Waziri Makamba: Msitegemee wala kutarajia bwawa la mto Rufiji kujazwa maji mwezi Machi

Hivi winchi ni kitu cha kusema haipo, tena waziri mzima, kabla hata ya mradi kuanza, inajulikana kila aina ya nyenzo zinazohitajika kwa kazi fulani, na hiyo ndio kazi ya mkandarasi, alafu huyo mkandarasi ana uwezo mkubwa tu. Alafu waziri anasema easily hakuna winchi, hii ni njia ya makusudi kuchelewesha mradi au kuuhujumu, imagine JPM angekuwa hai ndio Rais, hivi Makamba au waziri yeyote angethubutu kusema haya? Kwanza hii ni dharau kwa SSH.

Mama Samia Rais wangu, angalia sana huyu January, juzi kati tena tumesikia Tanesco wameingia mkataba wa USD 30 mil.. Takriban 69 bil tshs. Jamani, Mh. Rais mchunge huyu mtu, hatujakaa sawa mara gharama za kuchimba gesi tril 70.. Eeeeh eeeh, Mama yangu jamani, ebu mwangalie kwa umakini sana huyu January. Tril 70 ni gharama zote hizo kweli kwa ajili ya gesi kweli? Matrilioni hayoo jamaniiiii, OMG. Sasa kama ni tril 70, hiyo gesi hao wawekezaji si watatumia miaka 100 hadi warudishe gharama zao.. Mwanzoni tuliambiwa gharama ni tril 40 tu, ghafla imekuwa tril 70 za Tshs.
 
Tulimtukana MagufuliJP sana. Tuliposema nchi hii inahitaji kauzu hamkuelewa. Ngoja mkione cha moto kwanza. Na bado mtaambiwa kejeli zote hapa duniani hadi mkione cha mtemakuni. Ila mjue hadi 2025 nchi itakuwa paralyzed

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Nilisema chini ya hawa ndugu zangu CCM hututafika hata kanani,, yaani wanajiangalia wenyewe na mitumbo yao,,
Katiba mpya inatakiwa sasa hivi jamani!!!
 
Hoja ya kutokuwepo kwa "forklift" hapa nchini yenye uwezo wa kubeba kitu kizito chenye uzito wa tani 26, yaani 26,000Kg ni jambo la kushangaza sana. Forklift za Fantuzzi ambazo zinabeba makasha katika bandari zetu mbona zina uwezo huo!
 
Inaonesha kuna kundi kubwa la watu influential linaupinga mradi wa umeme wa Rufiji, tushukuru JPM aliukimbiza huu mradi kiasi kwamba umefika mbali kwamba kuureverse haiwezekani hivyo kinachofanyika ni kuuhujumu ili uchelewe au usiwe na manufaa kwa nchi.

Lengo la JPM ilikuwa mradi ukikamilika bei ya umeme ishushwe; lakini kutokana na namna ya gharama za uendeshaji wa TANESCO kuzidi kupelekwa juu kutokana na mikataba ya kifisadi iliyoanza kuingiwa kama ule tuliotangaziwa basi mradi wa Rufiji utakapokamilika bei haitashuka kwa sababu nafuu itakayopatikana itagharamia ufisadi.
 
Makamba yupo na Rais Samia Misri. Hayo maneno kaongelea Bunge la wapi?

Hizo chuki zenu dhidi ya Makamba zinaonesha kwa jinsi gani mlivyo vichaa
 
Msameheni mm nimeanza kutumia jamiiforumTz toka 2013.....lakin angalia id yangu ya sasa ni ya lini? Hajui kwamba unaweza kuwa na apps ya jamiiforum ukawa unasoma thread bila kuwa na id? Faida ya kuwa na id ni kuanzisha thread, kukoments, kuwa na pm, na mengine kama likes
 
Hoja ya kutokuwepo kwa "forklift" hapa nchini yenye uwezo wa kubeba kitu kizito chenye uzito wa tani 26, yaani 26,000Kg ni jambo la kushangaza sana. Forklift za Fantuzzi ambazo zinabeba makasha katika bandari zetu mbona zina uwezo huo!
Uko sahihi waende bandarini wakachukua hizo cranes

Zina uwezo mkubwa wa kunyanyua mizigo zaidi ya hizo Tani 26
 
Hii nchi ina viongozi wa hovyo hovyo kweli[emoji2297][emoji2297]
CCM ni janga kwa Taifa hili.
 

Kwahiyo Mkuu,
Kwanza Nimekupa Like,
Pili Kwa hiyo hilo winch lina Uwezo wa Kunywnyua Tani 26?Au halina Uwezo?
Ukiachana na Maneno mara nyingi Capacity za Machini Zinaandikwa kwenye Plate number kwa Mbele au Ubavuni mwa Equipment au Kwenye Engine!Kuna Kibati Either Colour au aluminium Ndio kinaandikwa Capacity of the Machine Kaka:
Load/lift Max tons:
Inawezekana ikawa Kweli Hatuna Winchi la Uwezo huo Kaka[emoji41]
 
Sasa kama Winch hakuna mnataka ziende nyumbu zikabebe, hawo wa SGR umesikia wao winch zao hazina kazi nao wanafanya kazi around the clock, badala ya kulalama mngeweka namba za mwenye hilo winch hapa waziri akisoma huu uzi hapa amtafute.
 
Utetezi mwingine kama huu hauna hata maana, Magufuli alikuta mradi wa umeme wa gas na uzalishaji umeshaanza. Ni kwanini apeleke 7t kwenye mradi mpya wa maji kuleta 2,115mg, kwani angeingiza 3t kwenye mradi wa gas tusingepata hizo 2,115mg? Au yeye Magufuli alikuwa anaharibu image ya JK? Tumekuwa nchi ya wajinga, kila rais akiingia anakuja na miradi ya kusaka sifa zake,matokeo yake tunabaki na mamiradi yaliyo chini ya kiwango, na madeni ya kutisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…