Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Kama rais ni mzima, kwa nini inakuwa mgogoro mkubwa sana kwa watu wa serikali kumuonesha huyu hapa Magufuli mzima wamalize uvumi kwamba ni mgonjwa?

Wanasubiri nini kufanya hivyo? Wanasubiri msaada wa wahisani?
Kwa hiyo wafanye hivyo kwa sababu mitandaoni watu wanasema haya!?
 
Ila kwa uhalisia kama Rais angekuwa katika hali kama hiyo inayosemwa ni dhahiri kungekuwa na taharuki na isingewezekana kamwe kwa waziri Mkuu kuendelea na ziara kama hizo.

I BET THE PRESIDENT IS FULLY FIT AND FINE
Unaamini hayo maigizo .... Inawezekana hayuko hoi kama inavyosemwa lakini kwa kutumia akili tu ya kawaida, something is not right. Imagine hata akiwa Chato kwenye mapumziko huwa hazipiti siku mbili hajaonekana, iweje leo anapiga week 3 bila kuonekana.
 
Hapo ndipo uwezo wako ulipoishia.

Nakupeleka ignore list sina muda wa kujishusha kumtukana guluguja ngumbaru asiye na ubongo wala uti wa mgongo.

Kuanzia hapa sitaona post yako yoyote.
Mazee...mi wala huwa siwaambii. Nagonga ignore tu halafu naendelea na mengine.
 
Unaamini hayo maigizo .... Inawezekana hayuko hoi kama inavyosemwa lakini kwa kutumia akili tu ya kawaida, something is not right. Imagine hata akiwa Chato kwenye mapumziko huwa hazipiti siku mbili hajaonekana, iweje leo anapiga week 3 bila kuonekana.
Mkuu ushaambiwa raisi yupo ni mzima na anaendelea na majukumu. Ukikubaliana na waziri mkuu wa nchi yako utapoteza nn? Angekuambia raisi ni mgonjwa yu mahututi hapo usingebisha na ungesambaza habari kwa kumtumia yeye kama reference, ni vile amesema usilotaka kusikia.
 
Hivi nyinyi mnao mbishia hata Waziri mkuu mna lengo gani?


Ikulu ni nyumba ya Watanzania hivi kuna ugumu gani kwa wiki mbili raisi kushidwa kutoka pale pale ikulu na kusema achaneni na uzushi. Watanzania wamekuwa hivi baada ya kudanganya sana kwenye Corona. Hii ni serikali ya kudanganya watu ! wakati vitu vinaonekana. Unasema waziri mkuu hata Raisi mwenyewe kadanganya watu kuhusu uchaguzi na Corona Watanzania sio wajinga. Mbona Kikwete watu walikuwa hawana hizi kutokufahamu ni muhula huu tu! ni kwasababu ya tabia ya kuwa waongo na Watanzania wengi wanajua hilo. Msinshangae kuona mpaka makanisa sasa yamejitenga kwa kuogopa kuhusishwa na uongo.
 
Asante Majaliwa; majibu yako ni kuwa Rais ni mzima wa afya na anaendelea na kazi zake. Mnafanya makosa kuacha habari hizi ziwe zinatokea kila baada ya muda fulani. S

Sijui kwanini.... inawezekana ni security operation mnaifanya lakini hamlitendei taifa haki. Nashukuru swali langu la juzi limejibiwa na maisha yanasonga mbele.

Lakini bila Rais mwenyewe kuonekana ni wachache wataamini kauli yako (mimi si mmojawapo). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Watanzania!
 
Jambo jema kama ni mzima. Lakini mbona wameachia hizi romours kwa muda mrefu hivyo bila kuzikanusha kama hivi?
 
Wanasubiri apone kwanza?
Siku hizi hawana zile mbwembwe za kupigiana simu kwenye mikutano na bwana mkubwa kuwasabahi washiriki wa mkutano.

Nakumbuka siku za bwana mkubwa kwa makonda, humphrey polepole, clouds fm, mkutano wa waalimu, etc etc.

Hata simu ya dakika 3 kusabahi, imeshindikana?Ukimya huu wa bwana mkubwa unatia mashaka makubwa.

Nasubiri mpaka JUMAPILI tuone kama bwana mkubwa bado atakuwa busy.
 
Asante Majaliwa; majibu yako ni kuwa Rais ni mzima wa afya na anaendelea na kazi zake. Mnafanya makosa kuacha habari hizi ziwe zinatokea kila baada ya muda fulani. Sijui kwanini.... inawezekana ni security operation mnaifanya lakini hamlitendei taifa haki. Nashukuru swali langu la juzi limejibiwa na maisha yanasonga mbele. Lakini bila Rais mwenyewe kuonekana ni wachache wataamini kauli yako (mimi si mmojawapo). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Watanzania!
Mwanakijiji, unataka kila utokeapo huu uzushi/uvumi wawe wanajitokeza kutoa neno?
 
Back
Top Bottom