DUBULIHASA
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 4,446
- 8,215
Kwenda kujiandikisha ni kama kuhudhuria sherehe za P. Diddy hasara ni nyingi kuliko faida....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukizingatia uandikishaji ulikua ukifanyika kwa mkono......labda kuna muujizaZoezi limefungwa jana jioni eti leo tayari wana takwimu za nchi nzima, huu uongo wa kipumbavu sana.
101.13%Watishaji ni Pwani kwa maana ya utishaji! Labda, kama una takwimu zako nyingine za mfukoni!
Wanatuchukulia watanzania kama watoto wa chekechea vile uwongo wa wazi kabisa mtu anautangazia umma.Ukizingatia uandikishaji ulikua ukifanyika kwa mkono......labda kuna muujiza
Utakuwa Mkoa wa 27 huo!101.13%
Hakuna wajinga 31m hapa Tanzania. Hiyo idadi ya kupika kadanganyeni mafala.Dogo usipende kukurupuka hovyo hovyo kama umelewa gongo
Huo ni uongo ama waandikishaji wamedanganya. Foren ya kwenye nida ndo ilikuwa kubwa zaidi lkn watu hawakufika idadi hiyo kama sijakosea.Inahitaji akili ya mwendawazimu kumuamini huyu mhuni.
NIDA walikuwa wakikusanyika sehemu chache.kujiandikisha kura ni sehemu nyingi ndio maana hungeona misururu mirefuHuo ni uongo ama waandikishaji wamedanganya. Foren ya kwenye nida ndo ilikuwa kubwa zaidi lkn watu hawakufika idadi hiyo kama sijakosea.
Sawa lkn yote Kwa yote hizo takwimu wamepika Tena Kwa gesNIDA walikuwa wakikusanyika sehemu chache.kujiandikisha kura ni sehemu nyingi ndio maana hungeona misururu mirefu
Muhtasari wa matokeo ya uandikishaji
Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura. Hii ni sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579, ambapo wanaume ni takribani 15,236,772 sawa na asilimia 48.71 na wanawake ni takribani 16,045,559, hii ni sawa na 51.29
Mwenendo wa uandikishaji
Kwa kila siku, kwa kipindi cha siku kumi, ulikadiriwa kuandikisha wastani wa asilimia 10 kwa siku hii ili kufikia lengo lililokusudiwa. Aidha mwenendo wa uandikishaji halisi ulikuwa kama ifuatavyo.
Siku ya kwanza waliandikishwa watu 3,852,994 sawa na asilimia 11.82 ya lengo la kuandikisha asilimia 10.
Siku ya pili waliandikishwa watu 2,554,375. Hii ni sawa na asilimia 7.78. Siku ya tatu waliandikishwa watu 2,660,084, hii ni sawa na asilimia 8.10.
Siku ya nne waliandikishwa watu 2,544,844 sawa na asilimia 7.75.
Siku ya tano waliandikishwa watu 2,460,664 sawa na asilimia 7.46.
Siku ya sita waliandikisha watu 2,472,605 sawa na asilimia 7.50.
Siku ya saba waliandikishwa watu 2,971,219 sawa na asilimia 9.01.
Siku ya nane waliandikishwa watu 3,409,211 hii ni sawa na asilimia …
Siku ya kumi waliandikishwa watu 4,512,336, hii ni sawa na asilimia 13.87 ya lengo siku.
