LGE2024 Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024

LGE2024 Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Screenshot 2024-10-21 124843.png

View: https://www.youtube.com/live/iqytGMZ2IcA?si=lDqC4sL9BZTHvY1J

Muhtasari wa matokeo ya uandikishaji
Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura. Hii ni sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579, ambapo wanaume ni takribani 15,236,772 sawa na asilimia 48.71 na wanawake ni takribani 16,045,559, hii ni sawa na 51.29

Mwenendo wa uandikishaji
Kwa kila siku, kwa kipindi cha siku kumi, ulikadiriwa kuandikisha wastani wa asilimia 10 kwa siku hii ili kufikia lengo lililokusudiwa. Aidha mwenendo wa uandikishaji halisi ulikuwa kama ifuatavyo.

Siku ya kwanza waliandikishwa watu 3,852,994 sawa na asilimia 11.82 ya lengo la kuandikisha asilimia 10.

Siku ya pili waliandikishwa watu 2,554,375. Hii ni sawa na asilimia 7.78. Siku ya tatu waliandikishwa watu 2,660,084, hii ni sawa na asilimia 8.10.

Siku ya nne waliandikishwa watu 2,544,844 sawa na asilimia 7.75.

Siku ya tano waliandikishwa watu 2,460,664 sawa na asilimia 7.46.

Siku ya sita waliandikisha watu 2,472,605 sawa na asilimia 7.50.

Siku ya saba waliandikishwa watu 2,971,219 sawa na asilimia 9.01.

Siku ya nane waliandikishwa watu 3,409,211 hii ni sawa na asilimia …

Siku ya kumi waliandikishwa watu 4,512,336, hii ni sawa na asilimia 13.87 ya lengo siku.

Jumla ya uandikishaji kwa kila mkoa (Mikoa 26)

1. Mkoa wa Pwani takribani asilima 112.61 wamejiandikisha
2. Mkoa wa Tanga asilimia 110.82 wamejiandikisha
3. Mkoa wa Mwanza asilimia 106.58 wamejiandikisha
4. Mkoa wa Dodoma asilimia 104.19 wamejiandikisha
5. Mkoa wa Iringa asilimia 100.54 wamejiandikisha
6. Mkoa wa Kigoma asilimia 99.79 wamejiandikisha
7. Mkoa wa Morogoro asilimia 97.25 wamejiandikisha
8. Mkoa wa Songwe asilimia 97.24 wamejiandikisha
9. Mkoa wa Kagera asilimia 97.22 wamejiandikisha
10. Mkoa wa Dar es Salaam asilimia 96.80 wamejiandikisha
11. Mkoa wa Katavi asilimia 96.37 wamejiandikisha
12. Mkoa wa Shinyanga asilimia 95.46 wamejiandikisha
13. Mkoa wa Mbeya asilimia 94.26 wamejiandikisha
14. Mkoa wa Arusha asilimia 93.44 wamejiandikisha
15. Mkoa wa Kilimanjaro asilimia 93 wamejiandikisha
16. Mkoa wa Singida asilimia 92.58 wamejiandikisha
17. Mkoa wa Geita asilimia 92.36 wamejiandikisha
18. Mkoa wa Ruvuma asilimia 92.25 wamejiandikisha
19. Mkoa wa Manyara asilimia 90.35 wamejiandikisha
20. Mkoa wa Tabora asilimia 89.05 wamejiandikisha
21. Mkoa wa Lindi asilimia 87.06 wamejiandikisha
22. Mkoa wa Mtwara asilimia 84.12 wamejiandikisha
23. Mkoa wa Njombe asilimia 85.95 wamejiandikisha
24. Mkoa wa Mara asilimia 81.94 wamejiandikisha
25. Mkoa wa Simiyu asilimia 81.78 wamejiandikisha
26. Mkoa wa Rukwa asilimia 64.58 wamejiandikisha

Jumla kuu ni takribani asilimia 94.83 ya Watanzania kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea wamejiandikisha kama ilivyokusudiwa.

Undikishaji umezidi ule wa 2019
Mikoa yote 26 imefanya kazi nzuri sana. Matokeo haya yanaonesha ongezeko la idadi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha ikilinganishwa na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 ambapo waliandikishwa wapiga kura 19,681,259 tu, sawa na asilimia 86 ya lengo lililokuw limewekwa la kuandikisha wapiga kura takribani 22,916,412.

Mafanikio haya yamechagizwa na uwekezaji mkubwa katika uelimishaji na uhamasishaji katika ngazi zote ambazo OR-TAMISEMI inasimamia.

Ukaguzi orodha ya waliojiandikisha
Baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika, sasa orodha ya waliojiandikisha inabandikwa kuanzia leo katika sehemu za matangazo ya uchaguzi ili kuwawezesha wananchi kukagua orodha hiyo ili kuomba, aidha, kurekebisha majina, kubadilisha taarifa zilizopo katika orodha hiyo, au kufuta jina kwani aliyeorodheshwa amefariki.

Ukaguzi huo utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia leo tarehe 21 Oktoba hadi tarehe 27 Oktoba. Ni muhimu wananchi waliojiandikisha kujitokeza kuona orodha hiyo.

