KERO Waziri Mkenda umechemka, acha kutumia vibaya cheo chako kwa nidhamu ya woga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Huyu jamaa kakurupuka sana,hafai kuwa waziri,huo wimbo mimi mwenyewe mara ya kwanza kuusikia ni kwa mtoto wangu wa miaka mitano,sasa je atuhumiwe mwalimu au mzazi pamoja na mazingira?
Pili mwalimu sio mdhibiti wa nyimbo ,basata wapo,sasa kama basata wameruhusu wimbo huo kufika kwa jamii kosa la mwalimu ni lipi!?

Najuta sana kuwa mwalimu,ila kuna wanasiasa wanaopenda coverage kupitia kwa walimu,siku moja ajichanganye kwangu ,nitang'oa taya la mtu mimi.

Mwalimu ni mfanyakazi peke mwenye mabosi wengi nchi hii,mwenyekit wa kijiji/mtaa,diwani,mtendaji kijiji/ mtaa,mkuu wa shule,katibu kata,katibu tarafa,mkuu wa wilaya,mkurugenzi,afisa elimu,afisa elimu taaluma,tsc bado ngazi za mkoa,na taifa kma hao wapuuzi akina mkenda

Mwisho wa siku mkenda atambue kuwa kazi na dawa,hawa watoto wanahitaji burudani,shuleni sio magereza kwamba ni shuruba mwanzo mwiso
Mtoto wako aendelee tu kusika hyo mijimbo mbeleni utakuja ona faida yKe

Ova
 
Hii dunia haitaki kabisa kuona maskini ana furaha hata masaa tu.

Ukichek ile video watoto wanafurahi,yaani wamesahau kama nyumbani jana walilala njaa,wamesahahu kama hawana uniform za shule,wamesahau kama wanaishi kwenye nyumba za nyasi,wamesahau kama kwao hakuna umeme na vitu vingine vingi sana. Japo kwa muda tu,lakini walifarijika.

Kwa uelewa wangu mdogo sijui kama wale watoto kwa umri ule sijui hata kama wanajua maana hasa ya ule wimbo. usikute kuna wanaoupenda wimbo ule kwasababu tu ya kisauti cha zuchu,au mdundo(beat) ya wimbo au whatever.
Watoto kusikia ujumbe wa Kjng jng mnaona sifa,duh mitoto yote hapo
Hasara

Ova
 
Acha ujinga waziri yupo sahihi huwezi wachezesha watoto nyimbo za mapenzi umri ule. Hao waalimu akili zao finyu hata uwezo wa kusoma hatari hawana. Jitahidi uboreshe iq yako ipo chini sana
unaijua PG (Parental Guidance) Muongozo wa maudhui kulingana na rika?

waziri kaangalia tulipoangukia, nakuuliza maswali yafuatayo kama nyyumbani kwako utakuwa kishimbusi cha DSTV.

Je, uliwahi kuona logo ya PG 12, PG 13, P14?
Kamauliwahi kuona ,uliwahi kujiuliza kwa nini imewekwa?
Unafahamu wajibu wa sera ya madili kwa wanaonesha maudhui kwenye TV au redioni?
Je, wanafunzi kwenye muda wa likizio au mapumziko kuna sheria inawakataza kucheza/ au kucheza muziki?
Je, kwa nini watoto wale hawachezi muziki ule kanisani au msikitini??????
Je, ni halali kumvua cheo cha uprofesa mh. mkenda kwa sababu wanafunzi wengi walifeli somo analofundisha aua wanfunzi aliowafundisha wamekuwa mafisadi?
Nijibu haya nikutajie IQ yako

chanzo cha watoto kucheza muziki kimeanzia kwenye udhaifu wa udhibiti maudhui ya rika uliofanywa na TCRA na BASATA na Wizara ya Jinsia na wiZARA ELIMU KUKOSA MIIONGOZO ya UPIGAJI MUZIKI SHULENI. Kama tungekuwa muongozo DJ asingepiga muziki ule shuleni.
 
