Waziri Makamba avunja Kitengo cha Habari na Mawasiliano TANESCO kwa tuhuma za kushindwa kulisemea Shirika

Lakini hatushangai mwenye mamlaka ameshasema kila mtu ale urefu wa kamba yake so kinachoendelea tanesco hakitushangazi
 
Ndg January sihitaji kuandika reply ila hizo za juu zinatosha kuwakilisha maoni yangu kama mmoja wa Watanzania, ila isije kuwa kama ya ndg Ndugai.

NB; Acha niendelee kujifunza tabia ya binadamu!.
 
Mwandishi wetu,Arusha

Waziri wa nishati ,January Makamba ameagiza kuondolewa Mara moja afisa habari wa shirika la umeme nchini(Tanesco) huku akiagiza kuvunjwa kwa idara ya uhusiano wa shirika hilo na kuwekwa watu wapya.

Mbali na agizo hilo pia amegiza hatua za haraka zichukuliwe kwa watendaji ambao ni wazembe ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.

Waziri Makamba ametoa maagizo hayo Leo wakati alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha mkoani Arusha kilichopo Njiro jijini hapa na kukagua hali ya upatikanaji wa umeme mkoani hapa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.

Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Makamba alisema kwamba ifikapo Febuari mosi mwaka huu ateuliwe msemaji mpya wa shirika hilo.

"Ninaelekeza msemaji abadilishwe ifikapo febuari mosi mwaka huu achaguliwe mpya " alisema Makamba

Waziri Makamba alisema kwamba kumekuwa na changamoto kwa Tanesco kuwasiliana na wateja wake pindi umeme unapokatika ghafla hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko mengi na lawama kwa serikali.

"Tanesco lazima iwasiliane na wateja wake kwa wakati hii ni changamoto umeme unapokatika hivyo ni lazima wawasiliane na wateja wao kwa wakati" alisema Makamba

Hatahivyo,alisisitiza kuwa idara nzima ya uhusiano ndani ya shirika hilo lazima ivunjwe na wawekwe watu wapya wanaoweza kuendana na kasi na uweledi ndani ya shirika hilo.

"Mnawasikia wasemaji wa vilabu vya soka vya Simba na Yanga hivi mmeshamsikia msemaji wa Tanesco?" Alihoji Makamba

Hatahivyo,Makamba alisema kuwa serikali haifurahishwi na hali ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara na kuitaka Tanesco kutojificha nyuma ya mgongo wa waziri.

"Hatutaki waziri wa nishati ageuke kuwa msemaji wa shirika tumewaambia menejimenti wasijifiche nyuma ya wizara " alisisitiza Makamba

Waziri Makamba alisema kuwa serikali inakusudia kubadilisha mfumo teknolojia wa Luku ndani ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo wateja watakuwa wakinunua umeme moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na kisha kupata umeme bila kuweka tokeni.

"Mtu ananunua umeme kupitia simu yake ya mkononi na unaingia moja kwa moja kwenye mfumo na sio kuchukua tokeni na kwenda kuingiza kwenye mita" alisema Makamba

Alisema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu wateja wote takribani elfu 80 wanaosubiria kuunganishiwa umeme wataunganishiwa umeme huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kubadilisha mfumo wa maombi ya umeme ambapo utakuwa kupitia mtandao.

Waziri Makamba alibainisha kwamba serikali inakusudia kubadili mfumo wa usambazaji wa umeme kote nchini ili uendane na kasi ya ongezeko la wateja kwa kuwa mfumo uliopo kwa sasa ni wa kizamani.

Mwisho.

View attachment 2095358View attachment 2095359View attachment 2095360View attachment 2095361View attachment 2095362
😂😂😂😂 kwamba TANESCO inajificha nyuma ya Mgogongo wa Makamba. Sawa bana mie nausubiri muda tu.
 
Mr. Kigogo hiyo wizara ni kubwa mno kwako! Ni au, Bado unauota urais na umeamua kumfitini boss wako na au wafanyakazi wameamua kukuhujumu Kwa kuwa huna msaada kwao! Utakoma Kwa unafiki wako!
 