Pia, Soma:
 
Attachments

Ndugu zangu habari njema ndio hiyo juu ya muamko mkubwa wa watanzania waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya kupiga kura hapo mwezi ujao
Screenshot_20241021-142853_1.jpg
Screenshot_20241021-142907_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu habari njema ndio hiyo juu ya muamko mkubwa wa watanzania waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya kupiga kura hapo mwezi ujaoView attachment 3131574View attachment 3131575

Inahitaji akili ya mwendawazimu kumuamini huyu mhuni.
 
Mb
Ndugu zangu habari njema ndio hiyo juu ya muamko mkubwa wa watanzania waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya kupiga kura hapo mwezi ujaoView attachment 3131574View attachment 3131575

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mbona hizi ni takwimu za sensa ya nyuma? Yaani mmecopy na kurusha tu? Mbona mnachezea bongo zetu? Achana na uchafunzi tuendelee na vilaza waliopo.
 
Muhtasari wa matokeo ya uandikishaji ni kama ifuatavyo:

Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura. Hii ni sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579, ambapo wanaume ni takribani 15,236,772 sawa na asilimia 48.71 na wanawake ni takribani 16,045,559, hii ni sawa na 51.29

Mwenendo wa uandikishaji

Kwa kila siku, kwa kipindi cha siku kumi, ulikadiriwa kuandikisha wastani wa asilimia 10 kwa siku hii ili kufikia lengo lililokusudiwa. Aidha mwenendo wa uandikishaji halisi ulikuwa kama ifuatavyo.

Siku ya kwanza waliandikishwa watu 3,852,994 sawa na asilimia 11.82 ya lengo la kuandikisha asilimia 10. Siku ya pili waliandikishwa watu 2,554,375. Hii ni sawa na asilimia 7.78. Siku ya tatu waliandikishwa watu 2,660,084, hii ni sawa na asilimia 8.10. Siku ya nne waliandikishwa watu 2,544,844 sawa na asilimia 7.75. Siku ya tano waliandikishwa watu 2,460,664 sawa na asilimia 7.46. Siku ya sita waliandikisha watu 2,472,605 sawa na asilimia 7.50. Siku ya saba waliandikishwa watu 2,971,219 sawa na asilimia 9.01. Siku ya nane waliandikishwa watu 3,409,211 hii ni sawa na asilimia 10.35… Siku ya kumi waliandikishwa watu 4,512,336 hii ni sawa na asilimia 13.87 ya lengo siku.

Ndugu wanahabari, matokeo ya jumla ya uandikishaji kwa kila mkoa ni kama ifuatavyo.

1. Mkoa wa Pwani takribani asilima 112.61 wamejiandikisha

2. Mkoa wa Tanga asilimia 110.82 wamejiandikisha

3. Mkoa wa Mwanza asilimia 106.58 wamejiandikisha

4. Mkoa wa Dodoma asilimia 104.19 wamejiandikisha

5. Mkoa wa Iringa asilimia 100.54 wamejiandikisha

6. Mkoa wa Kigoma asilimia 99.79 wamejiandikisha

7. Mkoa wa Morogoro asilimia 97.25 wamejiandikisha

8. Mkoa wa Songwe asilimia 97.24 wamejiandikisha

9. Mkoa wa Kagera asilimia 97.22 wamejiandikisha

10. Mkoa wa Dar es Salaam asilimia 96.80 wamejiandikisha

11. Mkoa wa Katavi asilimia 96.37 wamejiandikisha

12. Mkoa wa Shinyanga asilimia 95.46 wamejiandikisha

13. Mkoa wa Mbeya asilimia 94.26 wamejiandikisha

14. Mkoa wa Arusha asilimia 93.44 wamejiandikisha

15. Mkoa wa Kilimanjaro asilimia 93 wamejiandikisha

16. Mkoa wa Singida asilimia 92.58 wamejiandikisha

17. Mkoa wa Geita asilimia 92.36 wamejiandikisha

18. Mkoa wa Ruvuma asilimia 92.25 wamejiandikisha

19. Mkoa wa Manyara asilimia 90.35 wamejiandikisha

20. Mkoa wa Tabora asilimia 89.05 wamejiandikisha

21. Mkoa wa Lindi asilimia 87.06 wamejiandikisha

22. Mkoa wa Mtwara asilimia 84.12 wamejiandikisha

23. Mkoa wa Njombe asilimia 85.95 wamejiandikisha

24. Mkoa wa Mara asilimia 81.94 wamejiandikisha

25. Mkoa wa Simiyu asilimia 81.78 wamejiandikisha

26. Mkoa wa Rukwa asilimia 64.58 wamejiandikisha

Nina maswali:
1. Hivi majukumu ya Tume huru ya uchaguzi ni yepi?
2. Je, malengo ya uandikishaji yaliwekwa na nani kwa vigezo vipi?
3. Je, Kuna mahali popote online wanaotaka kujiridhisha na mwenendo wa uandikishaji na baadae upigaji kura wanaweza kupata orodha ya majina na hizo takwimu?

NB: ccm inaandaliwa mazingira ya ushindi kwa % sawa na za Tanga.
 
Back
Top Bottom