tanzania ilivyo sasa iko siku isiyojulika majina yao yatawekwa wazi tu.
 
Ni vyema kuchagiza na picha za matukio mbalimbali ili kuonyesha kiongozi anayekubalika na wazee wa chama chake. Si kila mtu anaweza kupata fursa kama hizi.
Screenshot_20220325-150409.jpg
Screenshot_20220325-152009.jpg
Screenshot_20220325-153253.jpg
Screenshot_20220325-153130.jpg
Screenshot_20220325-152143.jpg
Screenshot_20220325-145925.jpg
 
Ni vyema kuchagiza na picha za matukio mbalimbali ili kuonyesha kiongozi anayekubalika na wazee wa chama chake. Si kila mtu anaweza kupata fursa kama hizi.View attachment 2164017View attachment 2164018View attachment 2164019View attachment 2164021View attachment 2164022View attachment 2164023

Hiyo picha ya kwanza tukumbushe Jinsi Mzee Mwinyi alivyongaka alipojua inataka kutumiwa kwenye propoganda inayo weza kumharibia Mh Rais Mwinyi jr ili uweze kuubalansisha hii habari yako. Na usisahau hotuba za Mwl Nyerere ziko nyingi sana za kuwafanya null and void.
 
Hiyo picha ya kwanza tukumbushe Jinsi Mzee Mwinyi alivyongaka alipojua inataka kutumiwa kwenye propoganda inayo weza kumharibia Mh Mwinyi jr ili uweze kuubalansisha hii habari yako. Na usisahau hotuba za Mwl Nyerere ziko nyingi sana za kuwafanya null and void.
"Mzee Mwinyi aling'aka pale alipohisi kuwa matumizi ya picha yake inaweza kutumiwa kwenye propoganda inayoweza kumharibia Mh Mwinyi Jr"

Ni kweli kabisa, hayo yote yalitokea katika kipindi ambacho sauti za kina Makamba zilipodukuliwa zikihusishwa na kumnanga bwana mkubwa. Kwa hiyo Mzee Mwinyi hakupenda kabisa kuonekana kuwa yupo kinyume na JPM kutokana na maslahi ya kisiasa kwa familia yake.



Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hivi huyu makamba ana sifa gani za kuiongoza Tanzania.....MTU pekee mwenye sifa ya urais ni Hussein Mwinyi. He is smart na msikivu.

Chukulia makamba eti anaviongoza vyombo vya ulinzi na usalama....

Chukulia makamba aliyeshindwa kuiongoza tanesco aje aongoze nchi.

Makamba Jr
Mwigulu
Kigwangalla
Nape
Kikwete Jr
Hao wote hawafai maana hawana good code of conduct. Urais sio uhuni na sifa za kujifanya unajua kiingereza.
Urais ni huduma.
Urais ni hekima.
Urais ni uvumilivu.

Urais sio mitandao na media
 
"Mzee Mwinyi aling'aka pale alipohisi kuwa matumizi ya picha yake inaweza kutumiwa kwenye propoganda inayoweza kumharibia Mh Mwinyi Jr"

Ni kweli kabisa, hayo yote yalitokea katika kipindi ambacho sauti za kina Makamba zilipodukuliwa zikihusishwa na kumnanga bwana mkubwa. Kwa hiyo Mzee Mwinyi hakupenda kabisa kuonekana kuwa yupo kinyume na JPM kutokana na maslahi ya kisiasa kwa familia yake.



Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app

Gud gud, hizi picha za wakubwa hazimsaidii saanaa kwenye propogandaa maana wengi wanazijua, kitu chengine kinachoonesha jamaa sio smart kama anavyojifikiria na tunavyotaka kuaminishana.

