Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Wabunge wote waelezwe kinachoendelea Ngorongoro

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Wabunge wote waelezwe kinachoendelea Ngorongoro

Ukisema na bado ukimaanisha nini? Hiyo ni vita yenu wenyewe kwa wenyewe, yanipasani mimi? Hao wamasai wa Ngorongoro hawajawai chagua upinzani maisha yao yote.

Hiyo ni mbwa mwitu wanakulana wenyewe kwa wenyewe na shauri yao.
Mkuu kuna ukweli kwenye hilo ila kuna mwamko mkubwa sana katika Jamii ya Wamasai, Uchaguzi (uchafuzi) wa mwaka 2020 waliamua kulinda kura zao na kuna msimamizi alijaribu kuiba kura kwenye kituo kimoja alipelekewa Mkuki....baadaye polisi walikuja kufanya yao
 
Unaoushahidi? Jaribu kuwa Makini
Si ametolewa tayari jela unadhani atarudi shule kurisiti na kwenda kusomea kozi ya hotel management ili akafanye kazi Fountain Hotel kama manager?!

Huyo bibi karudi mzigoni tayari na anajipanga kivingine. Tembo na wanyama wengine wanarudi tena hatarini..... [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]

MUNGU baba mpe mzee wetu magufuli uongozi wa malaika ili atulinde raia kutokea Angani.
 
Hii ni aibu kwakweli mbunge yupo Tanzania anachangia kwa jambo lililopo Tanzania ambalo hifahamu.

Halafu unategemea mtu huyu huyu akatunge sheria zenye tija.

Sahau hilo.
 
Hao wamasai wa ngorongoro wajiandae kisaikolojia muda wowote wanaondolewa huko kwenye hifadhi
 
Kwanini msi waondoe hao wanyamapori na kuwaachia wamasaai hayo maeneo yao ya asili ya loliondo na ngorongoro??
Mbona wananchi wengine huondoka kwenye maeneo yao ya asili inapohitajika kufanya ivyo? Hao wamasai wao ninani wasihame.

Kama tukiendekeza huu upuuzi jamii nyingine pia zitagoma kupisha miradi mbalimbali kwa kisingizio cha maeneo yao ya asili.

Kama wanaishi kwa mujibu wa sheria ni sawa, ila sasa sheria hiyo imepitwa na wakati kabisa walipwe fidia waondoke
 
MAsai people are our last frontier , Wamasai wameishi na wanyama kwenye mbuga zetu kwa muda mrefu sana.Lakini sasa naona kuna uvamizi mkubwa sana kwa wamasai wengine kutoka sehemu nyingine za makazi na kuamua kwenda kuishi kwenye mbuga na hifadhi za taifa sababu upatikanaji wa ardhi ya kujenga na kulisha mifugo ni rahisi.
Serikali inachotakiwa kufanya ni kuorodhesha watu wote wanao ishi kwenye mbuga na hifadhi na kutoruhusu ujenzi wowote ule . Na watoe kibali cha miaka 99 wote waondoke kwenye hifadhi.
 
Si ametolewa tayari jela unadhani atarudi shule kurisiti na kwenda kusomea kozi ya hotel management ili akafanye kazi Fountain Hotel kama manager?!

Huyo bibi karudi mzigoni tayari na anajipanga kivingine. Tembo na wanyama wengine wanarudi tena hatarini..... [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]

MUNGU baba mpe mzee wetu magufuli uongozi wa malaika ili atulinde raia kutokea Angani.
Daaah
 
Suala la Ngorongoro lina pande mbili.

1. Wanaoamini wanyama, binadamu, na mifugo, wanaweza kuishi pamoja.

2. Wanaoamini wanyama, binadamu na mifugo hawawezi kuishi pamoja.

Jamii ya Wamaasai walioko Ngorongoro walihamishwa toka maeneo ya mbuga ya Serengeti wakati wakoloni walipoamua Serengeti iwe hifadhi ya taifa.

Wamaasai wa Ngorongoro wamekuwa wakiishi na wanyama na kulisha mifugo yao bila matatizo kwa muda mrefu sasa.

Jamii hiyo ina uzoefu mkubwa wa kujua majira mbalimbali ya ukuaji na upatikanaji wa malisho na movement za wanyama kulingana na misimu ktk mwaka.

