Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anataka wamasai watoke waweke Mahoteli yao ya kitalii kwa faida ya familia zao, Hawa Wanasiasa sio watu wazuri kabisa.Waache siasa, Ngorongoro inataka kuporwa na Chui jike na mawakala wake.
Kwani kuna hifadhi ambayo watu wanaishi hifadhini zaidi ya ngorongoro.Sijakuelewa. Nilichouliza ni kwamba Serikali inataka kuwaaondoa watu kwenye hifadhi ya Ngorongoro ili wanyama waongezeke. Swali langu ni kwamba jee, ni Ngorongoro tu kunakokuwepo na mgongano wa watu na wanyama? Au kuna kitu kingine nyuma ya pazia kunakofanya hicho kiwe kisingizio?
Huwezi tenganisha hifadhi na watalii sasa wakija wafikie wapi kama sio kwenye mahoteli pia hayo mahoteli yameajiri watanzania wengi sana sasa hao wamasai wameajiri nani achunge hao ng'ombe hayo ni maeneo ya kitalii...hata mimi nilikuwa na mtizamo kwamba upo uwezekano idadi ya watu na mifugo imeongezeka sana Ngorongoro.
..lakini nikaja kusikia kwamba kuna study ilifanywa na Danida 1982 na kubaini kwamba Wamaasai wamekuwa masikini zaidi tangu wahamishiwe Ngorongoro kwa kupoteza mifugo yao.
..inasemekana Danida walipendekeza ufanyike utaratibu wa kuwaongezea Wamaasai wa Ngorongoro mifugo, jambo ambalo linapingwa vikali na wahifadhi maofisa wa serikali.
..Sasa inawezekana kwamba mwaka 1982 mpaka sasa hivi ni muda mrefu na idadi ya watu na mifugo imeongezeka kiasi cha kutishia uhai wa Ngorongoro kwa hiyo hatua za kurekebisha hali hiyo zinatakiwa zichukuliwe.
..Lakini vilevile suala la uharibifu wa mazingira unaotokana na ujenzi wa mahoteli makubwa, camps za watalii, na mambo mengine ya kisasa, ni suala ambalo linatakiwa litupiwe macho. Isiwe kwamba wanahamishwa Wamaasai halafu anakuja mwenye fedha anapewa eneo aendeleze kwa namna ambayo inaathiri uasili wa eneo la Ngorongoro.
Mkuu umeongea vyema nnachokiona ukiwa makini na wanayoyaongea watawala utagudua Ni ama kunakitu hakipo sawa, au kunamtu anawashinikiza kufanya maamzi, Sasa hebu twende tu kwenye maana ya utalii,Suala la Ngorongoro lina pande mbili.
1. Wanaoamini wanyama, binadamu, na mifugo, wanaweza kuishi pamoja.
2. Wanaoamini wanyama, binadamu na mifugo hawawezi kuishi pamoja.
Jamii ya Wamaasai walioko Ngorongoro walihamishwa toka maeneo ya mbuga ya Serengeti wakati wakoloni walipoamua Serengeti iwe hifadhi ya taifa.
Wamaasai wa Ngorongoro wamekuwa wakiishi na wanyama na kulisha mifugo yao bila matatizo kwa muda mrefu sasa.
Jamii hiyo ina uzoefu mkubwa wa kujua majira mbalimbali ya ukuaji na upatikanaji wa malisho na movement za wanyama kulingana na misimu ktk mwaka.
Kwa mfano majira ambayo nyumbu wengi huzaliana Wamaasai wanajua wapi pa kwenda kulisha mifugo.
Pia msimu wa nyumbu kuhama kwa makundi makubwa Wamaasai hujua jinsi gani na eneo gani wanaweza kuchunga mifugo.
Zaidi Wamaasai wanajua jinsi ya kutunza maeneo ya malisho. Kuna msimu wa kuchoma majani ili kuzuia magugu mabaya yasiote na kutoa nafasi kwa malisho mazuri kumea.
Zoezi la kuchoma moto maeneo ya Serengeti na ktk hifadhi hufanywa hata na serikali / TANAPA.
Kwa kifupi Wamaasai sio maadui wa wanyama au uhifadhi hapa Tanzania. Kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na utaratibu SHIRIKISHI huko Ngorongoro ili kila upande ufaidike.
