Waziri Makamba avunja Kitengo cha Habari na Mawasiliano TANESCO kwa tuhuma za kushindwa kulisemea Shirika

Waziri Makamba avunja Kitengo cha Habari na Mawasiliano TANESCO kwa tuhuma za kushindwa kulisemea Shirika

Makamba anavyodai kitengo kimeshindwa kuitetea Tanesco ana maana gani? anataka kitengo kiwe kinazalisha propaganda au kifanyeje?

Navyojua hao watu wa idara ya habari wanatakiwa kupewa taarifa za majibu ya kero za wateja kutoka kwa wahusika (waziri, naibu wake, katibu mkuu nk) then wao ndio watangaze taarifa hizo kwa umma.

Sasa mfano wananchi wakiulizia ujio wa ile winchi ya tani 26 toka huko ilipoagizwa mbona mpaka leo kimya? Makamba anataka hao jamaa wa kitengo cha habari wajibu kitu gani kama hajawapa majibu?
Spot on.

Kwa kweli namkumbuka JPM, kwenye swala la umeme na kufanya kazi bila kupepesa macho nilimvulia kofia. Umeme ulikuwa sio tatizo, zile habari za ma-generator kila kona ya duka ziliisha. Hivi hawa viwavi hawashibi tu!
 
Makamba anavyodai kitengo kimeshindwa kuitetea Tanesco ana maana gani? anataka kitengo kiwe kinazalisha propaganda au kifanyeje?

Navyojua hao watu wa idara ya habari wanatakiwa kupewa taarifa za majibu ya kero za wateja kutoka kwa wahusika (waziri, naibu wake, katibu mkuu nk) then wao ndio watangaze taarifa hizo kwa umma.

Sasa mfano wananchi wakiulizia ujio wa ile winchi ya tani 26 toka huko ilipoagizwa mbona mpaka leo kimya? Makamba anataka hao jamaa wa kitengo cha habari wajibu kitu gani kama hajawapa majibu?
Unajua January hawezi hii wizara.....huku ni kuchanganyikiwa....
Ukiacha uwezo mdogo lakini pia ana laana ya kumtukana JPM....na bado.....
 
Waziri wa Nishati Mh Makamba amevunja kitengo cha habari na mawasiliano Tanesco akikituhumu kimeshindwa kulisemea shirika na kulitetea shirika kwenye nyakati ambazo kitengo na watu wake kimetakiwa kufanya hivyo!

Ikumbukwe kitengo cha habari na mawasiliano kinaongozwa na mwana dada Babra Semu...kama sijakosea na kwa misingi hiyo amekali kuti kavu ...

Maswali ya kujiuliza...
Ni kweli kitengo hichi ndicho tatizo kwenye shirika?
Ni kweli wameshindwa kuitetea tanesco?
View attachment 2095460
Makamba anakifua kivuli chake.
Halafu anaitwa January, si angegoja mwezi uishe?
Matatizo ya TANESCO hawezi kuyafutika, yatampigisha magoti!
 
Msemaji kama hapewi info za kutoa na wakubwa wake, inamuhusu nini!!!

Hataki kudanganya, sasa unamuondoa ili iweje!!

Waziri umechemka na maji moto yenye na degree 1000, umeongea mengi na wewe hujasema why tatizo lipo.

Umefeli as hao wote sio kiini, hawataki kutudanganya.

Mnakula tu kwa urefu wa kamba zenu.
Waziri mwenyewe mwizi wa mitihani pale Galanos sec. Tanga. Ashukuru baba yake alikuwa anauwezo wa kumpeleka huyu mwizi kule Forest Moro. Angekuwa mtoto wa mkulima leo angekuwa anauza machungwa kule Bumbuli.
 
Mbona bado mapema sana hadi kufikia mbuzi kuanza kula kamba zao wenyewe😀
 
Shirika Lina perform vibaya sana chini ya Magamba na Maharage. Badala ya wao kujitathmini wanamfukuza kazi msemaji.
Walitaka mama wa watu aseme umeme haukatiki au aseme tanesko hakuna rushwa au aseme hakuna mgao.
Lini tutaanza kuacha visingizio?
 
Huo ni uonevu tu waziri kashindwa kusimamia umeme anakimbilia kumtumbua afisa habari.Makamba hamna kitu hapo tumepigwa watanzania.
Waziri anasimamia umeme? 😁😁 Kivipi? Waziri ni kiongozi wa sera na hapa kafanya Kazi yake.

Tumepigwaje? Lini Tanesco walitoa sababu za msingi za umeme kukatika hovyo? Bado MD
 
Hapana ni kweli kwa nini umeme unakatika hovyo hakuna taarifa na hawasemi kuwaambia wananchi kuna nini umeme unakatika?

Lakini mkurugenzi mkuu anatakiwa kupewa onyo ,hawasimamii mameneja wa Mikoa.

Sio kweli bwana mbona huwa wanasema? Hawa wanabebeshwa lawana Tanesco ni mzigo mwingine
 
Mimi ni mpenzi wa Awamu ya 6, lakini Makamba is a let down.
Kukifuta kitengo cha habari ni kuingilia utendaji wa Management.
Angemfuta kazi CEO au Bodi nzima.
Kwani akija Waziri mwingine ndio inaenda kufunga nati kwenye karakana za Tanesco?

Waziri yuko sahihi kuwafuta Kazi hao wapuuzi.
 
Waongeaji wa kwenye majukwaa mbona wapo wengi wawachukue hao hata wale wa zamani waliopo Bungeni sasa wapewe hii kazi

Sisi ni bla bla tu na siku zinakimbia hahaha
 
Mimi ni mpenzi wa Awamu ya 6, lakini Makamba is a let down.
Kukifuta kitengo cha habari ni kuingilia utendaji wa Management.
Angemfuta kazi CEO au Bodi nzima.

Hahahaha hiki kitengo hata kiwe kizuri kama hakuna umeme ni kazi bure.... kuna muda wenye vitengo wanasikia aibu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapana ni kweli kwa nini umeme unakatika hovyo hakuna taarifa na hawasemi kuwaambia wananchi kuna nini umeme unakatika?

Lakini mkurugenzi mkuu anatakiwa kupewa onyo ,hawasimamii mameneja wa Mikoa.
Tanesco wsmrejeshe Mramba huyu Maharage wampe ubunge wa kuteuliwa akachape usingizi bungeni na covid 19.
Tanesco Ni kampuni kubwa sana sio sehemu ya kufanyia majaribio
 
Waziri anasimamia umeme? [emoji16][emoji16] Kivipi? Waziri ni kiongozi wa sera na hapa kafanya Kazi yake.

Tumepigwaje? Lini Tanesco walitoa sababu za msingi za umeme kukatika hovyo? Bado MD

Basi na MD afukuzwe
 
Anatafuta mchawi na wakati mchawi ni yeye mwenyewe, alitaka wawe wanatudangany?

Mpaka huyo Waziri anakuja kuvunja Idara ya shirika huyo MD yuko wapi? Inaelekea Waziri Makamba is micromanaging TANESCO kwa maslahi yake mwenyewe sio ya nchi!!! Sasa alitaka hicho kitengo kiseme uongo kuhusu utendaji mbovu wa shirika?
 
Back
Top Bottom