Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Wabunge wote waelezwe kinachoendelea Ngorongoro

Masai watatoka tu mle... it's a matter of time. Ni ajabu watanzania kuleta siasa kwenye mambo ya msingi. Binadamu ni mharibifu Sana, hawezi ishi kwenye hifadhi na ukategemea mazingira kutunzwa. Jiulize wanatoa wapi kuni za kupikia?
 
Wamasai na wanyama nasikia wameishi pamoja kwa miaka mingi sana na inasemekana ilikuwa ni moja ya vivutio vya watalii wengi kuona wanyama na binadamu wakiishi pamaja.. Mimi nafikiri tatizo lililopo kuna watu wanataka kunimilimisha hiyo hifadhi kwa kutaka kujenga mahoteli mengi na kualibu miundo mbinu ya hifadhi. Sasa wanaona wanapata upinzani kutoka kwa wamasai ndio matatizo haya tunayoyaona. Siasa imeliingilia
 
Kwani kuna hifadhi ambayo watu wanaishi hifadhini zaidi ya ngorongoro.
 
Huwezi tenganisha hifadhi na watalii sasa wakija wafikie wapi kama sio kwenye mahoteli pia hayo mahoteli yameajiri watanzania wengi sana sasa hao wamasai wameajiri nani achunge hao ng'ombe hayo ni maeneo ya kitalii.
 
Mkuu umeongea vyema nnachokiona ukiwa makini na wanayoyaongea watawala utagudua Ni ama kunakitu hakipo sawa, au kunamtu anawashinikiza kufanya maamzi, Sasa hebu twende tu kwenye maana ya utalii,

Huhitaji elim kubwa kujua kuwa kuishi na mnyama ambae si wa kufugwa Tena polini na mkawa marafiki, huo tu Ni utalii tosha, wazungu wanasafri mamia kwa mamia kuja kujifunza hw come mtu aishi na wanyama mama Simba, chui, tembo n.k na bado wakawa marafiki??

Harafu kunajambo hawalisemi mmasai Hali hao wanyama wa pori(nipo tayari kukumbushwa) maana Ni marafiki, Sasa unajiuliza huo utalii wanaotaka kuwaondoa hao ndugu wanautafsr vp??

Niwe mkwel tu hapa ingekuwa jpm Sasa yupo hai hlo Jambo lisingefanyika, ila kwa Sasa litafanyika maana Ni kama mtu amezima umeme sehem 1 kwa makusudi kuwa na giza ili afanye yake, akimaliza anawasha umeme..
 
Siku ya machifu Tanzania ndoimeleta yote haya, ndo mana wanngorongoro wana viburi kweli
 
Huwezi tenganisha hifadhi na watalii sasa wakija wafikie wapi kama sio kwenye mahoteli pia hayo mahoteli yameajiri watanzania wengi sana sasa hao wamasai wameajiri nani achunge hao ng'ombe hayo ni maeneo ya kitalii.

..hoteli zinatakiwa zijengwe maeneo ambayo hayataathiri mazingira, uasili, na uhai, wa Ngorongoro.

..kipaumbele ni kuilinda Ngorongoro kwani ikiharibika hakutakuwa na watalii, mapato kwa taifa, malisho kwa wafugaji, na ajira kwa wananchi.

..mwaka 93/94 Patrick Qorro mbunge wa Karatu aliwasilisha hoja binafsi bungeni kukemea uharibifu wa mazingira ambao usipothibitiwa utaua mbuga zetu za wanyama. Wakati huo tulikuwa na Waziri wa Utalii asiyejali kabisa mazingira ya vyanzo vyetu vya utalii.
 

..acha makasiriko na ujinga mwingi..
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iandae semina kwa wabunge wote ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu yanayoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro.
Hivi ndivyo heading ya huu uzi ilitakiwa iwe, walioagizwa ni Wizara na siyo wabunge
 
Kaziiendelee Tanzania
 
Mnaona mapungufu ya sheria ya hifadhi ya ngorongoro (1975) hamuoni mapungufu ya katiba (1977) iliyopo hata sasa
 
Masai watatoka tu mle... it's a matter of time. Ni ajabu watanzania kuleta siasa kwenye mambo ya msingi. Binadamu ni mharibifu Sana, hawezi ishi kwenye hifadhi na ukategemea mazingira kutunzwa. Jiulize wanatoa wapi kuni za kupikia?
Kumbuka pia hawalimi hao mkuu wanakula nini yaaani watu ni wabishi tu lakini hao watu hawapaswi kuishi ndani ya hifadhi!!
 
Kumbuka pia hawalimi hao mkuu wanakula nini yaaani watu ni wabishi tu lakini hao watu hawapaswi kuishi ndani ya hifadhi!!
Au labda huwa familia zinalipwa allowance fulani ndani ya mbuga ndiyo maana hawataki kuhama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…