Waziri Makamba: Ninatukanwa sana lakini nitalipa kisasi kwa matokeo

Waziri Makamba: Ninatukanwa sana lakini nitalipa kisasi kwa matokeo

Waziri wa hovyo kuwahi kutokea.
"Siku moja hapa umeme umekatika Bungeni, kumetokea hitilafu. Ghafla bwana “fukuza Waziri, fukuza TANESCO”. Kumbe kuja kuchunguza waala!.

Umeme umekatika kwenye uwanja wa mpira, “fukuza Waziri, fukuza TANESCO”. Kumbe ni mambo mengine. Jamani, sio wakati wote ni TANESCO, sio wakati wote ni Wizara.

Sisi tutachukua wajibu wetu pale inapotokea” Waziri wa Nishati, January Makamba.

Haya maneno yanatuongezea hamu na hamasa ya kupata matokeo. Sisi hamasa yetu ni imani ya Mheshimiwa Rais kwetu, hamasa yetu ni matokeo ya kazi yetu kwa uhai wa chama chetu.

Hamasa nyingine ni kuwasaidia Watanzania kwa majukumu tuliyopewa. Lakini hamasa ya mwisho ni maneno haya, mtu akikusema wewe hufai maana yake unajitahidi ili uonekane unafaa. Kwa hiyo haya maneno yanatusaidia. Lakini pia haya maneno yanatusaidia kwa sababu yanawaamsha wanaotupenda na wanaotutakia heri ili watuombee dua na sala.”- Waziri January Makamba

“Maneno haya yanatusaidia kwa sababu yanatufundisha ukomavu, yanatufundisha kuwa na subra, yanatufundisha kuwa na uvumilivu na yanatujenga kuwa viongozi bora zaidi. Sisi tumesema waendelee kwa sababu yanatusaidi. Sisi kisasi chetu ni MATOKEO. Hatutabishana, hatutatupa maneno, hatutajitetea, tutalipa kisasi kwa matokeo” Waziri wa Nishati, January Makamba.
 
Ijumaa Qareem Makatani
FB_IMG_1660396245327.jpg
 
Makamba kubali tuu kwamba you don't fit kwenye hiyo position uliyopo, mipasho ya nini?
Kama hafai mje na facts

inakuaje Generator ya Uwanja wa Taifa ikizimika katikati ya mechi ahusishwe Waziri wa Nishati

kama Umeme umekatika ndani ya Ubunge kwa hitilafu za Jengo ahusishwe Waziri wa Nishati?

Tabia yenu ya kumshambulia kwa hoja nyepesi nyepesi mara mtu akifa ofisi ya CAG basi akitajwa yeye kahusika basi nasi tuamini kichwa kichwa …hapana

Makamba sio chaguo langu lakini pia sikubali mtu kuchafuliwa

nilikuwa simkubali Lowassa lakini pia nilikuwa sikubali Siasa chafu dhidi yake
 
Mkiambiwa kweli mnasema. Mipasho. Tanesco inaelekea kukaa sawa sasa hivi kuliko wakati wowote.

Nimeshangaa nilipowapigia simu ya dharura Tanesco.

Kwanza nimejibiwa vizuri, nikatumiwa namba ya complaint kwa message, haikupita lisaa limoja nikapigiwa simu na mtu wa Tanesco kuhakiki anuani ya kwenye tatizo, haikupita muda nikapigiwa na mafundi wananambia tutafika kwenye tukio baada ya nusu saa.

Kweli, ndani ya nusu saa naona umeme umerudi, wakanipigia tena mafundi kuniuliza kama tatizo linaendelea, nikawaambia hakuna tatizo umeme umerudi, wakanambia vizuri, tumetatua tatizo dogo kwenye transformer yenu.

Hayajawahi kuonekana hayo Tanzania hii, ni kwa mara ya kwanza nayashuhudia. Tena nupo kijijini siyo mjini.

Makamba anaitendea haki wizara hiyo. Mwenye chuki ajinyonge.
Umeandika ujinga kujifurahisha lakini sio kumuaminisha mtu yoyote hapa, usifikiri watu hawajui na hawaoni
 
So ulitaka hiyo project isifanikiwe? Can u imagine itaingiza sh ngapi kwenye uchumi na mzunguko wa fedha kwa ujumla? Tuache chuki tutoe alternatives. Hii tabia ya kila project kusema kuna wizi au kuita watu waliotuzidi uwezo kuwa ni wezi ni tabia ya sadists tuiache na tujifunze kufurahia mafanikio ya wenzetu

Kwa taarifa yako asilimia 10 ya Trillion 90 ni Trillion 9! Hiyo hela tu ikiingia kwenye mzunguko itabadili maisha ya watu kwa malaki mtaani. Tuache chuki
Hata kwenye gas ya Mtwara mlijitapa hivi hivi na mkaenda mbali sana mkasema Kukatika umeme Tanzania itakuwa historia.Mnatufanya mazezeta lakini historia hujiandika kwa matendo na maneno yenu.
 