Jumla ya uandikishaji kwa kila mkoa (Mikoa 26)
1. Mkoa wa Pwani takribani asilima 112.61 wamejiandikisha
2. Mkoa wa Tanga asilimia 110.82 wamejiandikisha
3. Mkoa wa Mwanza asilimia 106.58 wamejiandikisha
4. Mkoa wa Dodoma asilimia 104.19 wamejiandikisha
5. Mkoa wa Iringa asilimia 100.54 wamejiandikisha
6. Mkoa wa Kigoma asilimia 99.79 wamejiandikisha
7. Mkoa wa Morogoro asilimia 97.25 wamejiandikisha
8. Mkoa wa Songwe asilimia 97.24 wamejiandikisha
9. Mkoa wa Kagera asilimia 97.22 wamejiandikisha
10. Mkoa wa Dar es Salaam asilimia 96.80 wamejiandikisha
11. Mkoa wa Katavi asilimia 96.37 wamejiandikisha
12. Mkoa wa Shinyanga asilimia 95.46 wamejiandikisha
13. Mkoa wa Mbeya asilimia 94.26 wamejiandikisha
14. Mkoa wa Arusha asilimia 93.44 wamejiandikisha
15. Mkoa wa Kilimanjaro asilimia 93 wamejiandikisha
16. Mkoa wa Singida asilimia 92.58 wamejiandikisha
17. Mkoa wa Geita asilimia 92.36 wamejiandikisha
18. Mkoa wa Ruvuma asilimia 92.25 wamejiandikisha
19. Mkoa wa Manyara asilimia 90.35 wamejiandikisha
20. Mkoa wa Tabora asilimia 89.05 wamejiandikisha
21. Mkoa wa Lindi asilimia 87.06 wamejiandikisha
22. Mkoa wa Mtwara asilimia 84.12 wamejiandikisha
23. Mkoa wa Njombe asilimia 85.95 wamejiandikisha
24. Mkoa wa Mara asilimia 81.94 wamejiandikisha
25. Mkoa wa Simiyu asilimia 81.78 wamejiandikisha
26. Mkoa wa Rukwa asilimia 64.58 wamejiandikisha
Jumla kuu ni takribani asilimia 94.83 ya Watanzania kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea wamejiandikisha kama ilivyokusudiwa.
Undikishaji umezidi ule wa 2019
Mikoa yote 26 imefanya kazi nzuri sana. Matokeo haya yanaonesha ongezeko la idadi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha ikilinganishwa na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 ambapo waliandikishwa wapiga kura 19,681,259 tu, sawa na asilimia 86 ya lengo lililokuw limewekwa la kuandikisha wapiga kura takribani 22,916,412.
Mafanikio haya yamechagizwa na uwekezaji mkubwa katika uelimishaji na uhamasishaji katika ngazi zote ambazo OR-TAMISEMI inasimamia.
Ukaguzi orodha ya waliojiandikisha
Baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika, sasa orodha ya waliojiandikisha inabandikwa kuanzia leo katika sehemu za matangazo ya uchaguzi ili kuwawezesha wananchi kukagua orodha hiyo ili kuomba, aidha, kurekebisha majina, kubadilisha taarifa zilizopo katika orodha hiyo, au kufuta jina kwani aliyeorodheshwa amefariki.
Ukaguzi huo utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia leo tarehe 21 Oktoba hadi tarehe 27 Oktoba. Ni muhimu wananchi waliojiandikisha kujitokeza kuona orodha hiyo.
Pia, Soma:
- Waziri Mchengerwa afafanua kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa utakaofanyika Novemba 27, 2024LGE2024 - Waziri Mchengerwa atangaza tarehe ya kuchukua na kurudisha Fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku zaongezwa
- Waziri Mchengerwa atangaza tarehe ya kuchukua na kurudisha Fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku zaongezwa
- Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024
- Waziri Mchengerwa atangaza tarehe ya Ukomo kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa, watakiwa kukabidhi nyaraka za ofisi
acheni uhuni wa kiccm kutuletea takwimu ya mapishi ya kwenye makaratasiDogo usipende kukurupuka hovyo hovyo kama umelewa gongo
maanayake ni figures beyond imaginationSamahani Wana JF naomba mnisaidie kidogo hivi kihesabu 112.61% maana yake Nini?
Upumbavu uliokithiri kabisa! Matokeo ya maporini huko wameyapataje haraka hivyo? Hii serikali wanatuona sisi ni Mazezeta Nini? Wakome kabisa kudanganya watu!Zoezi limefungwa jana jioni eti leo tayari wana takwimu za nchi nzima, huu uongo wa kipumbavu sana.
utashangaa siku ya kupiga kura hutaona vituoni watu kwenye foleni wakipiga kura ila ajabu ni kwamba utaambiwa watu walijitokeza kwa wingi na sisiemu imeshinda kwa 99.9%Na kura mil 30 ni za ccm,wapinzani watagawana hizo mil 1
Ccm oyeeeeee.