LGE2024 Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024

LGE2024 Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
utashangaa siku ya kupiga kura hutaona vituoni watu kwenye foleni wakipiga kura ila ajabu ni kwamba utaambiwa watu walijitokeza kwa wingi na sisiemu imeshinda kwa 99.9%
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

Ccm mbele kwa mbele
 
Wanatuchukulia watanzania kama watoto wa chekechea vile uwongo wa wazi kabisa mtu anautangazia umma.
Jana jioni alisema ni 26m+, baada ya kuona watu wamehoji kapata wapi hiyo figure kwa haraka hivyo, leo ameona aongeze cha juu ili ionekane ndio idadi kamili๐Ÿ˜‚ Halafu hapo ujitokeze kwenye uchaguzi ukitegemea matokea ya kweli kutangazwa.
 
utashangaa siku ya kupiga kura hutaona vituoni watu kwenye foleni wakipiga kura ila ajabu ni kwamba utaambiwa watu walijitokeza kwa wingi na sisiemu imeshinda kwa 99.9%
Sasa ukitaka ucheke, usishangae wapiga kura kutangazwa wamejitokeza 32m+. Yaani idadi kubwa kuliko hiyo. Watu wanaopika data hivyo hata wakikuambia ufanisi wa serekali unaweza kuamini vipi?
 
Ndugu zangu habari njema ndio hiyo juu ya muamko mkubwa wa watanzania waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya kupiga kura hapo mwezi ujaoView attachment 3131574View attachment 3131575

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mkwe

Ova
 
Duh, maisha haya.

Leo ndo nagundua kulikua na zoezi la kujiandikisha kupiga kura.

Kuna wakati, unakua so fucken busy, Mpaka unajikuta unamiss important dates in the society.
 
Hivi huyu mkwe anajua hesabu kweli? Hajui kuwa 112% ni ndogo kuliko 64.58%?
 
Hahaha madaftari huwa wanatunza ccm, hivyo takwimu hizi zisiwape shida. Ni zile zile miaka yote,

Hata msinge jiandikisha wangesema mlijiandikisha kwa asilimia 99.
 

WAZIRI MCHENGERWA - WANANCHI MILIONI 26.7 WAMEJIANDIKISHA, SAWA NA ASILIMIA 81.15 YA LENGO LA UANDIKISHAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema jumla ya wapiga kura 26,769,995 wamejiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, sawa na asilimia 81.15 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579 ikiwa ni masaa machache kufikia ukomo wa zoezi hilo ifikapo tarehe 20 Oktoba 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa tathmini hiyo ya uandikishaji wa wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha kujiandikisha cha Michikichini Kijiji cha Umwe Kaskazini Wilayani Rufiji.

โ€œMpaka tarehe 19.10.2024 ninaozungumza jumla ya uandikishaji kwa wanaume ni 13,033,988 sawa na asilimia 48.69 na wanawake ni 13,736,007 sawa na asilimia 51.31 ya watu wote waliojiandikisha kuanzia tarehe 11 hadi 19 Oktoba, 2024โ€, Mhe. Mchengerwa ameeleza.

Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa, mwenendo huo wa uandikishaji ni mzuri na kama utaendelea hivyo ambapo kwa siku ya leo ndio mwisho wa uandikishaji ni wazi kuwa lengo la kuandikisha wapiga kura 32,987,579 litafikiwa.

โ€œNichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza Watanzania wote waliojitokeza kujiandikisha hadi muda huu ninaotoa tathmini ya uandikishaji, kwani tayari wamejiwekea mazingira kubalika kisheria ya kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa wanaowataka ifikapo tarehe 27 Oktoba 2024,โ€Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Akianisha mikoa mitano yenye asilimia kubwa ya uandikishaji hadi kufikia tarehe 18 Oktoba, 2024 ambayo ilikuwa ni siku ya 8 ya uandikishaji, Mhe. Mchengerwa amesema mkoa wa Tanga umefikia asilimia 101.13% ya malengo, mkoa wa Pwani umefikia asilimia 98.74% ya malengo, mkoa wa Mwanza umefikia asilimia 94.09% ya malengo, mkoa wa Dar es Salaam umefikia asilimia 86.66% ya malengo na mkoa wa Dodoma umefikia asilimia 80.63% ya malengo.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lilizinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan aliyejiandilkisha katika Kitongoji chake cha Sokoine Kijiji cha Chamwino siku ya tarehe 11 Oktoba, 2024.
 

Attachments

  • GaZWzi7XUAAMOSF.jpg
    GaZWzi7XUAAMOSF.jpg
    126.6 KB · Views: 0
  • GaWHlQoW4AEP33S.jpg
    GaWHlQoW4AEP33S.jpg
    399.3 KB · Views: 0
  • GaWHlQlXQAE8bdH.jpg
    GaWHlQlXQAE8bdH.jpg
    598.2 KB · Views: 0
  • GaWHlQpWcAA-KzB.jpg
    GaWHlQpWcAA-KzB.jpg
    696.7 KB · Views: 0
  • Gaa6rzAWkAESl62.jpg
    Gaa6rzAWkAESl62.jpg
    211.1 KB · Views: 0
Back
Top Bottom