Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Wanabodi najua kabisa tupo kwenye msiba mkubwa. Msiba ambao umemgusa kila mtu na mpaka sasa kila Mwananchi haamini kilichotokea.
Lakini yapata kama wiki moja iliyopita taifa zima lilikumbwa na taharuki kubwa. Kila raia mwenye mapenzi na mkuu wa nchi yetu alitaka kujua kama anaumwa au haumwi. Wapo waliojitolea kuwa wapiga mbiu. Wao walisema kuwa Rais anaumwa na yupo hoi
Ghafla akaibuka Waziri mkuu akiwa ziarani huko nyanda za juu kusini. Alitoa tamko ambalo sababu yeye ndio msimazi wa shughuli za serikali kila mwananchi alimuamini. Aliwahakikishia watanzania kuwa Rais haumwi na anachapa kazi kama kawaida.
Tamko la Waziri mkuu kuwa Rais alikuwa mzima linakinzana na taarifa tuliyopewa na Makamu wa Rais kuwa tangu tar 6 Macih Rais amekuwa mgonjwa tena aliyekuwa amelazwa.
Je, kwa hali ya kawaida kuna raia ambae bado anaweza kumuamini Waziri Mkuu tena?