Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Kipindi cha kuugua kwake tungepewa taarifa mapema na tungefanya maombi kila mtu na imani yake labda Mungu Mwenyezi angesikia juu ya vilio vyetu watanzania. Lakini ikawa ni siri, haya ndio tunasema mficha maradhi kifo humuumbua
 
Kwenye taarifa ya VP alisema Rais aliruhusiwa kutoka hospital trh 7 na aliendelea na kazi zake kabla ya kuzidiwa tena, Kwa hiyo PM alikuwa correct aliposema kuwa Rais anachapa kazi zake hakudanganya wakuu unless kama tulichopewa kwenye taarifa siyo sahihi lkn kama ndivyo PM alisema kweli
Angalia clip ipon U tube, utajiona mjinga kutetea ujinga
 
For security purposes state ya ugonjwa wa Rais inakuwa confidential saa nyingine hata Waziri Mkuu sio lazima ajue au aliongelee and especially kwa nchi kama hii ya Tanzania ambayo kila kitu kila saa ni siasa tu
 
Si umeambiwa tarehe 7 aliruhusiwa kurudi nyumbani kisha alirudishwa hospitali tarehe 13?
 
Wakati tukiendelea na maombelezo ya kuondokewa na kiongozi wetu, ni muhimu pia kutafakari kwanini hatukufahamishwa rasmi juu ya kuugua kwake hadi kupelekewa kifo chake.

Maoni ya wananchi wengi juu ya msiba huu wa taifa yanaambatana na lawama kwa viongozi wa serikali kutokulifahamisha taifa juu ya kuugua kwa Rais wao.

Wanasema endapo wangejulishwa, wangemuomba Mungu amnusuru na maradhi yaliyopelekea kulazwa na hatimae kufariki na huenda Mungu angepokea maombi hayo au angalau angempa nafuu kidogo ya kuweza kutoa kauli ya kuwaaga. Zaidi waanalaumu kwamba serikali haikumtendea haki Marehemu ya kuombewa na wananchi wake aliokuwa akiwatumikia ikizingatiwa kuwa marehemu katika uhai wake alikuwa akiwaomba wananchi wamuombee kheri kwa Mungu.

Kwa mtazamo wangu juu ya jambo hili naamini serikali ilizingatia ule msemo "heri lawama kuliko fedheha" na kwahiyo ililazimika kuchagua LAWAMA badala ya FEDHEHA.

Kudhihirisha kwamba Rais ni mgonjwa ni jambo la fedheha/aibu hasa ikizingatiwa ukweli kuwa kuugua kwakwe kumetokea wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa korona ambao yeye na serikali yake wamekuwa wakikaidi kuonesha uwepo wake hapa nchini hata wakakwepa kuutambua kwa jina lake na badala yake kuubatiza jina la "changamoto ya upumuaji". Lakini kwakuwa tayari ilishaaminika na wanchi kuwa hiyo "changamoto ya upumuaji" inaambukiza na kusababisha watu kuugua au kufa kama korona na kwamba ikiwa changamoto hiyo tayari imeua wasaidizi wa karibu wa Rais, basi kivyovyote vile Rais hasingeweza kusalimika hasa ikizingatiwa kuwa hakuwa anachukuwa tahadhari yoyote kujikinga na maambukizi hayo.

Hakuna ubisha kuwa Rais alikuwa mkaidi kupindukia na ukaidi huo ulitokana na kupenda sifa aonekana yeye ni "MWAMBA" na hatishwi na chochote hata kile kinachoitwa "korona". Lakini pia alifanya hivyo ili aonekana yeye ni mchamungu na kwamba Mungu angemlinda na maradhi hayo.

Kwa misingi hii ni heri kwa Rais na seririkali wabebe LAWAMA hizi za wananchi kwa kuficha ukweli kuliko FEDHEHA ya kutangaza kuugua kwani kivyovyote vile ingeaminika kuwa maradhi hayo ameambukizwa na wasaidizi wake kutokana na ukaidi wake na kwamba korona ni mshindi dhidi ya misimamo ya serikali.

Ni hivyo tu.
 
Ingekuwa kwa wenzetu wanao heshimu kiapo chao cha kazi na kuilinda na kuiheshimu katiba tangu jana saa 12 angeshajizulu.
 
Back
Top Bottom