usikwazike waziri kafanya maamuzi kwa papara hili jambo linagusa maeneo mengi tuweke mkazo ili tufanikishe kwa pamoja , jiulize walimu walliopo wakijiuzuru wakaenda kufanya biashara nani atawafundisha hao watoto hapo shuleni. Ukumbuke kuacha kazi ni hiari so iktokea wameamua upande mwingine nani atafundisha? ni dosari ndogo ya kutoa maelekezo lakini siio kushusha mtu cheo
Ndiyo wameaanza mashuleni
Mambo ya kuwapeleka mashuleni wakina j lokole waache

Ova
 
Mtoto wako aendelee tu kusika hyo mijimbo mbeleni utakuja ona faida yKe

Ova
waziri kaangalia tulipoangukia, nakuuliza maswali yafuatayo kama nyyumbani kwako utakuwa kishimbusi cha DSTV.

Je, uliwahi kuona logo ya PG 12, PG 13, P14? (parental guidance)
Kamauliwahi kuona ,uliwahi kujiuliza kwa nini imewekwa?
Unafahamu wajibu wa sera ya madili kwa wanaonesha maudhui kwenye TV au redioni?
Je, wanafunzi kwenye muda wa likizio au mapumziko kuna sheria inawakataza kucheza/ au kucheza muziki?
Je, kwa nini watoto wale hawachezi muziki ule kanisani au msikitini??????
Je, ni halali kumvua cheo cha uprofesa mh. mkenda kwa sababu wanafunzi wengi walifeli somo analofundisha aua wanfunzi aliowafundisha wamekuwa mafisadi?
Nijibu haya nikutajie IQ yako

chanzo cha watoto kucheza muziki kimeanzia kwenye udhaifu wa udhibiti maudhui ya rika uliofanywa na TCRA na BASATA na Wizara ya Jinsia na wiZARA ELIMU KUKOSA MIIONGOZO ya UPIGAJI MUZIKI SHULENI. Kama tungekuwa muongozo DJ asingepiga muziki ule shuleni.

mzazi unao wajibu wa kuzuia chaneli zipi mwanao atazame jukumu la kulea ni la kwako na sio mwalimu.
 
Yaani waziri anaongea utadhani amekunywa bia bingwa. Mamlaka za uteuzi zimwangalie kwa jicho la pili huyu mtu
 
Ndiyo wameaanza mashuleni
Mambo ya kuwapeleka mashuleni wakina j lokole waache

Ova
TCRA ,BASATA watoe maelekezo kwa wamiliki wa wa TV na Rediio wadhibiti maudhui yasiyofaa kwa watoto, mzazi awekewe pg kwenye channel ili uamue kwa hiari yako waangalie maudhui ya wakubwa waangalie maudhui ya watoto wenzao
 
Nimefuatilia maamuzi ya waziri Mkenda kwa wakuu wa shule na walimu waliohusika kwenye kucheza wimbo wa zuchu Binafsi naona maamuzi ya Waziri Mkenda ni ya kukurupuka na hofu ya kutenguliwa nyadhifa yake. :

1. Maadili ya mtoto yaanzia nyumbani, Hawa watoto huu wimbo wamjifunza makwao kupitia redio na TV. Ukitizama Luninga DSTV wanaand kitu kinaitwa PG ,(Parental Guidance) utaona PG12,PG13,PG14 wakimaanisha mza kama mwanao sio miaka 12,13 au 14 asiangalie kwa sababu maudhui yake sio salama kwa maadili na ukuaji. Mwenye wajibu wa kuzia watoto wasiujue wimbo wa ZUCHU ni @tcra_tanzania kwa ushirikiano wa muongozo wa maadili ya watoto toka wizara ya Mh. Gwajima na wao wizara ya elimu.

(2) Wizara ya Elimu inaruhusu michezo na muziki ni sehemu ya michezo, hususani kwenye tafrija za shule (Graduation) Kungelikuwepo PG ya TCRA na wizara DJ wa siku hiyo asingelipiga wimbo wa zuchu. Mtaala wa michezo unautambua muziki kama sehemu ya nyezo ya ufundishaji na kuandaa vipaji.

