Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Kamarada karibu JF......Aisee kwa Waziri huyo tumepigwa!
Leo bungeni amedai Tanzania nzima eti hakuna winchi lenye uwezo wa kubeba milango yenye uzito wa tani 26 ili kuziba milango iliyokuwa inachepusha maji ili ujenzi wa bwawa uendelee.
Kadai winchi hilo hadi litoke nje ya Nchi 😂.
Hivi huyo jamaa anatuona hamnazo eti?!
Mawinchi mamia yaliyojaa Tanzania hii ambayo hata Waturuki wa SGR wanayo kibao ajabu leo tunadanganywa eti Nchi nzima hayapo?!
Naona mada zako zimeshushupalia sana pale bwawa la mwalimu Nyerere ambapo tutalipa jumla ya Trilioni 6.5 na malengo ya mradi kukamilishwa na arab contractors mwezi Juni 2022 tukipata MEGAWATI 2115.
Vipi una wasiwasi mradi huo kutoendelezwa?!!
Kwa sababu zipi?