Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Rais Magufuli kama yu mzima wa afya njema, ni jambo jema. Hata kama tukitofautiana kifikra, kimatazamo au kiitikadi, siyo sababu ya kufurahia au kutaka mwenzio asiwepo Duniani.

Hatutaki Polisi waue raia, hatutaki wasiojulikana waue, wapoteze au wateke watu wanaoikosoa Serikali au viongozi kwa sababu tunataka kila mmoja aishi mpaka pale ambapo hatuna uwezo wa kuzuia kuondoka kwake Duniani. Hata mmoja wetu anapoondoka, tunasikitika na kuomboleza.

Kama hatutaki mtu mwingine yeyote aondoke Duniani, nina hakika kila mwanadamu mwenye mapenzi mema na binadamu wenzake, hawezi kufurahia kifo cha Rais Magufuli au kutaka Rais Magufuli afariki.

Mimi siyo shabiki wa Rais Magufuli wala CCM, lakini simchukii Rais Magufuli wala mwanaCCM yeyote, bali nayachukia matendo ninayoamini siyo ya haki. Uchaguzi wa mwakajana uliudhi kila anayelitakia mema Taifa hili, lakini hiyo siyo sababu ya kumtakia kifo yeyote. Uchaguzi wa 2020 ulikuwa hovyo kabisa, na kwa hilo Rais Magufuli hakulitendea haki Taifa letu.

Lakini kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, nathubutu kusema, Rais Magufuli kuna mema mengi aliyoyafanya, na kuna baadhi ya makosa ameyafanya kwa sababu ya kuwa too ambitious katika kuitaka Tanzania ipate maendeleo ya ghafla. Siku Magufuli akiondoka Duniani, tukaja kuambiwa kila alilolifanya na maisha yake kwa ujumla, wengi tunaweza kushtushwa na ukweli, na tukamlilia wakati hayupo.

Kuna mambo ambayo, nadhani hayabishaniwi:

1) Magufuli angependa Tanzania iwe na maendeleo makubwa kwa muda mfupi, na kwa sababu ya dhamira hiyo kuna wakati amefanya makosa, ambalo siyo jambo la ajabu.

2) Mimi siamini kama Magufuli ni tajiri au mtu aliyejilimbikizia mali kupitia uongozi japo sifurahishwi na kila kitu kupelekwa Chato. Naambiwa anamiliki hoteli kule Chato, lakini hicho siyo kitu cha ajabu, na amejenga kabla ya kuwa Rais. Hata wabunge wana mahoteli.

3) Kuna wateule wake wengine wamefanya mambo mengi ya ajabu ajabu kwa kutaka kumfurahisha Rais, na yote anabebeshwa yeye, na huenda hakuwaagiza.

Mazuri mengi aliyoyafanya Magufuli, na ambayo tunaweza kuyathamini kwa sasa, mpaka yaondoke ni pamoja na:

1) Kutokomeza/kupunguza ujambazi. Hapo nyuma majambazi walitamba sana na ilikuwa kawaida sana kysikia vifo vilivyosababishwa na majambazi

2) Nidhamu ya wafanyakazi wa umma.

3) Ujenzi wa miundombinu msingi

4) Maamuzi ya haraka, hata kama kuna wakati yanakuwa na makosa.

Kubwa kabisa baya ambalo nililisemea sana ni kuruhusu wasiojulikana waue, washambulie, wateke na kupoteza watu. Hilo nililiona ni baya kuliko yote. Mengine yanavumilika, na wala hatumtegemei kutokosea maana naye ni mwanadamu. Ninachoshukuru, matukio hayo kwa sasa yamekoma, na tunaomba hali iendelee hivyo hivyo. Tubishane na kukosoana kwa hoja, na siyo kutekana au kuuana.

Lakini pamoja na yote hayo, tumtakie afya njema na maisha marefu Rais Magufuli. Mimi ni kati ya watu ambao , kwa yale mema aliyoyafanya, kwa kuzingatia ubinadamu wetu, nitahuzunika sana kama Rais Magufuli akitangulia mbele za haki. Tutaendelea kumkosoa pale tunapoona amekosea ili ikiwezekana arekebishe. Tutaendelea kusema kuwa uchaguzi wa 2020 aliuharibu, na kumtaka kuhakikisha hilo halitokei tena, ila kumtakia kifo HAPANA. Kama mimi nitamtakia kifo mwanadamu mwanzangu, nitakuwa na tofauti gani na wale wasiojulikana ambao wanafurahia kuua, kuteka na kupoteza watu?

Popote alipo, awe ana afya njema au anaumwa, Rais Magufuli namwombea afya njema na maisha marefu. Arudi kazini, atafakari maeneo uliyofanya vizuri ili ayaendeleze, alipokosea ajisahihishe na kujirekebisha, asikilize mawazo ya watu, anaweza kuyapokea au kuyakataa, lakini siyo kutumia vyombo vya dola kuwadhibiti wenye mawazo tofauti. Aoneshe mfano wa uvumilivu, usikivu, kujirekebisha, lakini asiwe legevu kwenye mambo ambayo anaamini ni sahihi ja ya msingi alimradi hamwonei wala kumpendelea mtu au kikundi fulani.
 