Kwa mfano majira ambayo nyumbu wengi huzaliana Wamaasai wanajua wapi pa kwenda kulisha mifugo.

Pia msimu wa nyumbu kuhama kwa makundi makubwa Wamaasai hujua jinsi gani na eneo gani wanaweza kuchunga mifugo.

Zaidi Wamaasai wanajua jinsi ya kutunza maeneo ya malisho. Kuna msimu wa kuchoma majani ili kuzuia magugu mabaya yasiote na kutoa nafasi kwa malisho mazuri kumea.

Zoezi la kuchoma moto maeneo ya Serengeti na ktk hifadhi hufanywa hata na serikali / TANAPA.

Kwa kifupi Wamaasai sio maadui wa wanyama au uhifadhi hapa Tanzania. Kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na utaratibu SHIRIKISHI huko Ngorongoro ili kila upande ufaidike.
Umeeleza vizuri sanaa mkuu... Swali tokea miaka hiyoo walipohamishiwa hapo Ngorongoro, ambapo natumai walikuwa wachache na Mifugo yao Michache. Ukichukulia kwamba eneo la NCAA ni lile lile (liko fixed) na kwa hakika hao wamasai watakuwa wameongezeka sanaa je hili si ni tatizo jipya la kugombania fixed resources??
 
Kunatakiwa uwiano mzuri kati ya wanyama na binadamu
Binadamu wanazidi kuongezeka zaidi ya wanyama. Miaka ijayo hakutakuwa na wanyama
Mbona Ulaya wameendelea bila hata hao wanyama,, China urusi na uturuki Kuna mbuga ngapi za wanyama......


Kinachoweza kutuletea maendeleo dunia ya leo ni watu si wanyama

Ng'ombe hao wa Masai ni bora kuliko hao wanyama pori wanaoishi humo ngorogoro

Hao mnaowaita watalii wanakuja kufaidisha matajiri waliojenga mahoteli kwenye mbuga hizo huku wananchi wa kawaida hawafaidiki kwa chochote
 
Nakubaliana wamasaai waondolewe Ngorongoro. Leo ukienda kule hifadhini utashangaa wanyama wa kufugwa wanavyozidi kuongezeka kuwazidi wanyama wa asilia. Ngorongoro ni eneo la hifadhi ya Dunia, lazima itunzwe kwa gharama yoyote. Period!!
Umeenda huko lini????

Watanzania kwa unafiki hamjambo!!!!!


Kosa la Masai ni kuwaacha hao wanyama pori waongezeke ndio inawapa shida leo
 
Umeeleza vizuri sanaa mkuu... Swali tokea miaka hiyoo walipohamishiwa hapo Ngorongoro, ambapo natumai walikuwa wachache na Mifugo yao Michache. Ukichukulia kwamba eneo la NCAA ni lile lile (liko fixed) na kwa hakika hao wamasai watakuwa wameongezeka sanaa je hili si ni tatizo jipya la kugombania fixed resources??

..hata mimi nilikuwa na mtizamo kwamba upo uwezekano idadi ya watu na mifugo imeongezeka sana Ngorongoro.

..lakini nikaja kusikia kwamba kuna study ilifanywa na Danida 1982 na kubaini kwamba Wamaasai wamekuwa masikini zaidi tangu wahamishiwe Ngorongoro kwa kupoteza mifugo yao.

..inasemekana Danida walipendekeza ufanyike utaratibu wa kuwaongezea Wamaasai wa Ngorongoro mifugo, jambo ambalo linapingwa vikali na wahifadhi maofisa wa serikali.

..Sasa inawezekana kwamba mwaka 1982 mpaka sasa hivi ni muda mrefu na idadi ya watu na mifugo imeongezeka kiasi cha kutishia uhai wa Ngorongoro kwa hiyo hatua za kurekebisha hali hiyo zinatakiwa zichukuliwe.

..Lakini vilevile suala la uharibifu wa mazingira unaotokana na ujenzi wa mahoteli makubwa, camps za watalii, na mambo mengine ya kisasa, ni suala ambalo linatakiwa litupiwe macho. Isiwe kwamba wanahamishwa Wamaasai halafu anakuja mwenye fedha anapewa eneo aendeleze kwa namna ambayo inaathiri uasili wa eneo la Ngorongoro.
 
Back
Top Bottom