Waziri Mkenda, kiokoe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kusimamia kauli yako

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Nakuandikia Waziri wangu wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda,

Mnamo mwezi Disemba, 2022 wewe Mhe Waziri ulitoa kauli: Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili.

Mimi ni mstaafu chamani na Serikalini. Pamoja na kwamba nami pia nimehitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa shahada zangu mbili za sheria, watoto wangu wawili nao wamehitimu Chuoni humo: mmoja amehitimu sheria kama mimi na mmoja amehitimu uchumi. Wa mwisho wangu naye amejiunga pale kwa shahada ya masuala ya biashara.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo kikuu kikongwe na bora kuliko vingine kwa Tanzania na kwingineko. Kinastahili heshima kubwa na tunakipenda. Lakini, kwasasa kinaelekea kukwama. Kinaelekea kubaya. Kinaongeza programu mbalimbali za kimasomo lakini hakiajiri Wahadhiri wa kutosha. Kinapata vibali vya kuajiri lakini hakiajiri.

Sababu kubwa zaidi ya zote ni GPA ya 3.8 au zaidi kwa Shahada ya Kwanza. Kupata au kukosa GPA hiyo katika Shahada ya Kwanza humtoa au humwingiza mhusika kwenye kuweza kupata ajira ya Uhadhiri. Hata watanzania na wasio watanzania wenye Shahada za Umahiri na Uzamivu lakini wasio na 3.8 Shahada ya Kwanza hawaajiriki.

Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ilishatoa Muongozo juu ya sifa za Wahadhiri Vyuo Vikuu. Sifa inayoainishwa kwenye Muongozo wa TCU ni GPA ya kuanzia 3.5 kwa Shahada ya Awali/Kwanza. UDSM imekuwa ikiiacha mbali sifa hii kutoka TCU na kutaka 3.8 na zaidi. Zote, lakini, ni GPA za Daraja la Pili la Juu (Second Upper Division).

Kung'ang'ania 3.8 sasa kunaipa tabu UDSM. Inakosa Wahadhiri. Inaathirika kitaaluma kwakuwa Wahadhiri wachache waliopo wanaelemewa na majukumu mengi na makubwa na hivyo huduma za kitaaluma zinayumba. UDSM inashindwa kupata Wahadhiri kwa kwakuwa tu waombaji 'walitenda dhambi' ya kukosa 3.8 kwenye Shahada zao za awali.

Ifike wakati 3.8 isiwe kikwazo cha kuajiri na kusongesha mbele gurudumu la kitaaluma. UDSM ishauriwe na kuelekezwa kufuata Muongozo wa TCU huku ikichuja waombaji wake kwa umahiri wao katika kufundisha au kwenye usaili wa namna nyingine. Nayaongea haya kwakuwa kwasasa UDSM inakosa waombaji na matangazo ya ajira yanarudiwa: University of Dar es Salaam-. UDSM isaidiwe!

GPA kubwa si kigezo pekee cha uelewa na uwezo wa Mhadhiri kufundisha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
haiwezekani kushusha gpa ati ilimradi tupate wahadhili.lazima ubora wa elimu uzingatiwe.we need quality education in this country.haya mambo ya kulegeza masharti ndo yaliyoifikisha elimu yetu hapa tulipo.
 
Kama watakosekana Wahadhiri wenye sifa (3.8 GPA and above) basi wata Outsource, lengo ni kuendelea kumeet standards walizojiwekea.

Hii itumike Kama molare kwa Vijana wetu kupambana na kuzipata hizo GPA pindi wanapokuwa chuoni kusoma, sio muda wote kuwaza starehe, bettings n.k
 
Upper second na Upper second zinazotofautiana kwa 0.3 points zinaweza kuathiri elimu? Elimu inaathirika sana kwa sera na maamuzi mbali mbali na wala sio kwa GPA za wahadhiri.
Unakuta huyo mwenye 3.8 anakwenda kufundisha somo ambalo yeye ana B+ wakati kuna mwenye 3.5 lakini kwa somo hilo ana A.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Acha hizo aisee, kama watoto wako walishindwa kupata GPA ya 3.8 basi kazi ya uhadhiri UDSM sio kwa ajili yao.

