Waziri Mkuu haondolewi kirahisi mnavyodhania. Akiondolewa Baraza la Mawaziri linavunjwa lote

Waziri Mkuu haondolewi kirahisi mnavyodhania. Akiondolewa Baraza la Mawaziri linavunjwa lote

Ni Mkapa Tu nafikiri hakuwahi kuvunja hilo Baraza la mawaziri, lakini Nyerere, Mwinyi, JK wote hawakusita kuvunja hayo mabaraza, ndiyo maana tuna orodha ndefu ya mawaziri wakuu, Nyerere, Kawawa, Sokoine, Salim Ahmed Salim, Warioba, Cleopa Msuya, John Malecela, Sumaye, Lowassa, Pinda, now Majaliwa
Who is next ??!!
 
Umeelewa hoja husika au unaleta ubishi wa kwenye kahawa?
Kama kuna wabunge wa kuwasimamia mawaziri, vyeo ambavyo haviko kisheria, ndio itakuwa kumtoa huyo waziri mkuu na kumuweka mwingine? Ingekuwa kuna anayejali gharama hapo sawa.
 
Kwani Waziri Mkuu hawezi kubadirishwa Wakati wa hiyo unayoiita reshuffle? Kwani Kassim mlimsikia akitoa nasaha pale baada ya mawaziri kuapishwa kama ilivyozoeleka huko nyuma??

PM hawezi kubadilishwa bila BW kuvunjwa. Hilo ni takwa la Katiba!
 
Mnapiga ramli juu ya PM Kassim kuondolewa mnadhania ni rahisi kama mnavyodhania?

Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisi anateua na kuapisha upya.

Someni ibara ya 57(2)(e) ya katiba ya JMT na muache kukurupuka kupiga ramli za kishamba.
KWANI KUAPISHA UPYA KUNATUMIA FEDHA ZA KIGENI MPAKA TUOGOPE?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Raisi ana uwezo wa kumpa ubunge mjinga yeyote anayemtaka kisha akampa uwaziri...

Ongeza ujuzi boss kwa free...

Nikupe references za waliopewa ubunge na uwaziri?
Hivi mbona hua mnajifanya watoto?? Membe ni Mbunge wa Jimbo gani la uchaguzi!! Au hujui hata sifa za mtu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu jombaa
 
Kila kitu kinawezekana nchi hii,hlo dogo sana kama mwenye nchi akiamua
Mnapiga ramli juu ya PM Kassim kuondolewa mnadhania ni rahisi kama mnavyodhania?

Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisi anateua na kuapisha upya.

Someni ibara ya 57(2)(e) ya katiba ya JMT na muache kukurupuka kupiga ramli za kishamba.
 
Hivi mbona hua mnajifanya watoto?? Membe ni Mbunge wa Jimbo gani la uchaguzi!! Au hujui hata sifa za mtu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu jombaa
Na ukiweza stop being too serious wenzako tuna have fun...

Maisha sio magumu hivyo...

Na hizi chats hazikuletei mapinduzi ya dhiki ama uchumi...

Punguza munkari mkuu
 
Mnapiga ramli juu ya PM Kassim kuondolewa mnadhania ni rahisi kama mnavyodhania?

Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisi anateua na kuapisha upya.

Someni ibara ya 57(2)(e) ya katiba ya JMT na muache kukurupuka kupiga ramli za kishamba.
Kwanini nyinyi wabongo kila kitu mnaona ni mchakato?., Rais kuvunja barazala la mawaziri ni chini ya dakika moja tu na kuunda list nyengine nikupelekewa mchapaji list ya majina tu pale ikulu jioni yake inasomwa habari kwisha, watu wanafanya shughuli zao
 
Mnapiga ramli juu ya PM Kassim kuondolewa mnadhania ni rahisi kama mnavyodhania?

Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisi anateua na kuapisha upya.

Someni ibara ya 57(2)(e) ya katiba ya JMT na muache kukurupuka kupiga ramli za kishamba.

..mbona Warioba, Malecela, na Lowassa, waliondolewa bila matatizo yoyote?

..wakati huu wa bunge la chama kimoja kuna shida gani kumuondoa Waziri Mkuu ikiwa Raisi hamtaki?

..wakati mwingine hoja imekuwa kwamba kumtunza Waziri mkuu mstaafu ni gharama kubwa.

..lakini kufariki kwa Mkapa na Magufuli kumeipunguzia serikali mzigo wa kuwatunza wastaafu.

..kwa hiyo gharama za matunzo ya viongozi wastaafu sio hoja tena ya kuzuia kumuondoa Waziri Mkuu.
 
51 (2).."mapema iwezekanavyo"...Kipengele hiki kinaongelea uundaji wa serikali mpya baada ya uchaguzi... haina limit yeyote ya mbunge wa kuteuliwa baadae kuwa waziri mkuu...
51(3) (d) inaongelea uteuzi wa mbunge mwingine bila kutaja kutoka jimboni ama chochote hivyo wakuteuliwa has a chance pia...
Ibara ya 51(2) ya Katiba ya JMT.
 
51 (2).."mapema iwezekanavyo"...Kipengele hiki kinaongelea uundaji wa serikali mpya baada ya uchaguzi... haina limit yeyote ya mbunge wa kuteuliwa baadae kuwa waziri mkuu...
51(3) (d) inaongelea uteuzi wa mbunge mwingine bila kutaja kutoka jimboni ama chochote hivyo wakuteuliwa has a chance pia...
Wewe unaonekana ni mbishi na hupendi kujifunza...huo si usomaji wa sheria, soma kifungu chote. I rest my case [emoji119]

51(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo ...

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa tz wala sio inshu,kwan kuteuwa baraza la mawaziri unazan n kaz sana kwa hawa watawala wetu!?
 
Back
Top Bottom