Waziri Makamba: Ninatukanwa sana lakini nitalipa kisasi kwa matokeo

Waziri Makamba: Ninatukanwa sana lakini nitalipa kisasi kwa matokeo

Kwenye maisha ya kawaida kila mtu anatamani kubebwa,kila mtu anatamani kufika sehemu fulani ya mafanikio!!

Swali langu Kwako,Je ungepata fursa ya kupata mtu wa kukubeba ungekataa?

Hata mimi,natamani nipate mtu aweze kunibeba lakini sina?,tuache wivu jamani kila mtu na bahati yake!!
Njoo mimi nitakubeba ila kwenye toroli sasa.
 
Mkiambiwa kweli mnasema. Mipasho. Tanesco inaelekea kukaa sawa sasa hivi kuliko wakati wowote.

Nimeshangaa nilipowapigia simu ya dharura Tanesco.

Kwanza nimejibiwa vizuri, nikatumiwa namba ya complaint kwa message, haikupita lisaa limoja nikapigiwa simu na mtu wa Tanesco kuhakiki anuani ya kwenye tatizo, haikupita muda nikapigiwa na mafundi wananambia tutafika kwenye tukio baada ya nusu saa.

Kweli, ndani ya nusu saa naona umeme umerudi, wakanipigia tena mafundi kuniuliza kama tatizo linaendelea, nikawaambia hakuna tatizo umeme umerudi, wakanambia vizuri, tumetatua tatizo dogo kwenye transformer yenu.

Hayajawahi kuonekana hayo Tanzania hii, ni kwa mara ya kwanza nayashuhudia. Tena nupo kijijini siyo mjini.

Makamba anaitendea haki wizara hiyo. Mwenye chuki ajinyonge.
Udini tu unakusumbua hakuna lolote, tunalala giza kila siku tena Arusha, labda hakati kwa waislamu wenzake, Arusha hatutaki hata kumuona, kufungua umeme sahivi imekuwa ni hisani na siyo huduma hata kama nguzo ipo kwako na umelipa 320,000
 
Watakuja kujisifu tumeweza baada ya bwawa la Nyerere kumalizika mwakani na tatizo la umeme kuisha.

Wakati alieanza ujenzi wa huo mradi, alikuwa anatoa umeme wa uhakika bila ya hata hiyo JNHPP.

Huyu mtu ana siasa very cheap na kupenda kusafiria nyota za wengine; watakuja kujisifia mafanikio mwakani baada ya mwezi wa sita na kutuambia mnaona kazi tuliyofanya. Wakati wao wenyewe hawana impact ya walichofanya toka wapewe wizara zaidi ya kuitisha mikutano na kutupiga porojo tu na slide zao uchwara.
 
Huyu ni Waziri jangili kabisa kuwahi kutokea

Huyu ni Waziri jangili kabisa kuwahi kutokea
Ha! Eti jangili. Kwa tuhuma. Tuhuma za mitandaoni. Kutokana na nini labda.

Kwani huyo January mwenyewe anasemaje? 🤣🤣

Ongeeni sana ila kisasi ni MATOKEO. Ingawa mnajifanya hamyaoni matokeo. 🤔

Karma is real.
 
Udini tu unakusumbua hakuna lolote, tunalala giza kila siku tena Arusha, labda hakati kwa waislamu wenzake, Arusha hatutaki hata kumuona, kufungua umeme sahivi imekuwa ni hisani na siyo huduma hata kama nguzo ipo kwako na umelipa 320,000
Isikilize hotuba ya Makamba, tatizo la kukatika umeme baadhi ya maeneo litaendelea kutatuliwa kidogo kidogo mpaka liishe, kasema wazi, hawezi kuahidi kuwa litaisha nchi nzima kwa mwaka huu.

Huo ndiyo ukweli.
 
Mbona kipindi cha Kalema umeme ulikuwa haukatiki hovyo? kwanini bei ya umeme imepanda(27,000 -320,000) na unakatika hovyo? mbona Zanzibar bei ya umeme ipo chini na wakati Unguja ni mjini kama ilivyo Morogoro?
 
Simfahamu huyo "kalema". Sisi kijijini kwetu tumepata umeme wa tanesco mwaka huu.

Ahsante mama, ahsante January.
 
Back
Top Bottom