Iamwhoiamm
JF-Expert Member
- Oct 18, 2022
- 503
- 887
Jee pia ni kipimo cha mtu kuwa mhadhiri bora??ukiondoa rushwa GPA ni kipimo kizuri Cha competency ya mwanafunzi ..
Sasa hapo tatizo liko wapi? Una GPA yako kubwa unakataa nini kufanyiwa usaili kujua upande mwingine ukiachilia mbali hayo katokeo yako ya darasani.Kweli nchi inaenda kubaya sana. Kwa hiyo wakifanyiwa usaili ndio elimu inakua bora. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3].
Mtu mwenye GPA kubwa kwa vyuo kama SUA, MZUMBE na UDSM huyo anauwezo mkubwa, haina haja ya kujiuliza mara mbili.
Nenda uendako, kwenye usaili watu wanakalili na kufaulu baada ya hapo wanasahau. Ila mwenye GPA kubwa ni mtu mwenye uwezo.
Haiwezekani mtu kidato cha Nne abamize one ya saba, kidato cha sita one ya nne na chuo GPA ya 4.6. Useme hana uwezo badala yake utegemee kumpima kwenye usaili Ili kupima uwezo wake.
Tuwekeze kwenye practical zaidi
Ndio ,,Kwa mfumo wa CBET huwezi pata GPA nzuri kama practical module umevurunda .... tatizo la vyuo vyetu ni rushwa ya ngono ,pesa ,au kubebana ..Jee pia ni kipimo cha mtu kuwa mhadhiri bora??
Hii hoja imepingwa sana kwamba ni kujitetea kwa watu wasio na akili.Ukiona mtu ana GPA ya 3.5 kwenye vyuo vya CBET mheshimu sana
Hata hivo ana akili mkuu... mtu uwe profesa na undergraduate ulitoka na First class halafu useme eti hana akili?Tatizo la mkenda huwa anajiona yeye anaakili sana
Umejipotosha bwana Mzee. Waziri hajasema wenye GPA ndogo watachukuliwa. Kasema hao hao wenye GPA kubwa watasailiwa kwa kina kwanza kabla ya kupewa kazi ya kuwa waadhiri ama wakufunzi wasaidizi. Tatizo liko wapi??Waziri anachosema ni ujinga mtupu
Mfano huajiri mtu kwa GPA unaajiri Tutorial Assistant umempata mmoja mzuri sana kwenye presentation lakini ana GpA ya chini sana ambayo haimuwezeshi hata kujiunga kwenda kusoma Masters degree sababu hakidhi vigezo anataka huyo aje kufia rank ya tutorial assistant atapandaje juu kuwa mhadhiri bila kuwa na Masters ?
Kwanza kabisa u Profesa ni ualimu. Pili, hawa jamaa wakiingia kwenye siasa kwa kiasi fulani wanapoteza dira zao. Kama academician alitakiwa ajiulize kwa undani kiini cha matatizo anayozungumzia. Kwa kukimbilia kwenye usaili ni kutafuta majawabu mepesi kwa maswali magumu, kitu ambacho wanasiasa wanafanya. Kwa mtazamo wangu tatizo sio walimu wapya bali ni wale waliopo ( pamoja na yeye) na tamaduni za ufundishaji katika vyuo vyetu. Mtu akiwa Profesa au akiwa na Ph.D anaona amemaliza na anajua kila kitu. Hataki kuwa challenged na vijana anaowafundisha akisahau kuwa mazingira wanayokulia ni tofauti kabisa na ambayo wao walikulia.mjadala sasa umenoga... Asante sana Fundi Mchundo maana unaandika mantiki sana kwenye kona mbali mbali za mjadala huu.
Ni kweli kwamba Chuo kikuu hufundishwa ni kwa nini matokeo fulani yanatokea wakati vyuo vingine wanafundishwa kufanya kitu ili kitokee kitu kingine. Lakini hoja yenyewe ni kweli hali iko ivo??
Maana kama Profesa aliyehudumu chuo Kikuu baada ya kupata alama za juu sana chuoni hapo akiwa mwanafunzi, (kwa maelezo ya Naantombe Mushi, )anaona kuna upungufu kwenye kusaili wahadhiri vyuoni, hiyo nadharia ya vyuo vikuu kutoa watu hao wenye kujua ni kwa nini matokeo fulani hutokea, inafikiwa kweli??
Nenda katafte historia ya Gregor Mendel father of genetics.. sio tuu gpa mwamba alifeli na kufeli lkn leo mchango wake unatambulika worldwideGPA itaendela kuwa kigezo cha kuita watu kwenye usaili na kuajirii Hilo halipingiki ....