PASCAL MAYALA na HAJI MANARA kitenisi hicho mmerushiwa ,mkishindwa kukishambulia msimlaumu mtu
 
Mwandishi wetu,Arusha

Waziri wa nishati ,January Makamba ameagiza kuondolewa Mara moja afisa habari wa shirika la umeme nchini(Tanesco) huku akiagiza kuvunjwa kwa idara ya uhusiano wa shirika hilo na kuwekwa watu wapya.

Mbali na agizo hilo pia amegiza hatua za haraka zichukuliwe kwa watendaji ambao ni wazembe ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.

Waziri Makamba ametoa maagizo hayo Leo wakati alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha mkoani Arusha kilichopo Njiro jijini hapa na kukagua hali ya upatikanaji wa umeme mkoani hapa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.

Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Makamba alisema kwamba ifikapo Febuari mosi mwaka huu ateuliwe msemaji mpya wa shirika hilo.

"Ninaelekeza msemaji abadilishwe ifikapo febuari mosi mwaka huu achaguliwe mpya " alisema Makamba

Waziri Makamba alisema kwamba kumekuwa na changamoto kwa Tanesco kuwasiliana na wateja wake pindi umeme unapokatika ghafla hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko mengi na lawama kwa serikali.

"Tanesco lazima iwasiliane na wateja wake kwa wakati hii ni changamoto umeme unapokatika hivyo ni lazima wawasiliane na wateja wao kwa wakati" alisema Makamba

Hatahivyo,alisisitiza kuwa idara nzima ya uhusiano ndani ya shirika hilo lazima ivunjwe na wawekwe watu wapya wanaoweza kuendana na kasi na uweledi ndani ya shirika hilo.

"Mnawasikia wasemaji wa vilabu vya soka vya Simba na Yanga hivi mmeshamsikia msemaji wa Tanesco?" Alihoji Makamba

Hatahivyo,Makamba alisema kuwa serikali haifurahishwi na hali ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara na kuitaka Tanesco kutojificha nyuma ya mgongo wa waziri.

"Hatutaki waziri wa nishati ageuke kuwa msemaji wa shirika tumewaambia menejimenti wasijifiche nyuma ya wizara " alisisitiza Makamba

Waziri Makamba alisema kuwa serikali inakusudia kubadilisha mfumo teknolojia wa Luku ndani ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo wateja watakuwa wakinunua umeme moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na kisha kupata umeme bila kuweka tokeni.

"Mtu ananunua umeme kupitia simu yake ya mkononi na unaingia moja kwa moja kwenye mfumo na sio kuchukua tokeni na kwenda kuingiza kwenye mita" alisema Makamba

Alisema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu wateja wote takribani elfu 80 wanaosubiria kuunganishiwa umeme wataunganishiwa umeme huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kubadilisha mfumo wa maombi ya umeme ambapo utakuwa kupitia mtandao.

Waziri Makamba alibainisha kwamba serikali inakusudia kubadili mfumo wa usambazaji wa umeme kote nchini ili uendane na kasi ya ongezeko la wateja kwa kuwa mfumo uliopo kwa sasa ni wa kizamani.

Mwisho.

View attachment 2095358View attachment 2095359View attachment 2095360View attachment 2095361View attachment 2095362
Kipara hana jipya hiyo wizara haiwezi hata apewe miaka 100
 
Waziri wa Nishati Mh Makamba amevunja kitengo cha habari na mawasiliano Tanesco akikituhumu kimeshindwa kulisemea shirika na kulitetea shirika kwenye nyakati ambazo kitengo na watu wake kimetakiwa kufanya hivyo!

Ikumbukwe kitengo cha habari na mawasiliano kinaongozwa na mwana dada Babra Semu...kama sijakosea na kwa misingi hiyo amekali kuti kavu ...

Maswali ya kujiuliza...
Ni kweli kitengo hichi ndicho tatizo kwenye shirika?
Ni kweli wameshindwa kuitetea tanesco?
View attachment 2095460
Huo ni uonevu tu waziri kashindwa kusimamia umeme anakimbilia kumtumbua afisa habari.Makamba hamna kitu hapo tumepigwa watanzania.
 
Makamba anavyodai kitengo kimeshindwa kuitetea Tanesco ana maana gani? anataka kitengo kiwe kinazalisha propaganda au kifanyeje?

