Waziri Makamba una majibu mepesi, Mawaziri wote hubanwa kwenye utendaji. Jibu maswali ya Kamati ya Nishati

Waziri Makamba una majibu mepesi, Mawaziri wote hubanwa kwenye utendaji. Jibu maswali ya Kamati ya Nishati

Makamba ajitahidi kwani yeye ndiye mmiliki wa Tanesco! Na hayo matatizo ya Tanesco yalianza leo? Siyo Serikali hii ya CCM iliyo tudanganya kipindi kile kulimaliza kabisa hilo tatizo la umeme, baada tu ya kugundua gesi?

Gesi iko wapi? Si mliwauzia nyinyi Mabeberu kwa siri! Sasa iweje leo mtu aliyekaa ofisini kwa miezi 4 tu aonekane ndiyo chanzo cha matatizo yaliyo tokea zaidi ya miaka 20 iliyopita? Ndiyo maana nimesema huyo Makamba Jr, yuko sahihi kujitetea. Huenda ni vita tu ya kugombania ulaji kwenye hiyo Wizara.

Na uzuri ccm wote mnajuana! Ni wapigaji tu.
[emoji23][emoji23][emoji23]Kweli kumbe humu jf kuna vichaa!

Basi tumwambie makamba hata bungeni pale asikifike kabisa kujibu maswali ajikalie tu nyumbani maana hilo halimhusu kabisa.

Kumbe tz ni masikini sababu ya upumbavu wetu bhana!

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Tanesco ipo chini ya wizara ya nishati, waziri wa nishati ni makamba. Unataka watu maswali wakaulize wapi?

Kwa Makamba! Ila maswali yakijikita kwenye eneo husika, yanaleta tija! Na ikitokea Mbinge akaamua kumu attack mtu kama mtu, badala ya Wizara husika, nadhani huyo mtu ana haki ya kujitetea.
 
Mbona hata Juma Aweso wakati anapewa Wizara ya Maji, mbona kila mtu aliamini tatizo ka maji nchini litabakia kuwa historia!

Lakini leo hii, na yeye ni mmoja kati ya Mawaziri wanopigwa vita! Na baadhi ya nyuzi za kumlaumu, zipo humu jukwaani. Kwangu mimi tamaa yangu ni kuona CCM inatoka madarakani, ili ikajipange upya. Ila kwa sasa haina jipya kwa maendeleo ya Nchi yetu.
Tatizo kubaki sio sababu ya kumuacha waziri ikiwa unaona mambo hayaendi.
Kuhusu CCM ni sawa kabisa na na kuunga mkono haipaswi kuendelea
 
The guy is simply incompetent to lead such a sensitive Ministry.
 
Kiutendaji mwezi wa kwanza wa malope ni mwepesi sana. Yaani anakimbilia kulialia eti sababu ni uwaziri, huo ni utoto. Sikutegemea mtu aliyekuwa anataka kuwa Kiongozi mkubwa wa kitaifa kupwaya namna hii. Unajua self-awareness ni kitu muhimu sana kwa Kiongozi anayekulia uongozi. Kama atakaa chini na kujua ni wapi anapaswa kurekebisha anaweza kuwa Kiongozi mzuri tu. Mwezi wa kwanza ebu jaribu kukaa chini uji- assess usiwe kama akina makonda. Magod-father wana limit zao pia, ipo siku watafikia kikomo.
 
Kwa Makamba! Ila maswali yakijikita kwenye eneo husika, yanaleta tija! Na ukiamua kumu attack mtu kama mtu, badala ya Wizara husika, huyo mtu ana haki ya kujitetea.
Kwa nini hili suala ni makamba tu? Swali langu mbona kwa aweso hatuoni haya unayosema?
Ni mbunge gani kamu attack makamba?
Makamba kaulizwa sababu za umeme kukatikatika, ni Kama anavyoulizwa aweso sababu za ukosefu wa maji. Hata waziri wa elimu amekumbana na maswali magumu ya kwa nini Watoto wanafeli sana.
Kwa nini ikiwa kwa makamba unaona Kama anashambuliwa na sio aweso au waziri wa afya au waziri wa elimu?
 
Anaulizwa swali kwanini visingizio vya umeme kukatika ni vingi na havina mashiko, anakimbilia kulia hati hawataki hawe waziri, na anamwingiza na Rais ati hawataki Samia hawe Rais.

Sijawahi kuona waziri mwenye uelewa mfupi kama Makamba Junior. Huyu anabebwa tu hakuna lolote wala chochote.
Akiulizwa umeme Tanzania yeye anaanzaa "oooh...duniani kote kuna hiki na hiki"
Anajifanya ana logic kumbe ni empty headed...zero brain"

Mawaziri wote uulizwa maswali, yeye ni nani asiye taka kuulizwa. Abadili kanuni na sheria za Bunge, ili asiulizwe.
Ati anajisifia, tuna bodi imara na uongozi mzuri wa Tanesco....! Rubish!
Weye bebwa tu na mama yetu, lkn akishindwa atakutua.
 
Mbona hata Juma Aweso wakati anapewa Wizara ya Maji, mbona kila mtu aliamini tatizo ka maji nchini litabakia kuwa historia!

