Waziri Mkenda, kiokoe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kusimamia kauli yako

Nadhani wameteremsha. Zamani ilikuwa GPA 4 ndio unaajiriwa. Tatizo sio kwamba wa GPA ya 3.8 hawapo. Wapo ila wanachukuliwa na taasisi binafsi zenye kutoa maslahi zaidi.
taasisi binafsi zipi? acha uongo
 
"Sio kigezo pekee", soma vizuri uelewe. Ndio maana mnapata GPA ndogo.
 
Mfumo wa elimu nchi hii pasua kichwa sana
 
hivi mkipewa haya majengo mjenge mnaweza?au ndiyo yanayoporomoka kwa kuwa mnafanya kny karatasi tu
 
Elimu yetu imevurugwa sana hasa kuanzia Primary na Secondary,ili elimu yetu iwe bora jitiada zingewekwa kwa Wanafunzi waliopata GPA ya 3.5 wapelekwe kufundisha Primary na Secondary schools,then kule ndiyo watakuwa wanachujwa na kupelekwa vyuoni kufundisha.
Kwa mtindo huu tutapata Wanafunzi competent na wakufunzi competent,lakini hawa wanafunzi wa sikuizi wanakalili vitini na vitabu hawasomi,watatupeleka wapi.
Sorry,kwa kutoka nje ya mada!
 
Mkuu hizi GPA nyingi za vyuo gani? Unadhani pia zinauwezo kudeliver mavitu.
Kuna vyuo huko GPA zinagawiwa tu, je uwezo upo wa kuitetea hiyo GPA yako kabla ya kudai maslahi makubwa?
GPA za rushwa ya ngono na pesa zipo vyuo vyote ikiwemo UDSM.Ila UDSM inakuwa overrated sana.Elimu yetu imeporomoka sana!
 
haiwezekani kushusha gpa ati ilimradi tupate wahadhili.lazima ubora wa elimu uzingatiwe.we need quality education in this country.haya mambo ya kulegeza masharti ndo yaliyoifikisha elimu yetu hapa tulipo.
Huku mtaani mambo yanaongozwa na waliopata GPS ya 2.3. Ndo wahandisi, wanasheria, madaktari, waalimu, wakuu wa idara, wakuu wa Taasisi. Hao nao wamefundishwa na haohao waliopata GPS ya 3.8. Quality education iko wapi hapo?
 
Ni hizi GPA za vyupi au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haiwezekani kushusha gpa ati ilimradi tupate wahadhili.lazima ubora wa elimu uzingatiwe.we need quality education in this country.haya mambo ya kulegeza masharti ndo yaliyoifikisha elimu yetu hapa tulipo.
Kaka GPA sio ubora wa mwalimu, kama wewe umesoma kingereza A Level kuanzia miaka ya 98 kuja juu nadhani ushamsikia Ustaadh Shabani Omar almaarufu USTADH, huyu jamaa ni noma kwenye kifundisha lakini pale UDSM haajiriki Ila ukiwauliza wanafunzi watakwambia balaa lake
 
Wenye GPA kubwa ni ngumu ku deliver. Hawatoboi yani wengi wao ni wakaririji. Anakuwa na vitu kichwani ila kudigest watu waelewe hawezi anawatupia notes tu za vitini mkapambane.
Tumefundishwa na PhD holders wa aina hio
 
Wanasahau tuliweza kuingia chuoni hapo na principle pass E kwa masomo mawili leo ni majaji wakubwa na wenye akili sana
Kuna wakati unaingia chuoni na principal moja tu
Ukiritimba huu utakiangusha chuo. Vyuo ni vingi vizuri kama UDSM,mfano Kairuki is among the best in Tz,Mzumbe nk nk
 
Wanatakiwa kupambana,hizo huruma ndio zinzokwamisha hili taifa
 
Una hoja mzee wetu japo kuna mambo pia ni muhimu kuyatazama;

Kwenye kila career, huwa kuna kipimo cha ubora. Mfano kwa sisi watu wa mpira ili tukubali kuwa striker ni hatari, lazima awe anafunga magoli mengi, kiungo mshambuliaji awe ametengeneza nafasi nyingi za magoli na beki awe hapitiki n.k.

Sasa unachotakiwa kujua pia ni kuwa kwenye mpira kuna levels za mafanikio upande wa employers, yaani Clubs. Kuna club kubwa (zenye mafanikio makubwa kuanzia makombe hadi fanbase) na club za kawaida au ndogo. Sasa ili Club kubwa kama Real Madrid ikusajili, basi lazima uwe exceptional katika career yako yani numbers zako ziwe zimenyooka na sio za mchongo! Japo sometimes kuna makosa huwa wanafanya kwenye kusajili lakini ni mara chache mno.

Hivyo standards alizojiwekea Madrid (au Club zingine kubwa), ndio zinafanya hadi wanamichezo wengi (kuanzia makocha hadi wachezaji) kuamini kuwa ni ndoto kubwa ya maisha yao kufanikiwa kuzitumikia hizo Clubs.

Sasa nirudi kwenye mfumo wetu wa Elimu.

Kipimo chetu cha ubora wa mwanafunzi kinajulikana. Kwa upande wa secondary ni Division 1&2, na kwa upande wa chuo ni First Class & Upper Second G.P.A.

Lakini wote tunajua ni ngumu sana kupata nafasi ya kusoma A'Level pale Feza au St Francis au Ilboru na the likes kama huna Flat A's au AAB kwenye combination yako. Hizo ni Standards zao wamejiwekea kutokana na ubora wao na malengo yao ya muda mrefu.

Sasa turudi kwenye hoja;

Ukizungumzia UDSM, unazungumzia chuo kikuu namba 1 (top) kati ya vyuo vyote hapa nchini. UDSM kuna kazi nyingi kama taasisi kubwa lakini kazi kuu inayoitambulisha ni kutoa elimu ya juu (Lectures). It means hiyo ndiyo sehemu ambayo lazima core values zao zizingatiwe kikamilifu. Kwahiyo ni muhimu sana kwao waka set high standards kwa watu wanaotaka kufundisha pale (kama ilivyo kwenye timu kubwa za mpira ambazo hazichukui wachezaji wenye uwezo na takwimu za kawaida).

So it's either you shoot and hit their target, or you miss. Candidates ndio wanatakiwa wapambane wafikie hizo standards na kamwe sishauri standards zishushwe ili ziwafikie incompetent candidates. Never do that!
 
You have said it all!
 
Watu wa vimemo mmebanwa mbavu sasa mnakimbilia jf πŸ˜‚οΈπŸ˜‚οΈπŸ˜‚οΈπŸ˜‚οΈπŸ˜‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…