Umbali wa kutoka Goli moja la mpira wa miguu hadi goli lingine kisha ukarudi hata kama ni kwa gari utatumia mafuta ya Tshs ngapi??
Labda tuanze hesabu zetu kwa style hii. Tufanye makisio/assumptions zile gari za msafara wa Waziri Mkuu zinaenda kilometa 7 kwa lita 1 ya mafuta. Na tufanye labda kila lita 1 inauzwa Tshs 2,000. Kwa hiyo kwa afuta ya Tshs 2,000 ambayo ni lita 1 zitaenda umbali wa kilometa 7.
Sasa basi kilometa 7 hizo ni sawa na mita 7,000. Kwa hiyo mafuta ya Tshs 2,000 ambayo ni lita 1 yanaweza kwenda umbali wa mita 7,000. Ndio kusema kwamba kila Tshs 1 inayotumika kwenye mafuta ina uwezo wa kuifanya gari iende mita (7,000 / 2000) = mita 3.5.
Au pia unaweza kusema kila mita 1 ina uwezo wa kuchukua mafuta ya Tshs 2000/7000 = Tshs 0.28. Yaani gari hizi kila zikisogea umbali wa mita 1 zinakua zimekula mafuta ya Cent 28. Na kama zitasogea umbali wa mita 200 basi zitakula mafuta ya Cent 28 x 200 ambayo ni kiasi cha Tshs 57.
Hizi gari kama ziko 7 basi tufanye zinakula mafuta ya Tshs 57 x 7 = Tshs 400 kwa zote saba kutembea umbali wa mita 200. Na kama zitarudi jioni basi itakua ni ara mbili ambayo inafikia Tshs 800. Labda tuseme na sababu zingine zingine basi zinakula mafuta ya Tshs 1,000 jumla kwa safari ya kwenda kumpeleka PM na kurudi nae jioni kwa siku moja.
Ili Msafara huu uweze kuokoa tuseme kiasi cha Tshs 1illion tu kwa hesabu hizi za Tshs 1,000 kwa siku basi inatakiwa uwe umetembea siku zipatazo (Tshs 1,000,000/ Tshs 1,000 kwa siku) = siku 1,000. Yaani PM akifanya misafara au siku 1,000 inayookoa Tshs 1,000 kwa siku ndio atakua ameokoa kiasi cha Tshs 1,000,000. Sasa hizo "mamilioni" zilizookolewa sijui itakua ni siku ngapi.
Mi naishia hapa, ila hizi hesabu zina assumptions zake mbalimbali, na pengine zinaweza kukuchanganya kama kwako hesabu ni tatizo.