Siku ya machifu Tanzania ndoimeleta yote haya, ndo mana wanngorongoro wana viburi kweli
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iandae semina kwa wabunge wote ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu yanayoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Februari 9, 2022) wakati alipochangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Huwezi tenganisha hifadhi na watalii sasa wakija wafikie wapi kama sio kwenye mahoteli pia hayo mahoteli yameajiri watanzania wengi sana sasa hao wamasai wameajiri nani achunge hao ng'ombe hayo ni maeneo ya kitalii.
Mnawafukuza wamasaai toka Ngorongoro na loliondo ambayo ni maeneo yao ya asili waende wapi? mmeisha waandalia sehem ya kwenda? hayoo mahifadhi na mambuga yenu yamewakuta wamaasai apo sasa sijui mnatakaje, basi waueni wamasaai wote mioyo yenu ilizikee sasa!
Hivi ndivyo heading ya huu uzi ilitakiwa iwe, walioagizwa ni Wizara na siyo wabungeWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iandae semina kwa wabunge wote ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu yanayoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro.
DaaahHivi wao hawavutii watalii?
Kaziiendelee Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iandae semina kwa wabunge wote ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu yanayoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Februari 9, 2022) wakati alipochangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2021, Bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema kuwa anaamini wapo wabunge wanaofahamu na wasiofahamau kuhusu yanaoendelea katika hifadhi hiyo “wakati tukiwa tunazungumza na wananchi, naiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya semina ya siku moja kwa wabunge wote ili wizara iwaambie kuna nini kule Ngorongoro, nini kilikuwepo awali na hali gani ipo sasa ili tuwe na uelewa wa pamoja”
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali kukutana na wakazi wanaoshi katika eneo la hifadhi Ngorongoro na utekelezaji wake umeanza kwa kukutana na viongozi wa mkoa wa Arusha na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
“Hatua iliyobaki ni kwenda Ngorongoro, nitafanya mikutano eneo la Ngorongoro, nitafanya mikutano na wakazi wa eneo la Loliondo, baada ya kufanya haya yote itatusaidia kuendesha zoezi hili kwa amani kabisa kadiri itakavyokuwa imeamriwa”
Akizungumza wakati akichangia hoja ya kamati hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Wizara italeta mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya Ngorongoro kulingana na mapendekezo ya kamati na maoni ya wabunge.
“Sheria ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1975 ni ya muda mrefu, mliyoongea Waheshimiwa wabunge yameonesha kuna mapengo kwenye sheria ile, msingi wa Sheria ile ni nguzo tatu za Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii, inaonekana nguzo hizi zimeshindikana kushikiliwa kwa pamoja”
Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia inajali haki za binadamu “hatutafanya chochote ambacho kiko kinyume na haki za binadamu, na kwa kuwa tunaheshimu haki za binadamu hatutaingilia uhuru wa vyombo vya habari”.
Mnaona mapungufu ya sheria ya hifadhi ya ngorongoro (1975) hamuoni mapungufu ya katiba (1977) iliyopo hata sasa

Afadhali umemuulizaIs that the end of your thinking capacity? Hayo matatizo ya Ngorongoro yameanza jana?
Kumbuka pia hawalimi hao mkuu wanakula nini yaaani watu ni wabishi tu lakini hao watu hawapaswi kuishi ndani ya hifadhi!!Masai watatoka tu mle... it's a matter of time. Ni ajabu watanzania kuleta siasa kwenye mambo ya msingi. Binadamu ni mharibifu Sana, hawezi ishi kwenye hifadhi na ukategemea mazingira kutunzwa. Jiulize wanatoa wapi kuni za kupikia?
Au labda huwa familia zinalipwa allowance fulani ndani ya mbuga ndiyo maana hawataki kuhama?Kumbuka pia hawalimi hao mkuu wanakula nini yaaani watu ni wabishi tu lakini hao watu hawapaswi kuishi ndani ya hifadhi!!
Labda mkuu, nahisi ni kuzitumia bila utaratibu maliasilia zilizopo maana kung'ang'ania huko si bureAu labda huwa familia zinalipwa allowance fulani ndani ya mbuga ndiyo maana hawataki kuhama?
Bangi ni tatizo kubwa sana kwako. Watu wanazidi kuzaliana mle, baada ya miaka 50 ijayo, itakuwa siyo hifadhi tena, utakuwa ni mjiWaache siasa, Ngorongoro inataka kuporwa na Chui jike na mawakala wake.