Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Wabunge wote waelezwe kinachoendelea Ngorongoro

Wamekutwa mule si busara kusema Ngorongoro ni ya wote waondolewe tu kwakuwa sio kwenu wala huhusiki?
 
Hao wamasai wa zamani, wa siku hizi wanakula chips
 
Umeandika kwa kuwasifia masai kana kwamba ni watu wenye akili kwelikweli kumbe nusu ng'ombe tu nyie
 
Kunatakiwa uwiano mzuri kati ya wanyama na binadamu
Binadamu wanazidi kuongezeka zaidi ya wanyama. Miaka ijayo hakutakuwa na wanyama
 
Naam idadi fulani ya Wamaasai (au kitu chochote) sio adui..., ila tatizo ni numbers zikiwa tofauti na sustainability ya ecosystem fulani...

Je unadhani hizo big numbers kwa eneo hilo ni sustainable ? au kama vipi wasambazwe wawe wachache wachache kila mbuga na pawe na population cap..., wakizidi sana waanze kuhamishiwa mitaani wawe majirani zetu...., nadhani wote tungependa kuishi Masaki au Oysterbay au Msasani ila swali linakuja je wote tutatosha pale ? (huku mtaani gharama itakufanya mwenyewe usiende kule; Je kinachowakataza wahamiaji zaidi kuamia kule ni nini)?
 
Nakubaliana wamasaai waondolewe Ngorongoro. Leo ukienda kule hifadhini utashangaa wanyama wa kufugwa wanavyozidi kuongezeka kuwazidi wanyama wa asilia. Ngorongoro ni eneo la hifadhi ya Dunia, lazima itunzwe kwa gharama yoyote. Period!!
 
Kunatakiwa uwiano mzuri kati ya wanyama na binadamu
Binadamu wanazidi kuongezeka zaidi ya wanyama. Miaka ijayo hakutakuwa na wanyama

..inawezekana idadi ya mifugo imezidi.

..lakini nasikia 1982 Danida walifanya utafiti wakabaini mifugo imepungua sana na Wamaasai wamefanywa masikini tangu wahamishiwe Ngorongoro.

..labda hiyo ripoti imepitwa na wakati.
 
mnawafukuza wamasaai toka Ngorongoro na loliondo ambayo ni maeneo yao ya asili waende wapi? mmeisha waandalia sehem ya kwenda? hayoo mahifadhi na mambuga yenu yamewakuta wamaasai apo sasa sijui mnatakaje, waueni sasa mioyo yenu ilizikee
Tulia wewe masaai uamuzi wowote utakaofikiwa ni kwa masilahi mapana ya taifa na vizazi vijavyo. Punguza mihemko usije ukakosea
 
Ili awakomoe mataga na sukuma gang eti ee?

[emoji23][emoji23][emoji23]Na bado
Ukisema na bado ukimaanisha nini? Hiyo ni vita yenu wenyewe kwa wenyewe, yanipasani mimi? Hao wamasai wa Ngorongoro hawajawai chagua upinzani maisha yao yote.

Hiyo ni mbwa mwitu wanakulana wenyewe kwa wenyewe na shauri yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…