Anaetetea hayo kasema alikuwa chamani, bado ana hangover ya Lumumba.haiwezekani kushusha gpa ati ilimradi tupate wahadhili.lazima ubora wa elimu uzingatiwe.we need quality education in this country.haya mambo ya kulegeza masharti ndo yaliyoifikisha elimu yetu hapa tulipo.
GPA ya 3.8 haijawahi kuwa tatizo UDSM. Nimesoma pale.Nakuandikia Waziri wangu wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda,
Mnamo mwezi Disemba, 2022 wewe Mhe Waziri ulitoa kauli: Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili.
Mimi ni mstaafu chamani na Serikalini. Pamoja na kwamba nami pia nimehitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa shahada zangu mbili za sheria, watoto wangu wawili nao wamehitimu Chuoni humo: mmoja amehitimu sheria kama mimi na mmoja amehitimu uchumi. Wa mwisho wangu naye amejiunga pale kwa shahada ya masuala ya biashara.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo kikuu kikongwe na bora kuliko vingine kwa Tanzania na kwingineko. Kinastahili heshima kubwa na tunakipenda. Lakini, kwasasa kinaelekea kukwama. Kinaelekea kubaya. Kinaongeza programu mbalimbali za kimasomo lakini hakiajiri Wahadhiri wa kutosha. Kinapata vibali vya kuajiri lakini hakiajiri.
Sababu kubwa zaidi ya zote ni GPA ya 3.8 au zaidi kwa Shahada ya Kwanza. Kupata au kukosa GPA hiyo katika Shahada ya Kwanza humtoa au humwingiza mhusika kwenye kuweza kupata ajira ya Uhadhiri. Hata watanzania na wasio watanzania wenye Shahada za Umahiri na Uzamivu lakini wasio na 3.8 Shahada ya Kwanza hawaajiriki.
Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ilishatoa Muongozo juu ya sifa za Wahadhiri Vyuo Vikuu. Sifa inayoainishwa kwenye Muongozo wa TCU ni GPA ya kuanzia 3.5 kwa Shahada ya Awali/Kwanza. UDSM imekuwa ikiiacha mbali sifa hii kutoka TCU na kutaka 3.8 na zaidi. Zote, lakini, ni GPA za Daraja la Pili la Juu (Second Upper Division).
Kung'ang'ania 3.8 sasa kunaipa tabu UDSM. Inakosa Wahadhiri. Inaathirika kitaaluma kwakuwa Wahadhiri wachache waliopo wanaelemewa na majukumu mengi na makubwa na hivyo huduma za kitaaluma zinayumba. UDSM inashindwa kupata Wahadhiri kwa kwakuwa tu waombaji 'walitenda dhambi' ya kukosa 3.8 kwenye Shahada zao za awali.
Ifike wakati 3.8 isiwe kikwazo cha kuajiri na kusongesha mbele gurudumu la kitaaluma. UDSM ishauriwe na kuelekezwa kufuata Muongozo wa TCU huku ikichuja waombaji wake kwa umahiri wao katika kufundisha au kwenye usaili wa namna nyingine. Nayaongea haya kwakuwa kwasasa UDSM inakosa waombaji na matangazo ya ajira yanarudiwa: University of Dar es Salaam-. UDSM isaidiwe!
GPA kubwa si kigezo pekee cha uelewa na uwezo wa Mhadhiri kufundisha!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Sahihi mkuu, Watu wanaangalia maslahi tu. Kama hilo ombwe limeshaonekana ni vizuri kuboresha maslahi yao ili kuwavutia wengiUko sahihi.Zamani wakati ajira hazikuwa za kupiga ramli ilikuwa wanapomaliza wale wanaohitajika kubaki kama tutorial assistant waliajiriwa.Shahada ya pili waliipata wakiwa kazini.Sasa hivi ni ngumu kuwapata kwa kuwa wahitimu wenye sifa hizo wanakuwa wamemezwa na soko huria.
Wakati utawaacha sana vyuo vikuu na GPA zao kubwa. Sisi wengine tuna hizo GPA kubwa lakini lazima ukweli usemwe. Wanaachwa na wakati. Kufundisha vyuo vikuu is no longer an attractive employment. Sekta zingine zimekuja juu. Zina maslahi mazuri zaidi na hazihitaji GPA kubwa zaidi. Halafu ni rahisi kufanya na hazina mzigo mkubwa kama kufundisha vyuo vikuu.🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Acha hizo aisee, kama watoto wako walishindwa kupata GPA ya 3.8 basi kazi ya uhadhiri UDSM sio kwa ajili yao.
Tumeharibu sana shule za msingi na sekondari kwa kuleta siasa za ajabu ajabu, tuesiendelee mpaka kwenye chuo bora cha taifa.
BTW, GPA sio kigezo pekee, ndio maana kuna usaili. Kwenye usaili mwenye GPA ya 4.0 anaweza kumshinda mwenye 4.4.
We ndugu umenifurahisha sana kwa kushukuru huku.Shukrani kunisahihisha Mkuu 🙏
Wanasema uungwana ni vitendo, nimeonesha uungwana kwa kushukuru kusahihishwa Mkuu 🙏We ndugu umenifurahisha sana kwa kushukuru huku.
Kongole sana.
Yule chatu mmeza watu hajafa bado na yupo kigamboni anasubiria mlo ujue!Kama ile Pihejidi ya maganda ya korosho?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Acha hizo aisee, kama watoto wako walishindwa kupata GPA ya 3.8 basi kazi ya uhadhiri UDSM sio kwa ajili yao.
Tumeharibu sana shule za msingi na sekondari kwa kuleta siasa za ajabu ajabu, tuesiendelee mpaka kwenye chuo bora cha taifa.
BTW, GPA sio kigezo pekee, ndio maana kuna usaili. Kwenye usaili mwenye GPA ya 4.0 anaweza kumshinda mwenye 4.4.
Ni kweli Mkuu, tusije kuzalisha Vilaza kwa kuendekeza Siasa kwenye Taaluma.
Standard lazima ifuatwe, kama mtoto ana wiwa kuwa Mkufunzi wa Chuo kikuu ni lazima asome kwa bidii na kufauru
Wenye GPA ya 3.8 wapo wengi sana tena sana ulizia competition ya waliooata hiyo GPA sema cha muhimu waongeze maslahi haiwezekani mwenye 3.8 alipwe take home chini ya milioni mbili na ukasema utapata watu
Swali zuri..Mkuu hizi GPA nyingi za vyuo gani? Unadhani pia zinauwezo kudeliver mavitu.
Kuna vyuo huko GPA zinagawiwa tu, je uwezo upo wa kuitetea hiyo GPA yako kabla ya kudai maslahi makubwa?
Nimekumbuka mbali sana kwa hii kauli 😆🙌Hizi GPA ndo zinawafanya hawa jamaa wanakula bata tu akija class anapiga blah blah imeisha hiyo, kazi kwenu mkasomeshane wenyewe.
Mkuu hizi GPA nyingi za vyuo gani? Unadhani pia zinauwezo kudeliver mavitu.
Kuna vyuo huko GPA zinagawiwa tu, je uwezo upo wa kuitetea hiyo GPA yako kabla ya kudai maslahi makubwa?
Swali zuri..