Waziri wa Nishati, January Makamba ametembelea mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere Agosti 08 2022 ili kukagua na kuangalia hatua mbalimbali zilizofikiwa na mradi huo.
"kwa sasa tumefika asilimia 67, Katika Miaka Miwili na nusu ya Mwanzo (Kuanzia Disemba 2018 - June 2021) tulifikia asilimia 37. Leo tuko asilimia 67 ni kasi kubwa katika kipindi hiki kifupi, Sasa hivi hapa kazi inafanyika saa 24 hakuna mapumziko kwa hiyo kasi imeongezeka" Makamba"
Katika kipindi hiki cha serikali awamu ya sita, tumeshuhudia kasi zaidi katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati. Na hili limekuwa ni kielelezo cha mhe rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha miradi yote mikubwa ya kimkakati inakamilika kwa uharaka.
Hakika Mama anaupiga Mwingi Sana.