(3) Wazazi wa hawa watoto wanawajibika moja moja kwa athari chanya kwa makusudi wameacha rimoti za TV na watoto wao wakajifunza wimbo wa zuchu kwa sababu ule mwitikio kufuatisha mashairi nimkubwa sana ina maanisha watoto wote wanajua kuimba beti kwa beti ingawaje hata neno mpenzi wangu hawajuui maana yake , je nani atawaadhibu wazazi hawa kwa mmomonyoko wa maadili ulioleta athari chanya kwa watoto wao?

(4)Nani atawatetea walimu walioamua kufurahi na watoto wakaonekana wao sio peke yao wenye makosa juu ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto hawa? Walimu ni sawa na third part kwenye mkataba hawana madhara ya moja kwa moja wanakuwa subjective kwa impact ya maoni ya mitandao. Tutafukuza walimu wangapi? Je, Graduation ngapi watoto wetu wancheza mbele ya wazazi na wazazi tunafurahi? Je , sherehe ngapi sisi watu wazima tumedhuruia halafu watoto wetu wanatoa show kushindana kucheza.

(5) Waziri wa Elimu katumia vibaya madarka yake kuwashusha vyeo walimu kwa makosa yasisowahusu moja kwa moja, natamani nione na afisa maendeleo ya Jamii wa mkoa husika na kata husika akiwajibishwa kwa madhara ya ukosefu wa maadili kwa ni kweli?

(6) Hivi leo hii seneti ya chuo kikuu Dar es salaam imvue hadhi uprofesa kwa sababu somo alilofundisha waliwahi wanafunzi kupata sup? how comes walimu wawajibike kwa suala mtambuka kama lile peke yao???

conclusion:
waziri amewaonea walimu wanaotakiwa kuwajibika ni TCRA, WAZAZI, WIZARA YA ELIMU.
@Mkenda
 
Huyu jamaa kakurupuka sana,hafai kuwa waziri,huo wimbo mimi mwenyewe mara ya kwanza kuusikia ni kwa mtoto wangu wa miaka mitano,sasa je atuhumiwe mwalimu au mzazi pamoja na mazingira?
Pili mwalimu sio mdhibiti wa nyimbo ,basata wapo,sasa kama basata wameruhusu wimbo huo kufika kwa jamii kosa la mwalimu ni lipi!?

Najuta sana kuwa mwalimu,ila kuna wanasiasa wanaopenda coverage kupitia kwa walimu,siku moja ajichanganye kwangu ,nitang'oa taya la mtu mimi.

Mwalimu ni mfanyakazi peke mwenye mabosi wengi nchi hii,mwenyekit wa kijiji/mtaa,diwani,mtendaji kijiji/ mtaa,mkuu wa shule,katibu kata,katibu tarafa,mkuu wa wilaya,mkurugenzi,afisa elimu,afisa elimu taaluma,tsc bado ngazi za mkoa,na taifa kma hao wapuuzi akina mkenda

Mwisho wa siku mkenda atambue kuwa kazi na dawa,hawa watoto wanahitaji burudani,shuleni sio magereza kwamba ni shuruba mwanzo mwiso
Kosa la Mwalimu ni kutochuja. Ni kweli dunia ni jalala lakini kuna nafasi ya kuchuja kipi ni kipi. Huwezi ukasema kwa sababu mtoto(mwanafunzi) 'ameruhusiwa' na wazazi wake kufanya ngono basi ni ruksa pia kwa Mwalimu kufanya nae ngono.

