Waziri Masauni aagiza uchunguzi maiti zilizookotwa kwenye viroba

Waziri Masauni aagiza uchunguzi maiti zilizookotwa kwenye viroba

Mkuu wa mkoa wa Tanga Mgumba amesema maiti zilizokutwa zimetupwa wilayani Kilindi yawezekana zimetoka nchi Jirani na siyo Tanga

Mgumba amesema maiti hizo zilifungwa kwa ustadi mkubwa kwenye viroba vya kilo 50 hali inayoonyesha wauwaji ni wazoefu wa matukio
hayo

Watu wote wa Kilindi wameshindwa kuzitambua maiti hizo

Naye waziri wa mambo ya Ndani mh Masauni amesema wahalifu hai wanatafutwa na jeshi la Polisi kwa nguvu zote

Source ITV habari
"Maiti zilizookotwa wilaya ya Kilindi-Tanga zinawezekana zimetoka nchi jirani..." Mkuu wa Mkoa wa Mgumba Tanga. Nchi jirani wanawezaje kuingia Tanzania kirahisi hivi bila kubainika? Kwa hiyo usalama wa nchi uko hatarini kiasi ambacho mgeni yeyote anaweza kuinga Tanzania na kufanya chochote bila kujulikana kisha akaondoka sijui kwa kupitia wapi? JW, je mipaka ya Jamhuri ya Tanzania iko salama au kuna ugaidi kwenye ukanda wa kasikazini mwa nchi? Waziri wa mabo ya ndani wa Tanzania uko wapi kulitolea ufafanuzi hili kwa ushahidi usio na shaka kuliko kutuhumu nchi jirani kuingia bila kibali kisha kuondoka bila kujulikana? Rais wa Tanzania na serikali yake mko peupe na hatarini kama hali ndio hiyo iliyoelezewa na mkuu wa mkoa wa Tanga......Aibu sana hii kama ilivyonukuliwa kutoka ITV Habari.
 
Ishu ya vifo mtu anaongea bila kufanya uchunguzi wa kina ndio atoe majibu kwa kuwa sio ndugu zake ila kwa kila baya tunalotenda lina karma yake wacha waendelee na maigizo tu..
 
"YAWEZEKANA" the dude is called RC aka the head of the Region.
Hata sisi tunasema inawezekana zimetoka pale Bermuda, sasa jukumu lake kama RC mkuu wa ulinzi na usalama kwa kutumia resources zake ahakikishe anaclear neno "YAWEZEKANA" na kuleta jibu sahihi.

Wapo hapo Forensic experts, take the bodies do what needed to be done, display the faces of all the dudez publically for recognition but should be in various looks.

The team may also advice the importnat of DNA registration to the system for all wananchi, this could be very easy to testify by sampling among wananchi.

They will say, "WE NEED KATIBA MPYA" without smart people onland and civilized society.

these people need mikwaju to activate their brains and set them to be proactive.
 
Haya ndio madhara ya kugawa ofisi kwa watu wenye elimu bila exposure, yeye toka amezaliwa anasomasoma tu darasani matokeo amekuwa na Robot.

Kabla ya kuwapa hawa watu vyeo waachwe kwanza mtaani huku sekta binafsi waogelee wakae kwenye nafasi za maamuzi na kuwa sehemu za maamuzi au watoa maamuzi yaliyoleta positive impact sehemu.

Unampa tu URC huku hajawahi hata kufanya maamuzi mahala yakaleta faida na watu wakanufaika.
 
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mgumba amesema maiti zilizokutwa zimetupwa wilayani Kilindi yawezekana zimetoka nchi Jirani na siyo Tanga

Mgumba amesema maiti hizo zilifungwa kwa ustadi mkubwa kwenye viroba vya kilo 50 hali inayoonyesha wauwaji ni wazoefu wa matukio
hayo

Watu wote wa Kilindi wameshindwa kuzitambua maiti hizo

Naye waziri wa mambo ya Ndani mh Masauni amesema wahalifu hai wanatafutwa na jeshi la Polisi kwa nguvu zote

Source ITV habari
Kwani huko Kuna mto unaotiririka toka Kenya kwenye hili kiangazi unaopitia kilindi mkuu wa mkoa? Tujibu hili swali

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Vipi na hivi Viroba tumlaumu Dr John Magufuli ?

dhambi ya kumnanga yule Mzee haitowaacha salama wanafiki

sasa hivi wakosoaji wa Serikali hawasikiki kabisa japo uhuru umerudi

Magazeti yote, wanaharakati wote,wanasiasa wote wapo kwny foleni ya kuelekea kwny kibuyu…unahisi ukipiga kelele utachomolewa kwny folen
Hawakosoi kwa sababu wameshalipwa stahiki zao.
We hushangai Mwenyekiti wa Saccos amekamatwa na huu utawala lkn anasingiziwa JPM.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamadi Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika na mauaji ya watu wawili na kuwatupa wakiwa kwenye viroba.

Maiti hizo ziliokotwa Agosti 11, 2022 zikiwa kwenye viroba katika kata ya Tunguli wilayani Kilindi mkoani Tanga na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi.

Masauni ametoa agizo hilo leo Jumatano Agosti 17, 2022 baada ya kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi mkoani Tanga ilipohifadhiwa miili hiyo.

Waziri huyo amesema amesikitishwa na tukio hilo la mauaji lililotokea Wilayani humo na kuagiza Jeshi hilo lishirikiane na vyombo vingine vya usalama kuendeleza uchunguzi ili kuwakamata waliofanya mauaji hayo.

"Tukio hili ni la kinyama dhidi ya raia wenzetu wa Kitanzania, jambo hili halikubaliki kwa namna yoyote ile na sio utamaduni wetu. Kama Serikali tumelichukulia kwa uzito unaostahili na tutafanya kila linalowezekana ili vyombo vyetu vya usalama vinawabaini na kuwakamata wahusika," amesema Waziri huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amesema watu waliofanya tukio hilo linaonyesha ni wazoefu sababu namna walivyo wakunja kwenye kiroba cha kilo 50 lakini utazani nikilo 20.

Mgumba amesema kuwa dalili za awali zinaonyesha kuwa mauaji hayo hayajafanyika mkoa wa Tanga bali sehemu nyingine na kupeleka kutupa katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Sofia Jongo amesema tayari Jeshi la Polisi nchini limeshaunda kamati kwaajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya wa Wilaya, Abel Busalama amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa wanapokuwa na mashaka na kitu chochote katika maeneo yao.

Mbunge wa Kilindi (CCM) Omari Kigua amesema tukio hilo linaweza kuwakimbiza wawekezaji wanaotaka kuwekeza huku akiliomba Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliotekeleza tukio hilo la kinyama.

Chanzo: Mwananchi
Je, Ripoti ya Uchunguzi kuhusu suala hili tayari imetoka na kuwekwa wazi kwa umma???
Nini hasa kilijiri ????
 
Back
Top Bottom