Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
WAZIRI MAKONDA UMEKATAA KUTUPA HELA WAANDISHI WA MTANDAONI KWANI SISI SIO CONTENT CREATORS?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Juzi tulionana pale kwenye Final ya Pongwe Cup, Upanga, ukiwa kama Mgeni Rasmi. Sikupata nafasi ya kukujulisha hili kutokana na hali iliyokuwepo.
Hii ni mara ya pili naandika hapa. Na kwenye mitandao ya kijamii kuhusu waandishi wa mitandaoni wenye tija katika jamii na taifa letu.
Nimekutaja Makonda kama mwakilishi lakini ujumbe huu ni waserikali nzima.
Nilisema na narudia kusema, kwa heshima ya kalamu na uandishi wa mitandaoni. Mimi kama Mtibeli, nawaombea hawa vijana na mabinti wanaojishughulisha na kuandika mitandaoni mambo yenye tija kwa taifa letu. Nao waonwe. Wakatiwe fungu lao. Wanufaike hata kwa kidogo tuu. Watashukuru sana
Mhe. Makonda, na serikali kwa ujumla. Unapoingia Google kutafuta elimu fulani iwe ya mambo yako ya faragha au mambo ya kiserikali, mambo utakayoletewa chanzo chake ni waandishi wa mitandaoni.
Ukimuuliza ChatGPT, ukiuliza Google ukiuliza Facebook popote utakachouliza kinachohusu maarifa na msaada kwa changamoto uliyonayo. Majibu utakayoletewa yanatokana na waandishi walioamua kutoa elimu na maarifa hayo na kuyaweka hadharani.
Sharing is Caring walisema wahenga
Kuandika inahitaji Akili njema. Ufahamu ulioshiba. Na kujitolea.
Hatuwezi kuwa na taifa la kuthamini wacheza uchi, wavaa vichupi na biki na kujirekodi na kuwaita hao ndio Content CREATORS tena serikali inawatolea macho na kuwatambua. Hapana.
Standing ili kujichimbia mrija kwenye Bomba kuu ili nami nipate ulaji. Hapana. Naandika kama mtunzi, mwandishi na ninajua kazi wanayoifanya watunzi na waandishi wa mitandaoni.
Na najua hata serikali inajua fika waandishi wa mitandaoni wanawasaidia na kuisaidia pia serikali. Viongozi wengi hujifunza kupitia maandishi ya wanaoandika mitandaoni.
Familia zenu zinanufaika pia.
Sasa kwa nini hamtaki kurudisha shukrani hata kidogo.
Wapeni hela vijana.
Vijana wanafanya kazi wapeni hela.
Kama hela inakuwa kazi. Watambueni hata kwenye matukio yenu, matamasha. Ili kuwajenga na kuwapandisha.
Ninavijana kadhaa ambao nilikuwa nawasiliana kwa miaka kadhaa wanalalamika.
Kwangu mimi nafanya hii kama hobby lakini vipi kwa wengine.
Wanakata tamaa.
Hakuna mtu yeyote nchi hii na dunia hii kwa zama hizi ambazo hata tumia waandishi wa mtandao kupata maarifa.
Kama ni mfugaji wa kuku, lazima aingie mtandaoni aulize jinsi ya kufuga kuku asome.
Kuhusu magari pia,
Kuhusu mahusiano pia.
Kuhusu jambo lolote lile.
ChatGPT na Chat robots zingine hazina uwezo wa kujitungia maarifa. Zinachukua mitandaoni, kwenye blogs na websites ambazo ziliandikwa na waandishi na watunzi.
Tunataka Hela sisi bhana!
Kila siku mnatenga mafungu ya mapesa huko. Huku hatuzioni.
Wapeni vijana Pesa.
Andaeni utaratibu namna ya kuratibu hili jambo.
Mambo ya siasa yasiingie humo. Sio mje mtoe hizo hela kwa machawa wa serikali au machawa wa upinzani.
Hela ziende kwa wanaostahili. Wanaoisaidia jamii.
Ni laana kubwa kutotambua na kuheshimu watu wanaosaidia jamii na taifa. Laana kubwa sana.
Mimi nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Masaki, Dar es salaam