Waziri Mkuu aelezea ubadhirifu wa mamilioni uliofanywa Bohari ya Dawa (MSD), asema ataenda akiongozana na Polisi na TAKUKURU

Chanzo cha tatizo letu ni ujinga uliochanganyikana na umasikini kwa viongozi wetu, ndio maana matatizo ya hili taifa hayaishi.
 
Matatizo yanaanzia chini kushuka chini, hakuna mtu anaweza kujiamini akaiba kama watawala hawaibi
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

"Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate," amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.
Vipi wale jamaa wa BOT waliojilipa posho za kufulu.. Majalliwa alienda pale... Je walichukuliwa hatua????
 
Uzuri ni kwamba serikalini wakishabaini hayo hakuna action yoyote inayochukuliwa kwa waliohusika

Iligundulika stendi ya mabasi pale Kibaha ilikuwa chini ya kiwango na haikuzinduliwa lakini hadi leo inafanya kazi na waliopiga ndio wanatutimulia mavumbi na magari yao ya kifahari

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Huyu abdul unayemzungumzia hapa ndio huyu mtoto wa Mama Samiah Hassan, naona watoto wa vigogo wakiendelea kubebwa na Wazazi wao kujinufaisha wao wenyewe. Hatari sana hii
 
Jamaa wamejipanga kula nchi vizuri sn
 
Huyu abdul unayemzungumzia hapa ndio huyu mtoto wa Mama Samiah Hassan, naona watoto wa vigogo wakiendelea kubebwa na Wazazi wao kujinufaisha wao wenyewe. Hatari sana hii
Yupo Dubai huyu habari zake na ushiriki wake kwenye zabuni za mafuta tunazo. Hii Nchi ina laana. Yaani ukiondoa watoto wa Nyerere, Marais wote waliofata ni wapiga dili tu wao na familia zao tofauti ni kiasi cha upigaji tu (Mfano Mkapa alijiuzia mgodi wa kiwira, kikwete na ishu ya escrow, magufuli na ununuzi wa ndege bila uwazi uwanja wa ndege chato) sasa tuna abdul mtoto wa samia.
 
Jana tarehe 05 Mei, 2022 Mhe. Waziri Mkuu akiwa katika kongamano la Maafisa Manunuzi aliongelea hali ya ufisadi katika manunuzi yaliyofanyika MSD. Kwa wapenda uwajibikaji...

Hata kama ni kupiga tupige pole pole huu ni urafi.
Wote hawa ni dini moja lakini Ijumaa utawakuta sehemu fulani wanajifanya watu wa Mungu
 
Daaaa mambo yaenda mbio sana acha tupate yajayo...
 
Huyu hua simuamini.

Alituambia August 2019 SGR itaanza kazi ! ikapita.

Mara tena April 2022 napo kimya.

Magufuli yuko fit anachapa kazi , ghafla kafariki.

Akasema tena mazishi ya Magufuli yametazamwa na watu billion 3 duniani kwenye TV.
 
Huyu hua simuamini.

Alituambia August 2019 SGR itaanza kazi ! ikapita...
Huyu mzee mwaka 2017 nilikutana naye live kwenye mambo fulani kumwangalia kichwani amepaka dawa nyeusi ilikuonekana nywele nyeusi mademu wasijue kama anamvi, kuanzia hapo nilimdharau sn, nikajiuliza nchi inamatatizo mengi hivi anapata wapi muda wa kwenda salon kila siku? ni mtu wa ajabu sn na muongo
 
Jana tarehe 05 Mei, 2022 Mhe. Waziri Mkuu akiwa katika kongamano la Maafisa Manunuzi aliongelea hali ya ufisadi katika manunuzi yaliyofanyika MSD. Kwa wapenda uwajibikaji tunakubalina kabisa hatua zichukuliwe kwa wahusika wote MSD katika kadhia hiyo ya manunuzi...
Yeye kazungumzia MSD kama unayo ya Tanroad weka hapa majungu hatutaki naona mmeanza kutumika kwa ajiri ya 2025 mmeanza mapema sana kuchafua watu
 
Sasa mkuu kwenye 300B ukitoa 17B unahasara gani? na bado una room ya kuendelea kuiba mali za umma
Ukiangalia ile kesi kule Mahakama ya usuluhishi ( ICSID) kulikuwa na grounds zote sisi kama Nchi kukata rufaa na kushinda kwa sababu wakati tunavunja mkataba na SYMBION tuliwataka waache kututoza capacity charges kwenye umeme wao kwa kuwa katika muda ule mitambo yetu ya gesi ya Kinyerezi ilikuwa ina uwezo wa kutupa umeme wa kutosha bila hata kununua ule wa Symbion. Wao wakakataa ndio Magu akaamua kuvunja mkataba. Kisheria tulikuwa na haki, Serikali ilitakiwa kusimamia maslahi mapana ya kesi hii na sio kulipa Symbion chapu na haraka.
 
Katelefoni mwongo jamani, yaani majaliwa kajaliwa huyu baba kwa fix fix. Akiongea kama mtu kweli
Ukimuona anapoongea utasema kiongozi si ndiyo huyu kumbe Mungu wangu ni bogasi la kutupwa. Halafu kuna mtu tunaambiwa anaupiga mwingi wakati wizi umetamalaki kila kona hivi vigezo vyetu vya kuwapima viongozi viko anti clockwise mbona kama sielewi??!!!!
 
Back
Top Bottom