Waziri Mchengerwa ukimsikiliza anaonesha utofauti mkubwa na wengine kimtazamo wa 'kifenotipia' ila hatujui kuhusu 'Jenotipia' yake

Waziri Mchengerwa ukimsikiliza anaonesha utofauti mkubwa na wengine kimtazamo wa 'kifenotipia' ila hatujui kuhusu 'Jenotipia' yake

Hana msaada wowote huyu waziri,kipande cha Nyamwage-Utete(Makao ya wilaya) barabara ya vumbi ameshindwa kuweka hata kokoto.Tunapigwa vumbi,Dar tunafika tumejaa vumbi(ngonja).


Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kumbe, Sasa mbona hakuna shida au wanataka waachane kisa mama kawa Rais?
Ndugu yangu, watu wenye umasikini wa fikra ndio wanaokaa kufikiria hela huwa inaletwa kwa kukaa kupiga majungu vijiweni, na itawakosti sana maana badala ya kufikiria namna ya kujikwamua na hali zao wao wanatumia huo muda kulalamika na kulaumu mtu aliyeoa kwa mapenzi yake .

Majungu sio mtaji .
 
Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Waziri huyu kwa mara ya kwanza nilimfahamu pale alipoleta hoja Bungeni akitaka kujua kwanini mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere Rufiji (JNHPP) utakaotoa ajira ya zaidi 7,000 na serikali kuwekeza zaidi ya TZS 6.55trilioni unafanyika katika Wilaya ambayo haina hata benki ya Serikali au hata benki binafsi,

Hoja ile imepelekea Serikali kupeleka benki ya Maendeleo katika wilaya hiyo Kongwe na hata leo ukipita hapo njiani utaiona banki hiyo,hapa ndio nilianza kuona kitu kilichopo ndani ya Waziri huyu,

Hebu Msikilize hapa anachowaambia watumishi wenzake, Hongera Rais Samia Suluhu Hassan kutuletea viongozi wa aina hii,

Watumishi chapeni kazi kwa bidii na maarifa kama ni mtetezi wa stahiki zenu zote hakika mnae,


Tunakupongeza Waziri
 
Back
Top Bottom