Waziri Mkenda, kiokoe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kusimamia kauli yako

-3.8 sio Kwa udsm tu, ni Kwa Vyuo vikuu vyote, except Institutes kama ifm,iaa,tia,nit nk
  • Kwa Sasa udsm is no longer chuo chenye wasomi Waziri kwenye sheria,Wenye uwezo mkubwa hiyo ilikuwa zamani enzi za kina Lissu, Shivji,Migiro,Ringo tenga, majamba, Kwa Sasa Udsm wako vizuri sana kule CoET ndiyo kweli Kuna Vichwa wale wa asili.
  • salary scale ya udsm na other universities ni ndogo sana imagine tutorial assistant analipwa 1.6m, wakati Kuna Mashirika ya Umma LLB analipwa 2.6m so sad
-
 
Unawatetea vilaza wenzako. UDSM in hadhi yake inayohitaji kulindwa.
 
Utaratibu wa G..P.A ya 3.8 ni mzuri, mimi nadhani kuondoa watu wanao fluke waanzie kuanzia secondary, yaani mtu asiwe chini ya division two, na hizo G.P.A
Ukiangalia matokeo ya sekondari sidhani kama kuna walimu watakatiza hapo.
Zamani mtu akifaulu F4 alikuwa anaenda F5, akifaulu tena anaenda UDSM.
Sasa, kuna walimu mpaka Maprofesa walianza kwa kwenda vyuo vya ualimu. Walipojiendeleza ufaulu wa ndio unaanza kuonekana.
Mtu kama Mwakyembe alianza kwenda Chuo cha Uandishi wa habari. Ina maana hakufaulu kwenda F4. Aliojiendelea na kujiunga na UDSM nyota ikang'aa kwa ufaulu.
Kwa hiyo kufaulu vyuoni sio kufluke. Mazingira na Ubora wa ufundishaji unachangia.
 
GPA kubwa ni muhimu, kwa mazingira ya Tanzania tukiondoa kujuana mwenye GPA kubwa ndiye mweye uwezo mkubwa. Tuache maneno tunapaswa kuanza kuwatumia wenye GPA kubwa kama kuna eneo haelewi tumfanyie training na kumwendeleza ili tumjengee uwezo tunaouhitaji. Tusijifariji kwamba mwenye GPA ndogo anaweza kumzidi mwenye GPA kubwa. Mimi binafsi kwenye taasisi yangu na nature ya kazi zangu naajiri wenye GPA kubwa pekee.

Kuna bwana mmoja alikua anaitwa Elias Kihombo huyu bwana alikua na uwezo mkubwa sana na alikua na matokeo makubwa mno form six na chuo kikuu. Lakini serikali yetu ilishindwa kumtumia pamoja na uwezo wake kwa kuwa na mawazo kama haya ya mtoa mada.

Na tukienda kwa mtindo kama huu tukafanikiwa kujaza wenye GPA ndogo makazini basi wale wote wenye GPA kubwa wataanza kubaguliwa na kujifanya kwamba wanauelewa mkubwa kuliko wenye GPA kubwa. Na ukutane na ofisi nzima imesoma kwa njia za kungaunga na kupata uzoefu kazini basi hujidai wao ndio wenye uwezo zaidi na hizo kazi. Embu jaribu kumchukua huyo mwenye GPA kubwa mfanyie training kwenye hiyo kazi alafu mwaangalie.

Kwa elimu yetu asilimia kubwa ya wanaopata GPA ndogo ni wavivu wa kusoma, na wapenda starehe. Na ukishakuwa mhadhili kazi yako sii kuufunisha pekee, inatakiwa ufanye tafiti, uchapishe mapisho na uendelee kusoma hadi huko PhD. Na ili ufikie huko PhD lazima ufaulu vizuri. Sasa kama kufaulu kwako ni kwa kiwango kidogo tangu shule ya msingi kufikia hiyo PhD utachukua muda mrefu sana.
 
GPA haikutakiwa kutumika kabisa.
 
Ndio maana kampuni yako sio Google. Wenzako walishaachana na GPAs au Interview.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…