Waziri Mkenda, kiokoe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kusimamia kauli yako

Waziri Mkenda, kiokoe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kusimamia kauli yako

Nadhani wameteremsha. Zamani ilikuwa GPA 4 ndio unaajiriwa. Tatizo sio kwamba wa GPA ya 3.8 hawapo. Wapo ila wanachukuliwa na taasisi binafsi zenye kutoa maslahi zaidi.
taasisi binafsi zipi? acha uongo
 
Kama unakubali GPA sio kigezo huku ukibeza kwenye ubeti wa kwanza nashindwa kukuelewa.

Shida ni kukwepa gharama za usaili katika kutafuta watu bora.
Wangeweza kuweka dirisha wazi kisha waanzishe mchakato wa kutafuta watu wenye uwezo.

Hii itasaidia kupata watu wenye uweza wa kutoa nondo na kuwaelekeza wanafunzi. Mbona huko shule za msingi na sekondari tumefundishwa na walimu walionekana kama wamefeli lkn bado wametengeneza watu wa maana.

Mie naamini wakubali gharama, waandae taratibu za usaili, iwe wa darasani na mahojiano watajuta kuwa hizi GPA zao sio vigezo tu.

Kuna watu wanauelewa mpana wa mambo na kujua kuyawasilisha.
GPA hoyeee…. Aione Kabudi.
"Sio kigezo pekee", soma vizuri uelewe. Ndio maana mnapata GPA ndogo.
 
Mfumo wa elimu nchi hii pasua kichwa sana
Upper second na Upper second zinazotofautiana kwa 0.3 points zinaweza kuathiri elimu? Elimu inaathirika sana kwa sera na maamuzi mbali mbali na wala sio kwa GPA za wahadhiri.
Unakuta huyo mwenye 3.8 anakwenda kufundisha somo ambalo yeye ana B+ wakati kuna mwenye 3.5 lakini kwa somo hilo ana A.
 
Nimekumbuka mbali sana kwa hii kauli [emoji38][emoji119]

Me nadhani kufundisha ni kipaji

Kuna Profesa mmoja alikuwa anatufundisha Structural Analysis I, kitu hakiendi wala nini.

Tukaja kufundishwa Structure analysis II na Eng. Mmoja yeye alikuwa ana Masters tu yaani unaona Jinsi Engineering inavyokuwa rahisi. Jamaa anaeleweka hadi basi.

Unapewa zako hata jengo la ghorofa 30+ unalishusha kama kumsukuma mlevi tu
hivi mkipewa haya majengo mjenge mnaweza?au ndiyo yanayoporomoka kwa kuwa mnafanya kny karatasi tu
 
Kama unakubali GPA sio kigezo huku ukibeza kwenye ubeti wa kwanza nashindwa kukuelewa.

Shida ni kukwepa gharama za usaili katika kutafuta watu bora.
Wangeweza kuweka dirisha wazi kisha waanzishe mchakato wa kutafuta watu wenye uwezo.

Hii itasaidia kupata watu wenye uweza wa kutoa nondo na kuwaelekeza wanafunzi. Mbona huko shule za msingi na sekondari tumefundishwa na walimu walionekana kama wamefeli lkn bado wametengeneza watu wa maana.

Mie naamini wakubali gharama, waandae taratibu za usaili, iwe wa darasani na mahojiano watajuta kuwa hizi GPA zao sio vigezo tu.

Kuna watu wanauelewa mpana wa mambo na kujua kuyawasilisha.
GPA hoyeee…. Aione Kabudi.
Elimu yetu imevurugwa sana hasa kuanzia Primary na Secondary,ili elimu yetu iwe bora jitiada zingewekwa kwa Wanafunzi waliopata GPA ya 3.5 wapelekwe kufundisha Primary na Secondary schools,then kule ndiyo watakuwa wanachujwa na kupelekwa vyuoni kufundisha.
Kwa mtindo huu tutapata Wanafunzi competent na wakufunzi competent,lakini hawa wanafunzi wa sikuizi wanakalili vitini na vitabu hawasomi,watatupeleka wapi.
Sorry,kwa kutoka nje ya mada!
 
