Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni, ameonya watu au vikundi vya watu ambavyo vinatumia uhuru wa kutoa maoni kutoa kauli za uchochezi na zenye mrengo wa kutaka kuligawa taifa, ambapo amesema serikali haitavumilia vitendo hivyo.
View attachment 2682444
Haswaa ! Kila siku Othman Masoud (OMO), Juma Duni Haji, Ismaili Jussa wapo majukwaani wakihoji, kejeli na kutukana Muungano. Wamefikia mahali hawana hata heshima wakiita Tanganyika mkoloni mweusi...Wazanzibari kama Othman Masoud, Juma Duni, Ismail Jussa,.wakiukosoa muungano hatusikii wakitishiwa na Bwana Masauni.
..Watanganyika wakikosoa muungano ndipo Bwana Masauni anajitokeza kuelekeza vyombo vya dola dhidi yao.
Jussa majuzi kasema tugawane mbao, OMO akitoa tuhuma za uongo na Duni akitaka muungano uvunjwe
Hatukumsikia Waziri Masauni akikemea au kudai kuna tishio la usalama au kugawa Taifa kwasababu tu Wazanzibar wana haki ya kuzungumzia Muungano kadri wanavyotaka. Wazanzibar wana haki ya kudai uwepo wa KERO na zikatatuliwa tena wakiwa wenyewe. Sasa imefikia mahali wanadai hawalipi Umeme na wanakubaliwa tu kwasababu ni Wazanzibar
Akizungumza Mtanganyika tunamsikia Masauni na kauli za kutisha.
Waziri Masauni nenda kawaambie Wazanzibar hayo maneno kwanza.