Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Hahahahaha
 
Usaili wa nini? Mtu hapati ajira mpaka baada ya muda wa matazamio kupita. Muda huo ndio unatakiwa kutumika kuamua kama mtu anastahili hiyo ajira au la.

Amandla...
Muda wa matazamio (Probation time/period) huwa unasimamiwa ipasavyo!!? Kama ni ndiyo ni kwa nini bado kuna wahadhirii wanaoonekana dhahiri shayiri kwamba viwango vyao viko chini sana kufundisha kwenye vyuo vikuu??
 
Mkuu wenye GPA kubwa watakusaport wenye GPA ndogo watakupinga, Africa si sahihi kwa wenye high grades in school ila utafanikiwa saana ukiwa na emotional intelligency kwani most people are not logic.
 
Mkuu wenye GPA kubwa watakusaport wenye GPA ndogo watakupinga, Africa si sahihi kwa wenye high grades in school ila utafanikiwa saana ukiwa na emotional intelligency kwani most people are not logic.(they don't see the logic?).
Usomi wa watu wetu una matatizo sana. Usomi unatakiwa ulete matokeo chanya kwenye taaluma uliyomo. Hii mikataba ya kimagumashi tunayoingia kila siku unadhani ni kwa sababu wanaotia sahihi kwa niaba yetu wameishia darasa la saba kama kina siye yakhe!!

Unaijua GPA ya Mwigulu? Inakuwaje kila siku analaumiwa kwa kutofanya mambo chanya ya kichumi kwenye nchi yetu? Nenda Chuo Kikuu cha Dar es salaam kaulize GPA ya Profesa Kabudi ambaye hivi karibuni amekiri kuwa alikuwa anatoa takwimu upogo za madai yetu dhidi ya Barricks. Hao wanahukumiwa kwa GPA zao au kwa matendo yao?

Hakuna anayebeza usomi bali kinachosisitizwa hapa ni kwamba, kilichomo kwenye vyeti vyako, kidhihirike kwa weledi wa matendo yako kwenye fani husika.
 
Hii sasa ni hoja lakini haihusiani na ile ya usaili kindakindaki. Nchi yetu mfumo wa kuwalea wasomi wetu ni mbovu. Mazoezi kwa vitendo (internship) ndiyo humkomaza msomi. wanaofanya ni madaktari tu.
Hii ndio hoj
Makampuni yote yateknolojia makubwa hayaajiri Degree na Masters yanaajili relevant experience

Kwa nchi za nje mtu mwenye PhD ana relevance experience kubwa sana.
Acha uongo wewe, mfano mzuri ni kwenye oil and gas, wanaajiri masters na PhD. Ww unazungumzia makampuni ya wahindi.
 
Nashare Job description ya kupata kazi facebook

Responsibilities/ Summary:

Meta's Reality Labs is looking for a Python Software Engineer specifically within DevOps/Build environments. This role is a critical function for Meta as you will be writing scripts to tie internal services together within a continuous integration and build infrastructure environment. You would be working with various teams, including the central DevOps and Infrastructure teams. You will write python scripts to interact and add more features to existing services at the infrastructure level. Meta operates within its own internal proprietary DevOps & Build tools and cloud infrastructure environment. We are looking for someone who can work in an ambiguous but collaborative environment and able to learn new technologies fast to contribute to Meta's next generation development capabilities. You will be joining the Agios team to help lead/contribute to engineering efforts from design to implementation, solving complex technical challenges around engineering productivity and velocity. You will design and build advanced automated build, test, release, and operations infrastructure. Please note that this role is fully funded and secure. This team specifically has continuously grown over the past few years and does not plan on slowing down its expansion. This team is very critical for Meta's research and growth as a company.





Required Qualifications

● 3+ years of professional Software Development experience

● 3+ years of industry experience developing/scripting in Python (must be proficient)

● Strong industry experience in at least one of the following development areas:

○ Configuration

○ Build infrastructure

○ Continuous integration infrastructure

○ Building tools/ DevOps

Kati ya Degree, Master na PhD wengi wengi wenye G.P.A kubwa hawatapa kazi
 
Kwa nchi yetu hali iko ivo ama haiko ivo na tatizo ni nini??
PhD wa Tanzania ni vilaza hata wengi hawajui why wanasoma wanayojifunza sababu target yao ni kufaulu mtihani, kupanda vyeo na si kuvumbua theory na njia mpya.

Also there is the little to know enough funds for research and development

Mfano Ulaya na Marekani wana Particle accelerator labs ambazo zinacost zaidi ya GDP yetu mara kadhaa
 
Mwenye GPA ya 2, akimshinda mwenye GPA kubwa kutumia python nakufa 😀😀😀😀😀😀aise. Python programming hizo ni hesabu. Mwenye GPA ya 2 hawezi mshinda hesabu mwenye GPA kubwa.
 