Mkuu hizi GPA nyingi za vyuo gani? Unadhani pia zinauwezo kudeliver mavitu.
Kuna vyuo huko GPA zinagawiwa tu, je uwezo upo wa kuitetea hiyo GPA yako kabla ya kudai maslahi makubwa?
GPA za rushwa ya ngono na pesa zipo vyuo vyote ikiwemo UDSM.Ila UDSM inakuwa overrated sana.Elimu yetu imeporomoka sana!
 
haiwezekani kushusha gpa ati ilimradi tupate wahadhili.lazima ubora wa elimu uzingatiwe.we need quality education in this country.haya mambo ya kulegeza masharti ndo yaliyoifikisha elimu yetu hapa tulipo.
Huku mtaani mambo yanaongozwa na waliopata GPS ya 2.3. Ndo wahandisi, wanasheria, madaktari, waalimu, wakuu wa idara, wakuu wa Taasisi. Hao nao wamefundishwa na haohao waliopata GPS ya 3.8. Quality education iko wapi hapo?
 
Kama watakosekana Wahadhiri wenye sifa (3.8 GPA and above) basi wata Outsource, lengo ni kuendelea kumeet standards walizojiwekea.

Hii itumike Kama molare kwa Vijana wetu kupambana na kuzipata hizo GPA pindi wanapokuwa chuoni kusoma, sio muda wote kuwaza starehe, bettings n.k
Ni hizi GPA za vyupi au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haiwezekani kushusha gpa ati ilimradi tupate wahadhili.lazima ubora wa elimu uzingatiwe.we need quality education in this country.haya mambo ya kulegeza masharti ndo yaliyoifikisha elimu yetu hapa tulipo.
Kaka GPA sio ubora wa mwalimu, kama wewe umesoma kingereza A Level kuanzia miaka ya 98 kuja juu nadhani ushamsikia Ustaadh Shabani Omar almaarufu USTADH, huyu jamaa ni noma kwenye kifundisha lakini pale UDSM haajiriki Ila ukiwauliza wanafunzi watakwambia balaa lake
 
Sahihi kabisa mkuu, ni lazima asome kwa bidii na kufaulu.

Lakini ni lazima tuwapime uelewa wao kwa mapana zaidi kuliko kuzingatia marks tu za darasani.

Walau amefaulu tu, apewe nafasi katika usaili, tuna mifano mingi jamaa wanaelewa mambo nakujua kuywasilisha vizuri. Njoo kwenye GPA sasa, mliokuwa mnalishwa nondo mnapunga upepo [emoji28]. Nipe darasa sasa uone, naaona kila mtu anaweza tu.

Hizi GPA ndo zinawafanya hawa jamaa wanakula bata tu akija class anapiga blah blah imeisha hiyo, kazi kwenu mkasomeshane wenyewe.
Wenye GPA kubwa ni ngumu ku deliver. Hawatoboi yani wengi wao ni wakaririji. Anakuwa na vitu kichwani ila kudigest watu waelewe hawezi anawatupia notes tu za vitini mkapambane.
Tumefundishwa na PhD holders wa aina hio
 
Nakuandikia Waziri wangu wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda,

Mnamo mwezi Disemba, 2022 wewe Mhe Waziri ulitoa kauli: Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili.

Mimi ni mstaafu chamani na Serikalini. Pamoja na kwamba nami pia nimehitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa shahada zangu mbili za sheria, watoto wangu wawili nao wamehitimu Chuoni humo: mmoja amehitimu sheria kama mimi na mmoja amehitimu uchumi. Wa mwisho wangu naye amejiunga pale kwa shahada ya masuala ya biashara.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo kikuu kikongwe na bora kuliko vingine kwa Tanzania na kwingineko. Kinastahili heshima kubwa na tunakipenda. Lakini, kwasasa kinaelekea kukwama. Kinaelekea kubaya. Kinaongeza programu mbalimbali za kimasomo lakini hakiajiri Wahadhiri wa kutosha. Kinapata vibali vya kuajiri lakini hakiajiri.