Afanye hivi kama anataka kutumia mapicha picha kwenye propoganda zake. Wizara yake inazo kazi nyingi za field aende akapige picha huko akiwa anafanya monitoring and evaluation tour ya hiyo miradi. Akienda huko avalie field gears za huko sio mashati ya rangi ya pink ama maua ua yasiyo eleweka. Wanachi wa kawaida wakimuona hivyo aah nyo zao zitakuwa kwatu.

Ajifunze kwa Mh Rais SSH anavyo upiga mwingi. Inapo mbidi anavua ushungi/hijabu anavaa JWTZ camouflage uniform, huko ndiko kunaitwa kuwa smart na hali ya hewa.
 
Ni sahihi na hili ni tatizo kubwa Sana kwa Tzn,mnaweza poteza watu wenye uwezo kwa sababu za kijinga.

Ndio maana nikasema kwa analysis yangu hakuna wa kumfikia si PM wala Mwigulu au Bashungwa.

Landa second kwake ni huyo Mwigulu lakina bwana madelu ana sifa ya majivuno na anaeamini yeye ndio ana akili kuliko watu wote,madelu ni jamii ya Mwendazake hafai kuwa kiongozi mkubwa watu wengi wataumia.

Labda watu wengine wenye kaliba ya Makamba ni Bashe,Bashungwa na Mrisho Gambo na yule dogo Shaka Hamidu Shaka.The rest ni watu wa kawaida Sana.
Kuna watu very smart and competent sema tu wana keep low profile trying to hide their ambitions,ukiwa judge kwa mihemuko siyo rahisi kuwa identify.
Ingawa siyo vibaya mtu kuonyesha ambitions zake Ila it is to dangerous to be overambitious, take it from me.
 
Huyo jamaa akiwa raisi tumekwisha Tanzania connection yake ni ya hatari sana mpaka mchanga utabebwa upelekwe ulaya
 
Gud gud, hizi picha za wakubwa hazimsaidii saanaa kwenye propogandaa maana wengi wanazijua, kitu chengine kinachoonesha jamaa sio smart kama anavyojifikiria na tunavyotaka kuaminishana.

Afanye hivi kama anataka kutumia mapicha picha kwenye propoganda zake. Wizara yake inazo kazi nyingi za field aende akapige picha huko akiwa anafanya monitoring and evaluation tour ya hiyo miradi. Akienda huko avalie field gears za huko sio mashati ya rangi ya pink ama maua ua yasiyo eleweka. Wanachi wa kawaida wakimuona hivyo aah nyo zao zitakuwa kwatu.

Ajifunze kwa Mh Rais SSH anavyo upiga mwingi. Inapo mbidi anavua ushungi/hijabu anavaa JWTZ camouflage uniform, huko ndiko kunaitwa kuwa smart na hali ya hewa.
Mkuu, kazi kubwa ya waziri ni kusimamia sera zinazosimamia uendeshaji wa wizara yake. Kwa kushirikiana na katibu mkuu na wataalamu wa wizara hutoa mapendekezo ya uboreshaji wa sera zilizopo ama kubuni mpya ili wizara anayoisimamia iendeshwe kwa ufanisi.

Tunategemea waziri atumie "abstract skills" zaidi huku wasaidizi wake wa karibu wakitumia "administrative skills" lakini wale watumishi wa chini ndiyo haswa hutumia "technical skills" kwa kuwa wao ndio muda mwingi huwa "field". Sasa kumtaka waziri aende "field" huku akiwa amevaa "protective gears" inasaidia nini. Yeye anapaswa atumie muda wake mwingi akiwa ofisini, na aumize kichwa kuhusu jinsi ya kutatua changamoto zinazoikabili wizara yake.

Kuupiga mwingi hakuna maana kama hakuna magoli ya ushindi yanayofungwa. Kuupiga mwingi ni kufanya kazi kama timu moja yenye ari, hamasa na kiu kubwa ya kubadilisha mchezo na hatimaye kuleta ushindi. Waziri akitumia vyema "executive power" aliyokuwa nayo, kila kitu katika "field" kitafanyika kwa ufanisi mkubwa hata kama hatatoka ofisini kwake.



Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, kazi kubwa ya waziri ni kusimamia sera zinazosimamia uendeshaji wa wizara yake. Kwa kushirikiana na katibu mkuu na wataalamu wa wizara hutoa mapendekezo ya uboreshaji wa sera zilizopo ama kubuni mpya ili wizara anayoisimamia iendeshwe kwa ufanisi.

Tunategemea waziri atumie "abstract skills" zaidi huku wasaidizi wake wa karibu wakitumia "administrative skills" lakini wale watumishi wa chini ndiyo haswa hutumia "technical skills" kwa kuwa wao ndio muda mwingi huwa "field". Sasa kumtaka waziri aende "field" huku akiwa amevaa "protective gears" inasaidia nini. Yeye anapaswa atumie muda wake mwingi akiwa ofisini, na aumize kichwa kuhusu jinsi ya kutatua changamoto zinaikabili wizara yake.

Kuupiga mwingi hakuna maana kama hakuna magoli ya ushindi yanayofungwa. Kuupiga mwingi ni kufanya kazi kama timu moja yenye kuleta ushindi. Waziri akitumia vyema "executive power" aliyokuwa nayo, kila kitu katika "field" kitafanyika kwa ufanisi mkubwa hata kama hatatoka ofisini kwake.



Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app

Monitoring and evaluation hata kama unaletewa riport mezani ni lazima uende ukashuhudie unacholetewa. Wewe na huyo Mh Makamba unaye muandikia sijui kama mnajua hulka za Watanzania walio wengi.Usiongoze Watanzania kama unaongoza wale wazungu na waswahili wa Boston. Wako waliokuwa wanamuita Marehemu JPM mshamba kumbe anawajua watu wake Watanzania. Mlipeni Dr Slaa awasaidie mlipokengeuka kuhusu uongozi wa JPM hamna jinsi.
 
Nje ya mada kidogo:

Mimi naamini kundi kubwa la watanzania "tuna uwezo mdogo".

Tuna uwezo mdogo wa kiakili.
Tuna uwezo mdogo wa kifedha.
Tuna uwezo mdogo kwenye mambo mengine meeengi sana.

Hali hiyo inatupelekea tuwe watu wa "jumla jumla" na "juu juu".

Tunakosa ufanisi na ubobevu katika karibia kila tunalolitenda.

Hatuna ufanisi na ubobevu kwenye kilimo, biashara, uchimbaji, uvuvi, ufugaji, elimu, mijadala na mambo mengine "chungunzima".

Tazama kama hapa JF, ni members wachache sana wanaweza kujadili jambo (lolote lile) kwa hoja. Iwe ni kwenye Michezo, Mahusiano, Biashara, Siasa, n.k

Nimefuatilia uzi wako tangu mwanzo, naona ni wachache sana au hakuna kabisa anayeweka hoja mezani kukupinga katika mawasilisho yako.

Wengi wetu "tumejikita" katika "jumla jumla na juu juu" tu....

Mara oooh uwaziri umemshinda, mara aliiba mtihani, mara awe Rais wa wasafi, mara wewe chawa wake, mara ooh bora tumpe huo Urais Steve Nyerere, mara tunataka Mkristo, n.k .....
Hivi vitu wewe umeviita "Nonsense".

Mimi nitaviita ndio utanzania wenyewe.

Safari ni ndefu sana.
Ile tu kuendesha akaunti ya Kigogo14 umetosha kutompa sifa ya kuwa kiongozi bora.

Ni traitor mbaya kabisa......

Yeye angeendelea na uandishi wake wa hotuba za rais au aende kwenye makambi ya wakimbizi huko UNHCR ambayo ndiyo Proffesional yake halisi.

Tunajua tunachokiandika,usijipe ujaji wa JF.

commonmwananchi
10101.
2022.
 
Back
Top Bottom