Eeeenh, Heeee.

Ninakuamini sana Mh Majaliwa.

Kwa mtu asiyejua kusema uongo ni vigumu sana kuutunga uongo na kuunyoosha uonekane ndio ukweli pekee.

Umejitahidi sana, lakini kwa vile si hulka yako, sio rahisi kuongopa.

Yaani jamaa kazungushazungusha maneno; lakini wapi, bado ikawa vigumu kuyanyoosha watu wayaamini.

Pole sana Majaliwa. Hizi kazi, ni basi tu, utafanyaje!
 
Shoka moja mbuyu chini.

Maswali yalikuwa mengi kuanzia hapa nyumbani, Ubelgiji hadi Canada kwa Lema wote wakihoji alipo Rais Magufuli baada ya kuwa wamemmis sana.

Leo saa 5 na dakika kadhaa Katibu mkuu wa CHADEMA mh J J Mnyika alihoji alipo Rais Magufuli kwa niaba ya kambi ya upinzani.

Na mnamo saa 6 na ushee Waziri mkuu mh Majaliwa alisema Rais Magufuli yupo anaendelea na kazi zake kama kawaida.

Kwa maana hiyo mjadala huu naomba ufungwe na kila mtu akaendelee kuchapa kazi kwani majungu siyo mtaji.

Maendeleo hayana vyama!
 
2019 walizikanusha?
Kama nakumbuka vema alijitokeza mwenyewe. Lakini pia haikuwa muda mrefu hivi. Za Dr Mpango majuzi walikanusha na press juu.

Ila pia tusiwalaumu sana kina Majaliwa. Kama nao kwa sababu fulani walikuwa hawajui kwa uhakika hali na alipo Rais, wasingeweza kukanusha.
 
Sasa serikali hapa ndio wanaonyesha kupoteana, ilitakiwa kama waliamua kukaa kimya basi wangekaa kimya wala wasishindane na watu wa mitandaoni.

Ila kwa hili la kuanza kumjibia Mh. Rais watu wataanza kuunganisha doti. Cha msingi waendelee kukaka kimya huku wakitimiza majukumu yao ya kila siku.
Hapo Majaliwa kaingizwa cha kike....!!
Bado kuna maswali mengi kuliko majibu. Kwa kawaida ya Jiwe kama yuko live and physically fit LAZIMA ANGELIMTWANGIA SIMU MAJALIWA NA KUONGEA NA WANA NJOMBE....!!!
Bado hii ni janjajanja tu ya kujaribu ku-buy time ili akae sawa!!!
 
Ndio maana yake, sote hapa tumecheza kamari, wanaombea apone tusutwe, twaombea aende tuwasute kwa kutuficha ukweli
Mimi hata siangalii hili jambo kama la kusutana.

Ninaliangalia hivi.

1. Katiba ya Tanzania inasema wananchi wana haki ya kupewa habari za muhimu kuhusu maendeleo ya nchi.

2. Afya ya rais inahusika kwenye mustakabali wa nchi na ni habari ya muhimu, wananchi wana haki ya kupewa habari kuhusu afya ya rais.
3.Rais kukaa wiki mbili hajulikani alipo ni suala kubwa.

4. Hata Magufuli akitokea leo na kufanya mkutano kusema yuko hai na ana afya, rais kukaa wiki mbili haonekani si habari nzuri, hivyo, waliotaka rais ajitokeze wako justified, hawana cha kusutwa.

Can you imagine rais kafariki kwa wiki mbili watu wameficha habari wanafoji nyaraka kwa saini yake wanaiba hela na kutorosha nje ya nchi?
 
Ahsanteni sana Studio. Kama mliweza kumtoa Dr. Ma-Plan kuudhihirishia Umma kuwa ni mzima........na huyu nae atoke hadharani.....Why kumnenea?

Mungu akupe maisha marefu mpendwa rais wangu
 
Kama nakumbuka vema alijitokeza mwenyewe. Lakini pia haikuwa muda mrefu hivi. Za Dr Mpango majuzi walikanusha na press juu.

Ila pia tusiwalaumu sana kina Majaliwa. Kama nao kwa sababu fulani walikuwa hawajui kwa uhakika hali na alipo Rais, wasingeweza kukanusha.
Na ule uvumi wa Mwamunyange je?
 
Rais Magufuli kama yu mzima wa afya njema, ni jambo jema. Hata kama tukitofautiana kifikra, kimatazamo au kiitikadi, siyo sababu ya kufurahia au kutaka mwenzio asiwepo Duniani...
Kwangu mimi failure kubwa ya JPM so far ni kushindwa kutengeneza mfumo utakaotusaidia hata kama yeye hayupo. Kila kitu ni yeye. Unaona hata matatizo madogo madogo tu ya Ardhi, mpaka yanafikishwa kwa Rais.

Atuwekee mfumo katika nchi ili hata kama yeye hayupo, basi nchi iendeleze yale mazuri aliyoacha. Nina wasiwasi sana akiondoka yeye, tutarudi nyuma kwenye masuala kadhaa ambayo amefanikiwa kuyafanya.
 
Back
Top Bottom