Lakini leo hii, na yeye ni mmoja kati ya Mawaziri wanopigwa vita! Na baadhi ya nyuzi za kumlaumu, zipo humu jukwaani. Kwangu mimi tamaa yangu ni kuona CCM inatoka madarakani, ili ikajipange upya. Ila kwa sasa haina jipya kwa maendeleo ya Nchi yetu.
Unasema ni mmoja ya mawaziri wanaopigwa vita, Sasa Kama umeme umekua shida na yeye hilo amekiri kwa nini asipigwe vita?
Kikwete kapigwa sana vita humu, Magufuli humu nae kapigwa vita sana na ilikuwa sawa kabisa kumpiga vita na sasa mama Samia anapigwa Sana vita humu na ni sawa tu. Kwa nini makamba kupigwa vita iwe issue kwako?
 
Waziri Makamba umeonyesha kiwango kidogo cha ukomavu, kwa kusema wabunge wanakubana kwa sababu ya uwaziri wako.

Hii ni kauli inayopaswa kutolewa na mtu ambae sio msomi, hakuna wabunge wenye shida na uwaziri wako bali wanachofanya ni wajibu wao kwa maana wanawakilisha wananchi.

Wabunge wanarudi majimboni wanaulizwa kuhusu umeme kwa kuwa unaathiri shughuli zao, wao ndio wanakuja bungeni kueleza kero hiyo. Wewe hutaki uulizwe.

Pia waziri unapaswa kufahamu sio wewe tu ambae unabanwa kwenye utendaji hasa Jambo fulani likienda vibaya. Ni mawaziri wote hubanwa hivyo, waziri wa afya amekuwa akibanwa kuhusu vituo vya afya.

Waziri wa maji juma aweso amekuwa akibanwa sana bungeni kuhusu upatikanaji wa maji, waziri wa ujenzi amekua akibanwa kuhusu ubovu wa miundombinu Ila wote hao hawakuwahi kusema tatizo ni uwaziri wao.

Majibu yako mh.makamba ni ya kushangaza, sasa unasema waya kwenye substation ya ubungo zipo uchi hivyo upepo ukipuliza tu umeme unakatika.

Kwa majibu ya namna hiyo unategemea watu wataacha kukuuliza maswali?

Kamati ya nishati ya bunge ni haki yao kuhoji na wamesema hakuna sababu za msingi za umeme kukatwa.

Makamba maswali ya kuhusu wizara ya nishati unataka aulizwe nani? Mbona mawaziri wengine wanaulizwa maswali kuhusu wizara zao na wanajibu bila shida, kwa nini wewe uone unaonewa wivu? Hutaki watu/wabunge waulize kuhusu wizara ya nishati?

Wajibu maswali yao kiuweledi na sio kusingizia uwaziri wako.
Hii kauli aliyo wahi kuiongea imemuweka uchi na kuonyesha ukilaza wake "zamani umeme ulikuwa haukatiki sababu walikuwa hawafanyi schedule maintenance...." na wenzake wanambana kwa kauli yake mwenyewe,ajibu hoja aache kulialia.
 
Nchi za European hazi Uzi mafuta na Russian wanauza gas kwa kupitia mabomba kwa baadhi ya nchi za European
Hilo anapaswa afahamu Makamba na sio mimi.

Maana yeye ndio kasema bei ya Mafuta imepanda kisa tension ya vita huko Russia.
 
Unasema ni mmoja ya mawaziri wanaopigwa vita, Sasa Kama umeme umekua shida na yeye hilo amekiri kwa nini asipigwe vita?
Kikwete kapigwa sana vita humu, Magufuli humu nae kapigwa vita sana na ilikuwa sawa kabisa kumpiga vita na sasa mama Samia anapigwa Sana vita humu na ni sawa tu. Kwa nini makamba kupigwa vita iwe issue kwako?

Ni Homeboy✍️ ☹️
 
Haya ndio madhara ya vyeo vya kupewa kwa kupendelea na kujuana😕

Yani nimemsikiliza bungeni nikasikitika sana ni kama anajibu mahasidi wake na sio kujibu kwa kutatua changamoto mbaya ya umeme inayoendelea nchini😕
 
Sasa waziri akianza kulialia nani atajibu maswali ya wananzengo, kama vipi aturudishie huo uwaziri ili asiendelee kuulizwa maswala. Kuna ule msemo 'ukikubali kuolewa...........'
 
Jamaa anajifanya Mwerevu sana, lkn kwann anadhani Watanzania ni wajinga? Hata wasione elements ndogo ndogo za kushindwa kwake?

Alivyomjanja wakutojielewa, anamchomekeamo "SAMIA" ili ajikinge kwamba Mama samia aliyemchagua aliona anafaa. Kwamba uwepo wa Samia, utafanya aendele kuwepo.

Shame!
Swila na Kibatala
 
Malop ni bonge la mswahili. Nchi Iko na waswahili full mipasho na kulialia.
 
Sukuma Gang hamjafurahishwa kabisa na uteuzi wa Makamba! Na ndiyo maana sishangai kuona kiongozi wa hayo mashambulizi ni mzee wa majungu! Joseph Kasheku Msukuma!

Mlitamani Kalemani awe Waziri wa maisha sijui! Makamba Jr ana haki ya kujitetea.
2-2= .
 
Siku mkikubali uwaziri utokane na merit za mtu na sio favour basi tutafika mbali.

Kama Makamba angekuwepo hapo kwa merit basi angwajibika pasina shaka.

Ila kwakua ni uteuzi wa bila sababu yoyote ya msingi basi tutarajie pia business as usual.

Makamba atakua mtiifu kwa aliyemteua na sio kwa wananchi ndio maana anamtaja sana aliyemleta hapo.

Hapo hofu yake iko kwenye kupoteza cheo tu na sio kutumikia wananchi.
 
Back
Top Bottom