Waziri Makamba una majibu mepesi, Mawaziri wote hubanwa kwenye utendaji. Jibu maswali ya Kamati ya Nishati

Waziri anasema eti bei ya mafuta imepanda kwenye soko la Dunia kwakua kuna tension ya vita kule Russia na Russia ni mmoja ya nchi inayouza mafuta kwa wingi.

Toka lini sisi tunanunua mafuta toka Urusi??

Na je hiyo tension ya vita imeathiri vipi production ya oil duniani??

Angezungumzia vita Iraq, Saudi Arabia na nchi nyingine za kiarabu ambazo ni major producers wa oil ningemuelewa ila sio kutudanganya na Urusi.
 
Empty kabisa, Ina maana mawaziri wengine waulizwe maswali Ila yeye asiulizwe?
 
Kama upo kwenye payroll yake hongera, Ila Kama unajitolea pole sana.
 
Waziri Makamba umeonyesha kiwango kidogo cha ukomavu, kwa kusema wabunge wanakubana kwa sababu ya uwaziri wako
Aachane na uwaziri kama uwaziri huo unambana kiasi cha kukosa amani ya kufanya kazi. Mbona wengine walipoona uwaziri mkuu ndiyo shida waliamua kuuacha?

Lakini kama anaona kubanwa huko siyo sababu afanye kazi hapa na ahakikishe kazi inaendelea! Siku 10 za marekebebisho/matengenezo ya mifumo ya umeme nchini zilishakwisha. Umeme bado unasumbua.
 
Nilikuwa najua ni smart huyu jamaa kumbe ni mswahili tu
Huo usmart autoe wapi?
Kila waziri huulizwa kuhusu wizqra yake kwenye maswali na majibu, yeye akiulizwa anakimbilia kusema wanamuonea wivu
 
Sukuma Gang hamjafurahishwa kabisa na uteuzi wa Makamba! Na ndiyo maana sishangai kuona kiongozi wa hayo mashambulizi ni mzee wa majungu! Joseph Kasheku Msukuma!

Mlitamani Kalemani awe Waziri wa maisha sijui! Makamba Jr ana haki ya kujitetea.
 
Makamba ni mmoja wa mawazir wenye uwezo mdogo sana. Sijuagi ni nn kinafanya mfumo umuone anafaa
 
Kama anaona uwaziri ni tatizo kwanini asiachie ngazi? uwezo mdogo sn ameonyesha anabebwa na udini pekee
 
Sukuma Gang hamjafurahishwa kabisa na uteuzi wa Makamba! Na ndiyo maana sishangai kuona kiongozi wa hayo mashambulizi ni mzee wa majungu! Joseph Kasheku Msukuma!

Mlitamani Kalemani awe Waziri wa maisha sijui! Makamba Jr ana haki ya kujitetea.
Mkuu mm sio sukuma, Ila hayo maswali yamekua yakiulizwa kwa wizara zote. Mbona aweso akibanwa kuhusu maji hasingizii tatizo ni uwaziri wake?
Ina maana hawapaswi kabisa kuhoji kuhusu wizara ya nishati?
Nape akibanwa kuhusu mabando, mbona hakukimbilia kusema wanamuonea wivu?
Hata huyo kalemani walimbana sana huko bungeni na mwisho akanonekana waziri asiye na mvuto kabisa
 
Yaani walimtoa Kareman wizara ya nishati ili kuhalalisha wizzi wao mkubwa ndani ya hiyo wizara, kule kwingine nako wakamtoa lukuvi na kumsimika jizi lililo kubuhu. Shame on you SSH na majizi menzakao!

CCM wote ni wezi tu! Hata huyo Kalemani na Lukuvi siyo Malaika. Kamwe huwezi kuwa ndani ya ccm halafu ukawa msafi.
 
CCM wote ni wezi tu! Hata huyo Kalemani na Lukuvi siyo Malaika. Kamwe huwezi kuwa ndani ya ccm halafu ukawa msafi.
ila degree / kiwango cha ujizi kinatofautiana ingawa wote ni ujizi tuu, atakacho kwiba rizi-1 si sawa hata kidogo alicho kwiba lukuvi, anacho kwiba makamba si sawa na alicho kwiba kaleman kwa ujumla wote, kuna kijizi kingine kinakuibia angalau kina kuachia hata udaga na maharage ya kuanzia maisha asubuhi, kuna lijizi linguine lina komba kila kitu kwa 'kokoro' yaani halikuachii hata chumvi...
 
Ni aibu kwa taifa hili lenye kila chanzo cha nishtati umeme kuwa anasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…