Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea nae kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli?. Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salam.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.




Mimi nashauri Majaliwa asipewe cheo zaidi ya hapa amekuwa kinara wa uongo na mnafiki
 
Ameidharirisha kada ya wavaa sendo[emoji14][emoji14][emoji14][emoji14][emoji14]
 
Mpaka sasa hivi kwa kiongozi mwenye ethics na anayejali heshima yake
Prime Minister, mwigulu nchemba na Albert chalamila walitakiwa wawe wameshamuandikia Madam President mama Samia barua za ku jiuzulu nyadhifa zao zote. Ili kulinda heshima zao na kwa manufaa ya nchi
Period
 
Freedom of speech and transparency hazijawahi kuwa acts of war..... Kule hta Rais wao anachambuliwa nje ndani na media ndio sembuse Rais wa nchi nyingine?
Wewe siyo professional journalist na Wala hujui Mambo ya international relations...hujui kitu...na hujui the concept of war and its sources or causes...hujui kitu..umekalia ushabiki tu...hujui hata maana ya freedom of speech...bill Shaka kama baba akifa na kuanza kuandikwa na kusemwa kwa mabaya utabariki kwa kigezo Cha freedom of speech and transparency...
 
Watu ni waongo sana.
watu hawamuogopi Mungu wao
wansema uongo Mchana kweupe
tena kwenye nyumba za Ibada!
Hivi hapo alipo anajisikiaje?
Aibu?
Sioni Majaliwa akifaa tena kuaminiwa na kupewa nafasi ya uongozi amejiwekea dosari kubwa!
Kitu kidogo tu kinakuondolea heshima na jina ulilotumia miaka kulijenga!
Jamii ilimuamini sana aende akatubu na aombe msamaha katika huo huo msikiti wa Njombe.
Hawa ndiyo viongozi tulio nao!
Bado tuna safari ndefu sana kama Taifa
Hakuna ambaye ni afadhali!
ww ulitaka asemeje kwa mfano?
 
Ila mimi Majaliwa sina imani naye kupewa majukumu ya kuongoza UMMA kama PM,VP kwasababu mnafiki!

Muhammad S.A.W alisema..

"Mnafiki ana tabia tatu, akiongea husema uongo, akiaminiwa hufanya hiyana"..... na sifa nyingine nimesahau
 
Mwanasiasa hata akikwambia Ni usiku usiamwamini ,toka nje angalia Kama kweli Ni usiku...manake anaweza akasema good morning hata Kama Ni saa sita mchana.[emoji850][emoji124][emoji2506][emoji41]
 
Rais John Joseph Pombe Magufuli piga kazi kuwaletea na kuwajengea misingi imara ya kimaendeleo Watanzania nilichogundua Watanzania wanampenda sana Rais wao kiasi cha kutokumuona wala kumsikia ndani ya wiki kila mmoja amekuwa hana raha kwa kuwa wameshazoea kumsikia akiwapa maagizo wateule wake na kutatua kero za wananchi.

Kwa dalili hizi ni kipimo cha mapenzi kilichopitiliza najua wenye account fake wakiwa peke yao au kwenye vikao vyao wanazungumzia muziki mnene wa mtetezi wa wanyonge.

Tuendelee kumuombea kwa Mungu raisi wetu azidi kuwa na afya njema na amuepushe na wenye husuda na roho mbaya ili aweze kutekeleza yale yote aliyo ahidi kipindi cha kampeni kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Raisi wetu wananchi wamekumiss na wanakupenda sana muda utakaonekana ama hakika watashangilia kama kumefungwa goli uwanja wa taifa!

Hapa kazi tu, tusisahau kufuata muongozo wa wataalamu wa afya Covid19 ipo!
jamaa yangu ulikua unahisi kitu gani moyon mwako kilichokupelekea kuyaandika haya
 
Ipo wapi na je mtu binafsi anaruhusiwa kutibiwa hapo?
Nimesikia wanatibiwa viongozi wa juu tu na wana TISS pamoja na familia zao tu.

Sisi wanyonge tutabanana Muhimbili na Hospital zingine za kawaida
 
Ila mimi Majaliwa sina imani naye kupewa majukumu ya kuongoza UMMA kama PM,VP kwasababu mnafiki!

Muhammad S.A.W alisema..

"Mnafiki ana tabia tatu, akiongea husema uongo, akiaminiwa hufanya hiyana"..... na sifa nyingine nimesahau

Ya 3 ni anapoeka ahadi haitimizi[emoji1688]
 
Marehemu alikuwa akisema kwerkwer
Unamtukana mwenzako kwa maoni yake tu binafsi tu. Sasa ukweli uko wazi, unakukodolea macho mbele yako...

Mpaka hapo nani mjinga? Obviously, ni wewe. Au siyo?

Aah bwana, kubali tu mshkaji maana huo ndio ustaarabu na uungwana. Ni kwa faida yako kukiri kosa na kuomba msamaha. Faida haiko kwa umwombae msamaha....

Yupo anaendelea kuchapa kazi siyo?. Okay. Hata kaburini zipo kazi. Anachapa kazi kweli kweli...!!
 
Back
Top Bottom