Siwezi kuita mjinga mwenye gpa ya 2.0 wakati mezani nina CV ya watu wenye gpa za 4.0 and above et Kwa kujipa Moyo anaweza kuwa na akili ...
Kama ameshindwa kuwa na kumbukumbu za alichokuwa anafundishwa shuleni na kujibu mtihani na kufaulu ataweza nin kazin ..
Harafu fuatili watu wengi wenye gpa za 2.0 ni weupe vichwani kama ilivyo kwenye karatasi ,gpa ya chuo ,matokeo ya form six ,matokeo ya form four havijawahi kudanganya [emoji3][emoji3][emoji3]...
Nioneshe vyetu vyako vyote hivyo nikuambie uwezo wako wa kufikili na kuchambua Mambo ....
Wameruhusu kuichezeq elimu ya o level na a level kwa kigezo cha kuongeza ufaulu.. leo hii mtihan wa kidato cha nne watoto wanafaulu tuu.. kuna mjomba wang kapiga form 4 one ya 10 mwaka jana ila ukikaa nae ukimpa maswali tuu ya kawaida hola, plus kumfundisha tuu mdogo wake changamoto shule ndogo.. unategemea dogo km huyo akifka chuo atakuaje??Ninachokueleza ni kwamba graduates, matokeo yao ya makaratasi hayafanani na kilichomo kichwani, Nawapokea sana, nawapa nafasi sana, field wanaziomba sana, kujitolea na ajira wanaomba hivyo nakutana nao mara nyingi tu na wakati mwingine yule ambaye kwenye makaratasi wala haonekani mwenye elimu kubwa na diploma ya vyuo visivyo rasmi anafanya vizuri tu kuzidi vijana wa IAA, Mzumbe, UD, UDOM SAUT n.k.
Mfano wa swali jepesi katika field ya biashara ambalo mwanachuo yoyote esp mwenye GPA kubwa hakupaswa kushindwa kulijibu: Ni nyaraka zipi zinatumika kufanya miamala baina ya raia wawili walio nchi tofauti wakati wanafanya biashara?
Hii ni international trade, Mtu ana BBA na GPA fiirst class lakini anajibu mpaka unaona huruma, wakati mwingine unadhani ni panic unamwambia relax, kunywa maji unampigisha hadithi nyingine ili asiumie kisha ukishaona karudi normal unaruhusu panel iendelee ila still wengi wanashindwa na hapo swali limeulizwa kwa kiswahili.
BOSS NAKUELEZA, TUNA TATIZO LINALOPASWA KUFANYIWA KAZI. TUNAPOELEKEA IKITOKEA PAKAWA NA UHURU WA KUAJIRI BAINA YA EA VIJANA WETU WATAUMIA SANA.
Upo sahihi sana Jombaa. Huyo huyo Mkenda akiwa mwalimu na mkuu wa idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar es Salaam walikuwa wanalazima aajiriwe mwanamke kisa idara ilikuwa na wanawake wawili tu mke wake na aliyekuwa naibu gavana wa benki kuu kipindi hicho. Maanake hapo una-risk kuweka mtu hata mwenye uwezo mdogo kwa ubaguzi wa kijinsia.shida ya hii nchi uhuni mwingi , ivyo ivyo wanavyotaka wao bado kuna wahuni watawapitisha wasiostahili
Kiukweli nakuunga mkono, wacha iendelee hivyo hivyo! Pengine hii mentality imeenea kutokana na ushenzi unaoendelea vyuoni.Unajiliwaza tu mkuu. Kigezo ndio hicho. Minimum GPA ni 3.8. Hapo ndio unqualify walau kuwa shortlisted kwa ajili ya interview. Na hizo ni guidelines za TCU. Hata kama unahisi una uwezo wa kufundisha, maadam hujakidhi hicho kigezo kimojawapo, sahau kuitwa kwny interview. Halafu tuache excuses za kufeli kwetu kwa kubeza waliofaulu kutuzidi. Mnatumia kigezo gani kuwa mwenye GPA kubwa kafake na mwenye GPA ndogo ni genuine? Nani aliyeingiza hii mentality kwa jamii?
Daaa. Tuna tatizo sana mkuu.Wameruhusu kuichezeq elimu ya o level na a level kwa kigezo cha kuongeza ufaulu.. leo hii mtihan wa kidato cha nne watoto wanafaulu tuu.. kuna mjomba wang kapiga form 4 one ya 10 mwaka jana ila ukikaa nae ukimpa maswali tuu ya kawaida hola, plus kumfundisha tuu mdogo wake changamoto shule ndogo.. unategemea dogo km huyo akifka chuo atakuaje??
Tumerahisisha sn elimu yetu