Sababu kubwa zaidi ya zote ni GPA ya 3.8 au zaidi kwa Shahada ya Kwanza. Kupata au kukosa GPA hiyo katika Shahada ya Kwanza humtoa au humwingiza mhusika kwenye kuweza kupata ajira ya Uhadhiri. Hata watanzania na wasio watanzania wenye Shahada za Umahiri na Uzamivu lakini wasio na 3.8 Shahada ya Kwanza hawaajiriki.

Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ilishatoa Muongozo juu ya sifa za Wahadhiri Vyuo Vikuu. Sifa inayoainishwa kwenye Muongozo wa TCU ni GPA ya kuanzia 3.5 kwa Shahada ya Awali/Kwanza. UDSM imekuwa ikiiacha mbali sifa hii kutoka TCU na kutaka 3.8 na zaidi. Zote, lakini, ni GPA za Daraja la Pili la Juu (Second Upper Division).

Kung'ang'ania 3.8 sasa kunaipa tabu UDSM. Inakosa Wahadhiri. Inaathirika kitaaluma kwakuwa Wahadhiri wachache waliopo wanaelemewa na majukumu mengi na makubwa na hivyo huduma za kitaaluma zinayumba. UDSM inashindwa kupata Wahadhiri kwa kwakuwa tu waombaji 'walitenda dhambi' ya kukosa 3.8 kwenye Shahada zao za awali.

Ifike wakati 3.8 isiwe kikwazo cha kuajiri na kusongesha mbele gurudumu la kitaaluma. UDSM ishauriwe na kuelekezwa kufuata Muongozo wa TCU huku ikichuja waombaji wake kwa umahiri wao katika kufundisha au kwenye usaili wa namna nyingine. Nayaongea haya kwakuwa kwasasa UDSM inakosa waombaji na matangazo ya ajira yanarudiwa: University of Dar es Salaam-. UDSM isaidiwe!

GPA kubwa si kigezo pekee cha uelewa na uwezo wa Mhadhiri kufundisha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Wanasahau tuliweza kuingia chuoni hapo na principle pass E kwa masomo mawili leo ni majaji wakubwa na wenye akili sana
Kuna wakati unaingia chuoni na principal moja tu
Ukiritimba huu utakiangusha chuo. Vyuo ni vingi vizuri kama UDSM,mfano Kairuki is among the best in Tz,Mzumbe nk nk
 
Wanatakiwa kupambana,hizo huruma ndio zinzokwamisha hili taifa
 
Una hoja mzee wetu japo kuna mambo pia ni muhimu kuyatazama;

Kwenye kila career, huwa kuna kipimo cha ubora. Mfano kwa sisi watu wa mpira ili tukubali kuwa striker ni hatari, lazima awe anafunga magoli mengi, kiungo mshambuliaji awe ametengeneza nafasi nyingi za magoli na beki awe hapitiki n.k.

Sasa unachotakiwa kujua pia ni kuwa kwenye mpira kuna levels za mafanikio upande wa employers, yaani Clubs. Kuna club kubwa (zenye mafanikio makubwa kuanzia makombe hadi fanbase) na club za kawaida au ndogo. Sasa ili Club kubwa kama Real Madrid ikusajili, basi lazima uwe exceptional katika career yako yani numbers zako ziwe zimenyooka na sio za mchongo! Japo sometimes kuna makosa huwa wanafanya kwenye kusajili lakini ni mara chache mno.

Hivyo standards alizojiwekea Madrid (au Club zingine kubwa), ndio zinafanya hadi wanamichezo wengi (kuanzia makocha hadi wachezaji) kuamini kuwa ni ndoto kubwa ya maisha yao kufanikiwa kuzitumikia hizo Clubs.

Sasa nirudi kwenye mfumo wetu wa Elimu.

