KERO Waziri Mkenda umechemka, acha kutumia vibaya cheo chako kwa nidhamu ya woga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hili goma watoto wameselebuka daa honey honey daa kizazi hiki shida pole mwalimu kwa kusombwa ba honey
 
Prof amefanya jambo jema sana na hili liwe funzo kwa wengine kuruhusu watoto kuimba na kucheza manyimbo ya hovyohovyo hatuwezi kuwa n taifa ka mitoto inayoimba namkatia vibuno
 
Hili goma watoto wameselebuka daa honey honey daa kizazi hiki shida pole mwalimu kwa kusombwa ba honey
walimu watafukuzwa kazi kwa wahaka na mizuka kwa mambo yasiyowahusu
 

 
ATUMBULIWE tu huyo waziri anatoa maamuzi kimihemuko!
 
Huyu jamaa kakurupuka sana,hafai kuwa waziri,huo wimbo mimi mwenyewe mara ya kwanza kuusikia ni kwa mtoto wangu wa miaka mitano,sasa je atuhumiwe mwalimu au mzazi pamoja na mazingira?
Pili mwalimu sio mdhibiti wa nyimbo ,basata wapo,sasa kama basata wameruhusu wimbo huo kufika kwa jamii kosa la mwalimu ni lipi!?

Najuta sana kuwa mwalimu,ila kuna wanasiasa wanaopenda coverage kupitia kwa walimu,siku moja ajichanganye kwangu ,nitang'oa taya la mtu mimi.

Mwalimu ni mfanyakazi peke mwenye mabosi wengi nchi hii,mwenyekit wa kijiji/mtaa,diwani,mtendaji kijiji/ mtaa,mkuu wa shule,katibu kata,katibu tarafa,mkuu wa wilaya,mkurugenzi,afisa elimu,afisa elimu taaluma,tsc bado ngazi za mkoa,na taifa kma hao wapuuzi akina mkenda

Mwisho wa siku mkenda atambue kuwa kazi na dawa,hawa watoto wanahitaji burudani,shuleni sio magereza kwamba ni shuruba mwanzo mwiso
 
Hajachemka amefanya vyema
huyu ni mwoga suala jepesi hapa , je wazazi nao wafukuzwe kazini kwa kwa kushindwa kuwalea watoto wao kwa sababu wanaimba matusi? vipi tumfukuze sheikh msikitini kwa sababu muumini wake ni kibaka? au tumfukuze padri kwa kosa mwenyekiti wa Jumuiya amebaka? hili ndio tatizo la waziri kawafukuza walimu kwa kosa lisilowahushu
 
sawa kabisa tuwasaidie walimu warudi kazini huwezi kumuondoa imamau msikitini kwa sababu watoto wa madrasa wameedna kuiba maembe sokoni, huwezi kumfukuza mchungaji kwa sababu muuumini wake ni mlevi wa kupindukia
 
Jinga kabisa. Unataka shuleni wasisitize maadili kwa sababu nyumbani kuna baadhi hawakufunzwa? Kuna mijitu upeo wao wa kuona mambo ni kama wa nyumbu.
Tumfukuze sheikh kwa sababu waumini anaowafundisha wameiba? kwa nini mwalimu afukuzwe kazi kwa kosa la mzazi na mamlaka nyingine.
 
Makosa yapo, lkn HAYASTAHILI kutoa adhabu kubwa kama hiyo.

Waalimu kwa ujumla wanabeba ADHABU nyingi za kila siku katika UTUMISHI wao.

Onyo tu! Linatosha .
 
Hii dunia haitaki kabisa kuona maskini ana furaha hata masaa tu.

Ukichek ile video watoto wanafurahi,yaani wamesahau kama nyumbani jana walilala njaa,wamesahahu kama hawana uniform za shule,wamesahau kama wanaishi kwenye nyumba za nyasi,wamesahau kama kwao hakuna umeme na vitu vingine vingi sana. Japo kwa muda tu,lakini walifarijika.

Kwa uelewa wangu mdogo sijui kama wale watoto kwa umri ule sijui hata kama wanajua maana hasa ya ule wimbo. usikute kuna wanaoupenda wimbo ule kwasababu tu ya kisauti cha zuchu,au mdundo(beat) ya wimbo au whatever.
 
MITOTO YENU HAINA HAJA KUWAFATILIA ACHA WASIKIE TU HIYO MIZIKI HONEYY NA TAKA TAKA ZINGINE,KWANZA MITOTO YENU SAHV ISHAKATA KAMBA
NA MPAKA KUFIKA 2030 HUKO WATAKUWA WAMECHAKAA

OVA
 
Naungana mkono na wewe, waalimu wakuu wameonewa
Vitoto vimekariri kila neno la wimbo huko makwao. kama siyo nyumbani ni kwa jirani
mimi mwenyewe nimependa vibe la vitoto
Acha wakate mauno tu
Wekezeni wajue kbandn vzr tu

Ova
 
Prof amefanya jambo jema sana na hili liwe funzo kwa wengine kuruhusu watoto kuimba na kucheza manyimbo ya hovyohovyo hatuwezi kuwa n taifa ka mitoto inayoimba namkatia vibuno
nyimbo wamejifunza shuleni au makwao? wewe ungekuwa imamau au mchungaji ungekubali kuondolewa cheo chako kwa sababu muuumini wako ni mwizi? ukiona haiwezekani basi ujue walimu wameonewa
 
NCHI ISHAKUWA YA WAKATA MAUNO SAHV

OVA
 
Acha wakate mauno tu
Wekezeni wajue kbandn vzr tu

Ova
usikwazike waziri kafanya maamuzi kwa papara hili jambo linagusa maeneo mengi tuweke mkazo ili tufanikishe kwa pamoja , jiulize walimu walliopo wakijiuzuru wakaenda kufanya biashara nani atawafundisha hao watoto hapo shuleni. Ukumbuke kuacha kazi ni hiari so iktokea wameamua upande mwingine nani atafundisha? ni dosari ndogo ya kutoa maelekezo lakini siio kushusha mtu cheo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…