Waziri Mkenda hawa walimu walikosea nini hadi wapewe hii adhabu ya kuporwa madawati ya kukalia?

Kama waliweza kumnunulia fomu ya uchaguzi mama inakuwaje washindwe kujinunulia viti vyao, usiwatetee hao, pia wapigwe marufuku kukalia vitabu kwani kutabu hakisomwi kwa makalio kinasomwa kwa macho.
 
Hivi kwanini hawa madiwani sijui watendaji wanapenda sana kuwaoshea walimu? Wamewafanya kama vile ndo wanyonge wao yaani
Mbona huwa hawajaribu kwenda kwenye kada zingine kuleta utemi wao? Huu udhalilishaji wanaofanyiwa walimu inatakiwa utaratibu uangaliwe upya maana wamekua na maboss wengi sana kuliko watetezi kiasi kwamba wanafanywa kama watu wasio na maana yoyote
 
Hivi kumbe mtendaji wa Mtaa ni Boss wa Mwalimu, yaani kweli unamaliza ujana wako kusomea BAed kuja kuendeshwa na takataka za certificate zinazosubiri rushwa na hela za wauza viwanja ili ziishi.... ningemchapa kofi huyo mtendaji na kazi yake naacha apo
 
Aliona kuliko apoteze kazi bora achezee bakora kwa hiyari akirudi nyumbani akakandwe michirizi ya bakora za mapaja na mke wake

Sasa siku zote hizo kawa mtoro karudi kasamehewa kirahisi hivyo inamaana taarifa za utoro zilikua hazitolewi kwenye mamlaka za juu?
 
Waweza kuta walikula hela ya kununulia samani za shule na hapo wamewajibishwa.

Mwalimu huyo wa kawaida ndo amepewa hela? Kwa lipi labda! Kua basi
Hiyo ni dhana tu. Lazima ipo sababu "ya maana" iliyowapelekea 'kuishi mavumbini' na wakaridhia.

Nilitangulia kusema, habari inayotolewa kwa upande mmoja hufikirisha na kupelekea kutoa maoni yasiyo sahihi sana.

Ujue nini, hapa kila mmoja anaunga unga dot ili kutafuta sababu iliyopelekea kutokea jambo hilo, maana mleta mada katuacha kwenye ombwe.
 
Leak , njoo na taarifa kamili.

Mkuu, GGM imejitahidi kusaidia kila kona, kweli hata wangewaomba wangewanyima! Wazazi,walikataa! Walimu wakuu na kamati walizifanyia mambo yao.
 
Hiyo ndiyo sababu iliyofanya huyo kiongozi amalizie hasira zake kupiga.

Kiukweli nilivokuja kufuatilia mambo kwisha kishikaji namna hiyo, nilikuja kugundua kumbe ofisi walizembea kutuma ripoti yake ya utoro ngazi za juu kwa wakati ndiyo maana wakaamua 'kila mtu apate'
 
Hasa wanawaonea primary wenye certificate, sekondari hawaendagi kufanya ujinga wao....
Na huku primary ukiwa na bachelor wanakuchukia kuanzia walimu wenzio hadi halmashauri.....wanapendaga mizezeta ya kutafutia kiki
 
Hasa wanawaonea primary wenye certificate, sekondari hawaendagi kufanya ujinga wao....
Na huku primary ukiwa na bachelor wanakuchukia kuanzia walimu wenzio hadi halmashauri.....wanapendaga mizezeta ya kutafutia kiki
Wana wanyanyasa wote tuu matukio ni menginwalimu hawana pakusema na haluna wa kuwatetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…