Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Mtateseka sana, Tanga walipewa na salamu za Mhe Rais, eti mmesahau!! machadema mnahangaika sana, mjue hapa ni nyundo juu ya nyundo, kwanza mtuache kidogo bado tunaomboleza nyie mnawaza vyeo hovyo kabisa nyie!
Poleni sana wasakatonge,walamba viatu kwa msiba mzito kwenu.
 
Waliogopa. Maana mzee asingependa endapo angepona halafu akute walitangaza anaumwa.



Uoga to such extent?

Inashangaza kama ni hivyo!

Sasa kwanini asingependa wakati ni kiongozi mkuu wa Taifa hili?
 
Uoga to such extent?

Inashangaza kama ni hivyo!

Sasa kwanini asingependa wakati ni kiongozi mkuu wa Taifa hili?
Magufuli maisha yake na family ni siri yake. Ndo maana hata kina Jesca hawapo social media yeyote ile. Watoto wengi wameonekana public kwenye kipindi hiki cha msiba.
 
Hamna lolote! Mnataka kufuta footmark za JPM kwa kumpunguzia mama Samia wasaidizi.....aides

Tunasisitiza big No kwa wanamtandao
 
Wanabodi najua kabisa tupo kwenye msiba mkubwa. Msiba ambao umemgusa kila mtu na mpaka sasa kila Mwananchi haamini kilichotokea.

Lakini yapata kama wiki moja iliyopita taifa zima lilikumbwa na taharuki kubwa. Kila raia mwenye mapenzi na mkuu wa nchi yetu alitaka kujua kama anaumwa au haumwi. Wapo waliojitolea kuwa wapiga mbiu. Wao walisema kuwa Rais anaumwa na yupo hoi

Ghafla akaibuka Waziri mkuu akiwa ziarani huko nyanda za juu kusini. Alitoa tamko ambalo sababu yeye ndio msimazi wa shughuli za serikali kila mwananchi alimuamini. Aliwahakikishia watanzania kuwa Rais haumwi na anachapa kazi kama kawaida.

Tamko la Waziri mkuu kuwa Rais alikuwa mzima linakinzana na taarifa tuliyopewa na Makamu wa Rais kuwa tangu tar 6 Macih Rais amekuwa mgonjwa tena aliyekuwa amelazwa.

Je, kwa hali ya kawaida kuna raia ambae bado anaweza kumuamini Waziri Mkuu tena?
Kudanganya ni kosa la jinai.
 
Back
Top Bottom