Suala la Ngorongoro lina pande mbili.
1. Wanaoamini wanyama, binadamu, na mifugo, wanaweza kuishi pamoja.
2. Wanaoamini wanyama, binadamu na mifugo hawawezi kuishi pamoja.
Jamii ya Wamaasai walioko Ngorongoro walihamishwa toka maeneo ya mbuga ya Serengeti wakati wakoloni walipoamua Serengeti iwe hifadhi ya taifa.
Wamaasai wa Ngorongoro wamekuwa wakiishi na wanyama na kulisha mifugo yao bila matatizo kwa muda mrefu sasa.
Jamii hiyo ina uzoefu mkubwa wa kujua majira mbalimbali ya ukuaji na upatikanaji wa malisho na movement za wanyama kulingana na misimu ktk mwaka.
Kwa mfano majira ambayo nyumbu wengi huzaliana Wamaasai wanajua wapi pa kwenda kulisha mifugo.
Pia msimu wa nyumbu kuhama kwa makundi makubwa Wamaasai hujua jinsi gani na eneo gani wanaweza kuchunga mifugo.
Zaidi Wamaasai wanajua jinsi ya kutunza maeneo ya malisho. Kuna msimu wa kuchoma majani ili kuzuia magugu mabaya yasiote na kutoa nafasi kwa malisho mazuri kumea.
Zoezi la kuchoma moto maeneo ya Serengeti na ktk hifadhi hufanywa hata na serikali / TANAPA.
Kwa kifupi Wamaasai sio maadui wa wanyama au uhifadhi hapa Tanzania. Kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na utaratibu SHIRIKISHI huko Ngorongoro ili kila upande ufaidike.