Kipimo chetu cha ubora wa mwanafunzi kinajulikana. Kwa upande wa secondary ni Division 1&2, na kwa upande wa chuo ni First Class & Upper Second G.P.A.

Lakini wote tunajua ni ngumu sana kupata nafasi ya kusoma A'Level pale Feza au St Francis au Ilboru na the likes kama huna Flat A's au AAB kwenye combination yako. Hizo ni Standards zao wamejiwekea kutokana na ubora wao na malengo yao ya muda mrefu.

Sasa turudi kwenye hoja;

Ukizungumzia UDSM, unazungumzia chuo kikuu namba 1 (top) kati ya vyuo vyote hapa nchini. UDSM kuna kazi nyingi kama taasisi kubwa lakini kazi kuu inayoitambulisha ni kutoa elimu ya juu (Lectures). It means hiyo ndiyo sehemu ambayo lazima core values zao zizingatiwe kikamilifu. Kwahiyo ni muhimu sana kwao waka set high standards kwa watu wanaotaka kufundisha pale (kama ilivyo kwenye timu kubwa za mpira ambazo hazichukui wachezaji wenye uwezo na takwimu za kawaida).

So it's either you shoot and hit their target, or you miss. Candidates ndio wanatakiwa wapambane wafikie hizo standards na kamwe sishauri standards zishushwe ili ziwafikie incompetent candidates. Never do that!
 
Una hoja mzee wetu japo kuna mambo pia ni muhimu kuyatazama;

Kwenye kila career, huwa kuna kipimo cha ubora. Mfano kwa sisi watu wa mpira ili tukubali kuwa striker ni hatari, lazima awe anafunga magoli mengi, kiungo mshambuliaji awe ametengeneza nafasi nyingi za magoli na beki awe hapitiki n.k.

Sasa unachotakiwa kujua pia ni kuwa kwenye mpira kuna levels za mafanikio upande wa employers, yaani Clubs. Kuna club kubwa (zenye mafanikio makubwa kuanzia makombe hadi fanbase) na club za kawaida au ndogo. Sasa ili Club kubwa kama Real Madrid ikusajili, basi lazima uwe exceptional katika career yako yani numbers zako ziwe zimenyooka na sio za mchongo! Japo sometimes kuna makosa huwa wanafanya kwenye kusajili lakini ni mara chache mno.

Hivyo standards alizojiwekea Madrid (au Club zingine kubwa), ndio zinafanya hadi wanamichezo wengi (kuanzia makocha hadi wachezaji) kuamini kuwa ni ndoto kubwa ya maisha yao kufanikiwa kuzitumikia hizo Clubs.

Sasa nirudi kwenye mfumo wetu wa Elimu.

Kipimo chetu cha ubora wa mwanafunzi kinajulikana. Kwa upande wa secondary ni Division 1, na kwa upande wa chuo ni upper second G.P.A.

Lakini wote tunajua ni ngumu sana kupata nafasi ya kusoma A'Level pale Feza au St Francis au Ilboru na the likes kama huna Flat A's au AAB kwenye combination yako. Hizo ni Standards zao wamejiwekea kutokana na ubora wao na malengo yao ya muda mrefu.

Sasa turudi kwenye hoja;

Ukizungumzia UDSM, unazungumzia chuo kikuu namba 1 (top) kati ya vyuo vyote hapa nchini. UDSM kuna kazi nyingi kama taasisi kubwa lakini kazi kuu inayoitambulisha ni kutoa elimu ya juu (Lectures). It means hiyo ndiyo sehemu ambayo lazima core values zao zizingatiwe kikamilifu. Kwahiyo ni muhimu sana kwao waka set high standards kwa watu wanaotaka kufundisha pale (kama ilivyo kwenye timu kubwa za mpira ambazo hazichukui wachezaji wenye uwezo na takwimu za kawaida).

So it's either you shoot and hit their target, or you miss. Candidates ndio wanatakiwa wapambane wafikie hizo standards na kamwe sishauri standards zishushwe ili ziwafikie incompetent candidates. Never do that!
You have said it all!
 
Back
Top Bottom