Waziri Makamba una majibu mepesi, Mawaziri wote hubanwa kwenye utendaji. Jibu maswali ya Kamati ya Nishati

Waziri Makamba una majibu mepesi, Mawaziri wote hubanwa kwenye utendaji. Jibu maswali ya Kamati ya Nishati

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Waziri Makamba umeonyesha kiwango kidogo cha ukomavu, kwa kusema wabunge wanakubana kwa sababu ya uwaziri wako.

Hii ni kauli inayopaswa kutolewa na mtu ambae sio msomi, hakuna wabunge wenye shida na uwaziri wako bali wanachofanya ni wajibu wao kwa maana wanawakilisha wananchi.

Wabunge wanarudi majimboni wanaulizwa kuhusu umeme kwa kuwa unaathiri shughuli zao, wao ndio wanakuja bungeni kueleza kero hiyo. Wewe hutaki uulizwe.

Pia waziri unapaswa kufahamu sio wewe tu ambae unabanwa kwenye utendaji hasa Jambo fulani likienda vibaya. Ni mawaziri wote hubanwa hivyo, waziri wa afya amekuwa akibanwa kuhusu vituo vya afya.

Waziri wa maji juma aweso amekuwa akibanwa sana bungeni kuhusu upatikanaji wa maji, waziri wa ujenzi amekua akibanwa kuhusu ubovu wa miundombinu Ila wote hao hawakuwahi kusema tatizo ni uwaziri wao.

Majibu yako mh.makamba ni ya kushangaza, sasa unasema waya kwenye substation ya ubungo zipo uchi hivyo upepo ukipuliza tu umeme unakatika.

Kwa majibu ya namna hiyo unategemea watu wataacha kukuuliza maswali?

Kamati ya nishati ya bunge ni haki yao kuhoji na wamesema hakuna sababu za msingi za umeme kukatwa.

Makamba maswali ya kuhusu wizara ya nishati unataka aulizwe nani? Mbona mawaziri wengine wanaulizwa maswali kuhusu wizara zao na wanajibu bila shida, kwa nini wewe uone unaonewa wivu? Hutaki watu/wabunge waulize kuhusu wizara ya nishati?

Wajibu maswali yao kiuweledi na sio kusingizia uwaziri wako.
 
waya kwenye substation ya ubungo zipo uchi hivyo upepo ukipuliza tu umeme unakatika.
... nyeti za kuku zi wazi! Umeme kukatika pindi manyunyu yanapoanza imekuwa jambo la kawaida nchi hii; sio jana tu; ni tatizo la miaka na miaka. How long does it take kuzivalisha hizo nyaya nguo ili kuondokana na tatizo? CCM ni wapuuzi sana; imefika mahali wamehalalisha upuuzi wao uonekane kawaida maisha yanaendelea.
 
Ndugu zangu,

Ni tahadhari tu ninampa mdogo wangu January ya kwamba maneno yako mwenyewe ndio kitanzi chako. Wizara ya Nishati sio ya propaganda ni ya vitendo.

Muda utajibu kama utaendelea na mtindo huu wa propaganda kwani wananchi wanataka Nishati ya umeme tu sio visingizio lukuki huku ukilialia.
 
Anaomba apewe muda. What an incompetent fellow! 😂

Wenzie walifanya kazi right away, hawakuomba muda.

Wenzie hawakujificha kwenye Uwaziri wala Urais.

Huyu anabebwa tu na jina la mzee wake, lakini kiuhalisia na kiutendaji hakuna kitu pale.

He is overrated.
 
Jamaa anajifanya Mwerevu sana, lkn kwann anadhani Watanzania ni wajinga? Hata wasione elements ndogo ndogo za kushindwa kwake?

Alivyomjanja wakutojielewa, anamchomekeamo "SAMIA" ili ajikinge kwamba Mama samia aliyemchagua aliona anafaa. Kwamba uwepo wa Samia, utafanya aendele kuwepo.

Shame!
 
... nyeti za kuku zi wazi! Umeme kukatika pindi manyunyu yanapoanza imekuwa jambo la kawaida nchi hii; sio jana tu; ni tatizo la miaka na miaka. How long does it take kuzivalisha hizo nyaya nguo ili kuondokana na tatizo? CCM ni wapuuzi sana; imefika mahali wamehalalisha upuuzi wao uonekane kawaida maisha yanaendelea.
Wanahalalisha upuuzi wao kwa majibu mepesi kama ni serikali ya chama kingine ndio ilifanya madudu yote. CCM wanachukulia awamu za uraisi kama ni awamu za chama pia. Ni kama vile kila raisi anakuja na chama chake.
 
Mpuuzi sana. Nimesikiliza majibu yake nikamdhalau sana. Analaumu kushambuliwa na mh Msukuma kuwa amepanda helicopter. Kwani kweli unaweza kukagua miundombinu ya umeme kwa kutumia helicopter? Kama siyo matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa!!
[emoji871]Mkuu wababayangu!

[emoji871]Kuhusu makamba kukagua vina vya mito na mabwawa ya maji kwa kutumia HELIKOPTA!

[emoji871]Mimi binafsi niliwahi kujiuliza sana bila majibu.

[emoji871]Utawezaje kujua kina cha maji ukiwa Angani.
 
Sipend blame game hasa kwa vitu ambavo siwez kuinfluence,

Ila sioni maajabu yoyote anayofanya Makbamba na Maharage, frequent outbreak zimekuwa nyingi, na hope/prospect ya kuondoka au kupungua hazionekani. Waswahili wanasema hana jipya kwenye uongozi wake
 
Mama ad 2030 na makamba ad 2028 kaeni kwa kutulia na chuki zenu binafsi

Yan mnataka watu wote wafanye kaz kwa mazoea km msukule wenu
Hii nchi itakua ngumu sana km mkitaka kla Raisi awe Magufuri jiwe
Raisi ww ni Jaji, ni polisi ww ni mwanasheria, Mungu mtu , ww ni tume ya uchaguzi, muhasibu , injinia
Acheni watu wafanye kaz siasa ni 2030 baada ya Mama kutoka
 
Back
Top Bottom