Nimefuatilia maamuzi ya waziri Mkenda kwa wakuu wa shule na walimu waliohusika kwenye kucheza wimbo wa zuchu Binafsi naona maamuzi ya Waziri Mkenda ni ya kukurupuka na hofu ya kutenguliwa nyadhifa yake. :
1. Maadili ya mtoto yaanzia nyumbani, Hawa watoto huu wimbo wamjifunza makwao kupitia redio na TV. Ukitizama Luninga DSTV wanaand kitu kinaitwa PG ,(Parental Guidance) utaona PG12,PG13,PG14 wakimaanisha mza kama mwanao sio miaka 12,13 au 14 asiangalie kwa sababu maudhui yake sio salama kwa maadili na ukuaji. Mwenye wajibu wa kuzia watoto wasiujue wimbo wa ZUCHU ni
@tcra_tanzania kwa ushirikiano wa muongozo wa maadili ya watoto toka wizara ya Mh. Gwajima na wao wizara ya elimu.
(2) Wizara ya Elimu inaruhusu michezo na muziki ni sehemu ya michezo, hususani kwenye tafrija za shule (Graduation) Kungelikuwepo PG ya TCRA na wizara DJ wa siku hiyo asingelipiga wimbo wa zuchu. Mtaala wa michezo unautambua muziki kama sehemu ya nyezo ya ufundishaji na kuandaa vipaji.
(3) Wazazi wa hawa watoto wanawajibika moja moja kwa athari chanya kwa makusudi wameacha rimoti za TV na watoto wao wakajifunza wimbo wa zuchu kwa sababu ule mwitikio kufuatisha mashairi nimkubwa sana ina maanisha watoto wote wanajua kuimba beti kwa beti ingawaje hata neno mpenzi wangu hawajuui maana yake , je nani atawaadhibu wazazi hawa kwa mmomonyoko wa maadili ulioleta athari chanya kwa watoto wao?
(4)Nani atawatetea walimu walioamua kufurahi na watoto wakaonekana wao sio peke yao wenye makosa juu ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto hawa?? walimu ni sawa na third part kwenye mkataba hawana madhara ya moja kwa moja wanakuwa subjective kwa impact ya maoni ya mitandao. Tutafukuza walimu wangapi? Je, Graduation ngapi watoto wetu wancheza mbele ya wazazi na wazazi tunafurahi? Je , sherehe ngapi sisi watu wazima tumedhuruia halafu watoto wetu wanatoa show kushindana kucheza.
(5) Waziri wa Elimu katumia vibaya madarka yake kuwashusha vyeo walimu kwa makosa yasisowahusu moja kwa moja, natamani nione na afisa maendeleo ya Jamii wa mkoa husika na kata husika akiwajibishwa kwa madhara ya ukosefu wa maadili kwa ni kweli?
(6) Hivi leo hii seneti ya chuo kikuu Dar es salaam imvue hadhi uprofesa kwa sababu somo alilofundisha waliwahi wanafunzi kupata sup? how comes walimu wawajibike kwa suala mtambuka kama lile peke yao???
conclusion:
waziri amewaonea walimu wanaotakiwa kuwajibika ni TCRA, WAZAZI, WIZARA YA ELIMU.