Mwenye GPA ya 2, akimshinda mwenye GPA kubwa kutumia python nakufa 😀😀😀😀😀😀aise. Python programming hizo ni hesabu. Mwenye GPA ya 2 hawezi mshinda hesabu mwenye GPA kubwa.
1. Kwenye hiyo kazi hakuna sehemu ambayo wamesema uwe na Degree, Masters au PhD

wakitokea mtu ambaye hajawahi kufanya kazi popote (Degree na Masters) au hata mwalimu wa chuo akiomba hiyo kazi hatokuwa shortlisted hata kama ana G.P.A ya tano na badala yake atachukuliwa mtu mwingine ambaye hana hiyo vingine vyote ila amewahi kufanya kazi mbili miaka 3 iliyopita
 
Juzi tu hapa watu walikuwa wanakataaa waalimu wa vyuo vikuu kufundisha Law School of Tanganyika badala yake wakataka mawakili na majaji ndiyo wapewe fursa ya kutoa mihadhara kwenye shule hiyo ya sheria Tanganyika
 
Kwa hiyo mtu mwenye gpa kubwa na mkali kwenye python plus 4 years of experience hatapewa kazi kwa sababu ana gpa kubwa?

Mkuu sorry lakini ila inaonesha una kajentomeni gpa so kanakufanya uchukie gpa kubwa.
 
Si lazima kwanza ubadilishe mfumo wa kuwapata watoa elimu ndipo upate matokeo bora!!??
Uko sahihi. Lakini sio kwa usaili peke yake. Wote tunajua namna ambavyo interviews zinavyopindishwa ili kumpata mtu fulani. Njia bora zaidi ni kupima utendaji wao wakiwa kazini pamoja na feedback kutoka kwa wanafunzi na sehemu ambako wanafunzi wanaenda kufanya kazi. Kwa mfano sasa hivi Faculty ya Sheria inatakiwa ifumuliwe ili kupata matokeo tunayotegemea. Ingawa mara nyingi wanasingiwa wanafunzi kuwa hawana akili tatizo hasa ni kwa hao watoa elimu.

Amandla...
 
shida ya hii nchi uhuni mwingi , ivyo ivyo wanavyotaka wao bado kuna wahuni watawapitisha wasiostahili
 
Muda wa matazamio (Probation time/period) huwa unasimamiwa ipasavyo!!? Kama ni ndiyo ni kwa nini bado kuna wahadhirii wanaoonekana dhahiri shayiri kwamba viwango vyao viko chini sana kufundisha kwenye vyuo vikuu??
Sasa huko ndiko kwenye tatizo. Hata huyo mtakayempata kwa usaili asiposimamiwa vizuri matokeo yatakuwa haya haya. Matatizo yetu ni kuwa hatufuatilii utendaji wa kazi baada ya ajira kiasi kuwa hiyo probation period imekuwa kama formality tu.

Amandla...
 

Naunga mkono hoja yako.
 

Wewe unaongelea uwezo wa kitaaluma tu.
Uhadhiri unahitaji zaidi ya huo.
Mhadhiri ajue kupresent alichonacho, awe diverse culturally, awe up to date na technology (at least zinazohusu taaluma yake) n.k.
Sasa mtu ana GPA ya 4.5 ila hawezi hata kujibu maswali ya wanafunzi kwa ufasaha kisa lugha. Hapo tuna mhadhiri?
 
Kwa hiyo mtu mwenye gpa kubwa na mkali kwenye python plus 4 years of experience hatapewa kazi kwa sababu ana gpa kubwa?

Mkuu sorry lakini ila inaonesha una kajentomeni gpa so kanakufanya uchukie gpa kubwa.
1. Nina G.P.A kubwa za Engineering na Physics
2. Nimefanya kazi kwenye kampuni kubwa ndani na nje ya TZ.
3. Ninawajua wenzangu tuliosoma nao na ninajua uwezo wao

Paragraph ya kwanza umeongea vitu viwili tofauti...

Kuna mtu anaweza kuwa na G.P.A na akajua Python na mwingine asiye na G.P.A kubwa na akajua Python.

1. Hakuna chuo Tanzania kinafundisha Python chuoni, so mtu ambaye anajua Python na alipata G.P.A kubwa it means ni Extra cariclum activity ambayo ni nje ya shule.

2. Context ya kupost hiyo job description ni kuonesha kwamba lazima mindset za watu zibadilishwe ili wasiogope kusoma kwa ajili ya G.P.A badala yake wahangaike kupata relevant skills.

3. Ni rahisi sana mwanafunzi kupata G.P.A nzuri, narudia ni rahisi sana ru
 
Waache mapuuza wameharibu elimu kwa kufaulisha vilaza vilaza huku chini sasa wanataka waharibu na taasisi za juu?
Gpa ndio mpango mzima tunahitaji watu wenye sophisticated brain wa handle vyuo. Wasitake tujazie vilaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…