Kwenda zako bwana. Hizi ni hoja za kizembe sana kutetea haiba ya mtu. Kwahiyo akiingia waziri akakataza viroba automatically anakuwa the best?

Hizi ni hoja hafifu. Huyu mtu ana tuhuma nyingi sana za ubadhirifu wa pesa za umma so ni ngumu at this point kuassume at ni chuki binafsi bali kuna something very fishy going on behind that fake good government official face of his.

Time will reveal all that is hidden.
Kuna jambo lipo Waziri mwizi,fisadi na mzembe anafumbiwa macho aendelee kuiumiza nchi.
 
Tatizo hii wizara mliianza kwa propaganda nyingi mno Bwana Makamba kutaka kuonesha waliotangulia walikuwa hawafai na bado mnaendelea na huu utoto.

Juzi Kaimu Meneja wa Huduma kwa wateja (TANESCO) anadai katikakatika ya umeme mitaani ni wiring za nyumba hazifanyiwi service.

Yaani mtaa,kata au wilaya nzima ikose umeme kisa hawajafanya service ya wiring za nyumba huku zingine nyumba mpya kabisa!

Hii wizara haitaji porojo,ukifanya fyongo hadi vipofu wanajua leo hakuna umeme.
 
jambazi kubwa, kisasi pekee atakacholipiza ni kuiba pesa zaidi.

we jitu gani kila linapokwenda linachukiwa, anadhani ni coincidence tu?? kajamaa kanajifanya kajanja sana lakini tamaa zake zinamfanya avurunde.
anayemchukia nani, labda we na mamako, lile ni jembe jana alikuwa anasifiwa na kila mbunge. Nami namkubali sana ana akili na maarifa makubwa sana, na ni mvumilivu ana ngozi ngumu hasikili wala kuzingatia porojo za wapuuzi km wewe. Na umeze sumu siku akiwa rais wa nchi hii. Kinachowasumbua wivu mlitegemea angechemka lakini amefanya na anaendelea kufanya makubwa.
 
anayemchukia nani, labda we na mamako, lile ni jembe jana alikuwa anasifiwa na kila mbunge. Nami namkubali sana ana akili na maarifa makubwa sana, na ni mvumilivu ana ngozi ngumu hasikili wala kuzingatia porojo za wapuuzi km wewe. Na umeze sumu siku akiwa rais wa nchi hii. Kinachowasumbua wivu mlitegemea angechemka lakini amefanya na anaendelea kufanya makubwa.
Mama yangu kaingiaje hapa? Hii ndio athari ya nyie mitoto ya kuzaliwa kwenye madanguro mnahisi kila mtu ni baba yenu.
 
Ni kuwapuuza tuu uzuri Historia itaandikwa mikononi mwake..

Atasema nilisimamia bwawa la Nyerere
Nilisimamia mapinduzi ya Nishati Tanzania
Nilisimamia ndoto ya Tanzania kuwa na mradi mkubwa kabisa wa LNG Africa

Hii tuu ni credit kubwa kabisa kwake na historia itamuandika hivyo..

Cha Kuombea ni Rais Samia asikubadilishe Wizara hata baada ya 2025 Ili uandike historia vizuri na kuondoa ule ukakasi wa Mawaziri wa Nishati kutodumu..
Gesi ya Mtwara mmefikia wapi?Kumbukeni Ahadi ni deni?
 
anayemchukia nani, labda we na mamako, lile ni jembe jana alikuwa anasifiwa na kila mbunge. Nami namkubali sana ana akili na maarifa makubwa sana, na ni mvumilivu ana ngozi ngumu hasikili wala kuzingatia porojo za wapuuzi km wewe. Na umeze sumu siku akiwa rais wa nchi hii. Kinachowasumbua wivu mlitegemea angechemka lakini amefanya na anaendelea kufanya makubwa.
Ungeyataja hayo aliyofanya makubwa
 
Back
Top Bottom