Navyojua hao watu wa idara ya habari wanatakiwa kupewa taarifa za majibu ya kero za wateja kutoka kwa wahusika (waziri, naibu wake, katibu mkuu nk) then wao ndio watangaze taarifa hizo kwa umma.

Sasa mfano wananchi wakiulizia ujio wa ile winchi ya tani 26 toka huko ilipoagizwa mbona mpaka leo kimya? Makamba anataka hao jamaa wa kitengo cha habari wajibu kitu gani kama hajawapa majibu?
Sio kutetea ni KULISEMEA,,, elewa kiswahili
 
Angeanza na Maharage.
Ni Kiri tu kwamba Kuna sehemu hapo jirani tu Kibaha , Kongowe kuanzia Ungindonu, mashine ya maji Hadi VETA mpaka Kigelo. Hili eneo kila ndani ya masaa. 24 Lazima umeme ukatike huu Sasa mwaka wa nne au wa tano.
Ikinyesha mvua kidogo tu hata ya mchongo lazima umeme ukatike.
Hebu meneja wa Kibaha ajieleze au ajiuzuru kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
 
Mwandishi wetu,Arusha

Waziri wa nishati ,January Makamba ameagiza kuondolewa Mara moja afisa habari wa shirika la umeme nchini(Tanesco) huku akiagiza kuvunjwa kwa idara ya uhusiano wa shirika hilo na kuwekwa watu wapya.

Mbali na agizo hilo pia amegiza hatua za haraka zichukuliwe kwa watendaji ambao ni wazembe ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.

Waziri Makamba ametoa maagizo hayo Leo wakati alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha mkoani Arusha kilichopo Njiro jijini hapa na kukagua hali ya upatikanaji wa umeme mkoani hapa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.

Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Makamba alisema kwamba ifikapo Febuari mosi mwaka huu ateuliwe msemaji mpya wa shirika hilo.

"Ninaelekeza msemaji abadilishwe ifikapo febuari mosi mwaka huu achaguliwe mpya " alisema Makamba

Waziri Makamba alisema kwamba kumekuwa na changamoto kwa Tanesco kuwasiliana na wateja wake pindi umeme unapokatika ghafla hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko mengi na lawama kwa serikali.

"Tanesco lazima iwasiliane na wateja wake kwa wakati hii ni changamoto umeme unapokatika hivyo ni lazima wawasiliane na wateja wao kwa wakati" alisema Makamba

Hatahivyo,alisisitiza kuwa idara nzima ya uhusiano ndani ya shirika hilo lazima ivunjwe na wawekwe watu wapya wanaoweza kuendana na kasi na uweledi ndani ya shirika hilo.

"Mnawasikia wasemaji wa vilabu vya soka vya Simba na Yanga hivi mmeshamsikia msemaji wa Tanesco?" Alihoji Makamba

Hatahivyo,Makamba alisema kuwa serikali haifurahishwi na hali ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara na kuitaka Tanesco kutojificha nyuma ya mgongo wa waziri.

"Hatutaki waziri wa nishati ageuke kuwa msemaji wa shirika tumewaambia menejimenti wasijifiche nyuma ya wizara " alisisitiza Makamba

Waziri Makamba alisema kuwa serikali inakusudia kubadilisha mfumo teknolojia wa Luku ndani ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo wateja watakuwa wakinunua umeme moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na kisha kupata umeme bila kuweka tokeni.

"Mtu ananunua umeme kupitia simu yake ya mkononi na unaingia moja kwa moja kwenye mfumo na sio kuchukua tokeni na kwenda kuingiza kwenye mita" alisema Makamba

Alisema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu wateja wote takribani elfu 80 wanaosubiria kuunganishiwa umeme wataunganishiwa umeme huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kubadilisha mfumo wa maombi ya umeme ambapo utakuwa kupitia mtandao.

Waziri Makamba alibainisha kwamba serikali inakusudia kubadili mfumo wa usambazaji wa umeme kote nchini ili uendane na kasi ya ongezeko la wateja kwa kuwa mfumo uliopo kwa sasa ni wa kizamani.

Mwisho.

View attachment 2095358View attachment 2095359View attachment 2095360View attachment 2095361View attachment 2095362
Yaleyale alisemaga watu walikuwa wanashindwa kufanya kazi sababu ya ukali unafiki mbaya mzee wa Schedule Maintenance.
 
Back
Top Bottom