Tumeharibu sana shule za msingi na sekondari kwa kuleta siasa za ajabu ajabu, tuesiendelee mpaka kwenye chuo bora cha taifa.

BTW, GPA sio kigezo pekee, ndio maana kuna usaili. Kwenye usaili mwenye GPA ya 4.0 anaweza kumshinda mwenye 4.4.
 
Kama watakosekana Wahadhiri wenye sifa (3.8 GPA and above) basi wata Outsource, lengo ni kuendelea kumeet standards walizojiwekea.

Hii itumike Kama molare kwa Vijana wetu kupambana na kuzipata hizo GPA pindi wanapokuwa chuoni kusoma, sio muda wote kuwaza starehe, bettings n.k
Sahihi pia Viwango vya TCU ni minimum sio kila chuo lazima kizingatie hayo ya TCU

Wao wanetoa mwongozo tu kuwa chuo chochote kisiajiri kiwango chini ya hapo

Shida ya GPA ikichukuliwa ya chini nyingine hata kusomea masters degree vyuo vingine vizuri hawaruhusu sasa akiajiriwa.mtu kama huyo ataishia u tutorial assistant sababu kwenda masters na PhD huko kugumu kwake
Aende akaombe serikalini

UDSM huhitaji vichwa na utakimbizwa mbio ukasome masters na uka perform huko.pia sababu utakimbizwa mbio ukasome PhD vinginevyo unatishiwa kupelekwa shule za sekondari kuwa hawataki kuendelea na wewe chuoni

Ku.maintain standard ni pamoja na kuwa na wahadhiri wenye standard za juu za ufaulu
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Acha hizo aisee, kama watoto wako walishindwa kupata GPA ya 3.8 basi kazi ya uhadhiri UDSM sio kwa ajili yao.

Tumeharibu sana shule za msingi na sekondari kwa kuleta siasa za ajabu ajabu, tuesiendelee mpaka kwenye chuo bora cha taifa.

BTW, GPA sio kigezo pekee, ndio maana kuna usaili. Kwenye usaili mwenye GPA ya 4.0 anaweza kumshinda mwenye 4.4.
Primary elimu waliharibu kwa kuchukua waliofeli form four wakasomee ualimu.wa msingi,sekondari nako wakaharibu waliopata pass za chini pia form four wakawapeleka kusomea diploma za ualimu waende wakafundishe sekondari ,sasa wamenogewa.kuua elimu sasa wanataka kuhamia vyuo vikuu kuwa waliopata GPA ya chini ndio wawe wahadhiri.Loo hata haya hawana

Hawajachoka bado tu kuua elimu?

UDSM shikilieni hapo hapo hakuna kushusha.standards za wahadhiri
 
Sahihi pia Viwango vya TCU ni minimum sio kila chuo lazima kizingatie hayo ya TCU

Wao wanetoa mwongozo tu kuwa chuo chochote kisiajiri kiwango chini ya hapo

Shida ya GPA ikichukuliwa ya chini nyingine hata kusomea masters degree vyuo vingine vizuri hawaruhusu sasa akiajiriwa
Ni kweli Mkuu, tusije kuzalisha Vilaza kwa kuendekeza Siasa kwenye Taaluma.
Ku.maintain standard ni pamoja na kuwa na wahadhiri wenye standard za juu za ufaulu
Standard lazima ifuatwe, kama mtoto ana wiwa kuwa Mkufunzi wa Chuo kikuu ni lazima asome kwa bidii na kufauru
 
Mimi nimehitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa shahada zangu mbili za sheria,
Duh, kumbe na wewe ni LL.B UDSM na LL.M UDSM!, ndio maana you are so good!.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo kikuu kikongwe na bora kuliko vingine kwa Tanzania na kwingineko. Kinastahili heshima kubwa na tunakipenda
Naunga mkono hoja
Lakini, kwasasa kinaelekea kukwama. Kinaelekea kubaya. Kinaongeza programu mbalimbali za kimasomo lakini hakiajiri Wahadhiri wa kutosha. Kinapata vibali vya kuajiri lakini hakiajiri.