Samahani kwa mfano mbaya.
Nipo pamoja na waziri.
 
hoja yako nzuri sana, tena sana lakini ni nzito kuliko uzito wa hoja tunayoijadili tumfukuze sheikh msikitini asiswalishe kwa sababu muumini wake amekamatwa anaiba? na huy naye atakuwa hajachuja waumini wa kuwafundisha dini? tuwaache walimu kila mzazi awajibike aangalie watoto wake wanatizama nini kwenye luninga? hapo vipi tuendelee na waziri au tubaki na walimu
 
Kama Shehe(Mchungaji) ameshiriki kwenye huo 'ukibaka' wa huyo kibaka kwa nini asifukuzwe?
 
walimu wameshiriki vipi kufundisha watoto shairi la zuchu ubeti kwa ubeti, ukitizama video watoto wanaimba bila kukosea ubeti hata mmoja. Muziki ni sehemu ya michezo wewe graduation ngapi watoto wanacheza nyimbo za hovyo Tanzania nzima , tuwaache walimu wazazi tulee watoto wetu hiyo ni reflection kwamba wazazi wa kitanzania hatuzingatii watoto wanajifunza nini kwenye tv. Katika mfano wangu wa sheikh namaanisha sheikh aliyenyooka na hawa wlimu wamenyooka wao walikuwa wanacheza na watoto kama sehemu ya michezo na muziki ni michezo
 
hoja yako nzuri sana, tena sana lakini ni nzito kuliko uzito wa hoja tunayoijadili tumfukuze sheikh msikitini asiswalishe kwa sababu muumini wake amekamatwa anaiba? na huy naye atakuwa hajachuja waumini wa kuwafundisha dini? tuwaache walimu kila mzazi awajibike aangalie watoto wake wanatizama nini kwenye luninga? hapo vipi tuendelee na waziri au tubaki na walimu
Haya maisha ni kama kucheza mpira uwanjani,mwenzako akipuyanga wewe chap sana rekebisha kosa lake ili msifungwe. Mzazi kashindwa kulea mwanae nyumbani mimi Mwalimu nitamlelea mwanae shuleni.
Nafasi ya kumkaba Shetani ikipatikana ni anakabwa hadi koromeo liwake moto[emoji120]
 
walimu wameshiriki vipi kufundisha watoto shairi la zuchu ubeti kwa ubeti, ukitizama video watoto wanaimba bila kukosea ubeti hata mmoja. Muziki ni sehemu ya michezo wewe graduation ngapi watoto wanacheza nyimbo za hovyo Tanzania nzima , tuwaache walimu wazazi tulee watoto wetu hiyo ni reflection kwamba wazazi wa kitanzania hatuzingatii watoto wanajifunza nini kwenye tv. Katika mfano wangu wa sheikh namaanisha sheikh aliyenyooka na hawa wlimu wamenyooka wao walikuwa wanacheza na watoto kama sehemu ya michezo na muziki ni michezo
Walimu kwa nafasi yao walitakiwa waoneshe kuchefukwa na huo wimbo kichefuchefu na sio kuulamba[emoji120]
 
Hao watoto watapoteza Usichana / bikra zao mapema sana
 
Kabisa mkuu. Waziri kashughulikia tulipoangukia badala yatulipojikwaa. BASATA wapo na wanabariki nyimbo hizi kusikika na kuchezwa kwenye vyombo vya habari na si hao waalimu wakuu.
Kitu ambacho mnashundwa kukiona ni kwamba mawaziri wawili Prof Mkenda na Dr Gwajima wametuma ujumbe tosha kwa BASATA, na pia kwa Waziri mwenye dhamana na BASATA, kwamba wameshindwa kutimiza wajibu wao hivyo wao wameamua kuwasaidia kuifanya hiyo kazi. Huwezi kuruhusu nyimbo za kijinga kabisa kuchezwa mashuleni, ambapo walau tunategemea kutusaidia kujenga maadili bora kwa watoto wetu, kwa sababu wazazi walio wengi, hasa wazazi vijana ambao wanazalishana hovyo hovyo na tena bila malezi mazuri ya pamoja (wazazi wote). Hizo nyimbo zikapigwe huko Bar ili walevi washikane vizuri viuno na wahudumu wa Bar au madada poa, na siyo kuziruhusu mashuleni. Halafu walimu wa siku hizi hawajui hata kufundisha wanafunzi nyimbo za hamasa, upendo, bidii ya masomo na kazi nk kazi yao ni kuweka flash kwenye Subufa na kupiga haniiiii haniiiii... biunoo biunoooo daaah aiseeee...
 
Yaani ni kichefuchefu
 
Back
Top Bottom