Sababu kubwa zaidi ya zote ni GPA ya 3.8 au zaidi kwa Shahada ya Kwanza. Kupata au kukosa GPA hiyo katika Shahada ya Kwanza humtoa au humwingiza mhusika kwenye kuweza kupata ajira ya Uhadhiri. Hata watanzania na wasio watanzania wenye Shahada za Umahiri na Uzamivu lakini wasio na 3.8 Shahada ya Kwanza hawaajiriki.
Nasimama na msimamo wa UDSM wa wahadhiri lazima wapate GPA ya 3.8 and above, no retreat, no surrender!, hii ndio heshima ya UDSM!, unataka sasa na wao waanze ku recruit wahadhiri vilaza?.
Mimi nilipanga kujoiin UDSM kusoma LL.B direct from school. Nilipokosa 1st Class, I had to forget LL.B, ndipo nikaenda journalism.

Milango ya private candidates ilipofunguliwa UDSM FoL, nikajoin. Hivyo kwa Tanzania kusoma UDSM ni heshima, hivyo kamwe wasiruhusu vilaza wa less than GPA ya 3.8 kuajiriwa. Kwa vile sasa Tanzania tuna vyuo vikuu vingi, hao Watanzania wengine wenye uwezo mkubwa ila hawana GPA ya 3.8, wakawafundishe Watanzania wenzetu huko kwenye vyuo vingine, UDSM maintains GPA ya 3.8 and above ila iboreshe maslahi ili kuatract GPA above 3.8 kutoka dunia nzima!.
Kung'ang'ania 3.8 sasa kunaipa tabu UDSM. Inakosa Wahadhiri. Inaathirika kitaaluma kwakuwa Wahadhiri wachache waliopo wanaelemewa na majukumu mengi na makubwa na hivyo huduma za kitaaluma zinayumba. UDSM inashindwa kupata Wahadhiri kwa kwakuwa tu waombaji 'walitenda dhambi' ya kukosa 3.8 kwenye Shahada zao za awali.
Wawalipe vizuri sana hao wachache na kuongeza mishahara kuvutia GPA za 3.8
Ifike wakati 3.8 isiwe kikwazo cha kuajiri na kusongesha mbele gurudumu la kitaaluma. UDSM ishauriwe na kuelekezwa kufuata Muongozo wa TCU huku ikichuja waombaji wake kwa umahiri wao katika kufundisha au kwenye usaili wa namna nyingine. Nayaongea haya kwakuwa kwasasa UDSM inakosa waombaji na matangazo ya ajira yanarudiwa: University of Dar es Salaam-. UDSM isaidiwe!
I'd like to differ
GPA kubwa si kigezo pekee cha uelewa na uwezo wa Mhadhiri kufundisha!
Naunga mkono hoja, ila it's muhimu UDSM kumaintain it's superior standards!. Au unataka mwanao afundishwe na vilaza?.

Hiyo superior standards ndio zinatufanya tuwe very proud of waalimu wetu kama hapa Hongera Spika Dkt. Tulia Ackson. You've Become So Good! B'Cause you're Smart, Bright & Brilliant! Kuna haja MaSpika wetu iwe lazima kuwa Wanasheria?

P
 
Kama watakosekana Wahadhiri wenye sifa (3.8 GPA and above) basi wata Outsource, lengo ni kuendelea kumeet standards walizojiwekea.

Hii itumike Kama molare kwa Vijana wetu kupambana na kuzipata hizo GPA pindi wanapokuwa chuoni kusoma, sio muda wote kuwaza starehe, bettings n.k
Uko sahihi.Zamani wakati ajira hazikuwa za kupiga ramli ilikuwa wanapomaliza wale wanaohitajika kubaki kama tutorial assistant waliajiriwa.Shahada ya pili waliipata wakiwa kazini.Sasa hivi ni ngumu kuwapata kwa kuwa wahitimu wenye sifa hizo wanakuwa wamemezwa na soko huria.
 
Back
Top Bottom