Waziri Mkuu: Mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora Serikali iyauze kuliko kuyaacha yakiozea pale yard

Waziri Mkuu: Mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora Serikali iyauze kuliko kuyaacha yakiozea pale yard

Kwa namna yanavyopigishwa kazi, magari hayo yangekuwa yanauzwa kila baada ya miaka miwili wakati bado yanauzika. Tatizo ni utaratibu wa kuuza mali za umma una ukiritimba sana. Na nani atakae yanunua? Ubaya mwingine utakuta hayana bima, kwa hiyo yakipata ajali inakula kwa serikali.

Pengine ingekuwa bora kama wange yakodi kutoka muuzaji kwa makubaliano kuwa kila baada ya miaka kadhaa wanamrudishia na wanapewa mapya. Muuzaji angeweza kuyatengeneza na kuwauzia wengine. Na mpango wa lease unamwachia muuzaji jukumu la service na maintenance.

Amandla...
 
Waziri mkuu mh Majaliwa ameshauri mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora yauzwe kuliko kuyaacha yakioza pale yard

Waziri mkuu amesema hayo baada ya kushuhudia mabasi takribani 50 yakiwa yamelala kabisa kwa ubovu na yakizidi kuchakaa.

Source ITV habari

Ramadhan Kareem!
hata chuma chakavu hayafai
 
Mnataka mabasi yafanye kazi ya treni. Wenzao wanatengeneza "commuter train" wao bado wanapigana na diesel engine zisafirishe watu kwenye busy chaotic city kama dar. Mi nilishangaa sana huu mradi back in the days enzi za JK.
 
Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Mzee uko vizuri kwa extrapolation😆..!!
 
halafu magari hayo yalikuwa ni used, pili njia za bongo changamoto sana angalia maji jangwani pale!?

Mabasi ya mwendokasi yaliletwa toka mtumbani????!!! mmh
 
SGR imekufa hata kabla haijaanza.
ATCL ndege zilizopo haziruki huku tunaendelea kununua nyingine, sio moja. Tatu
Ndege moja tungenunua mabasi zaidi ya Mia mbili
Ile MV Bagamoyo iliyonunuliwa kwa Bei pouwer iko wapi?
We don't have priorities.
Mabasi ya kipuuzi yale bora wanunue yutong kama za mikoani tu zile 😛 walau watapiga hela au wanunue Hino za mjapani!
 
Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Wakati Kuna dcm za mbagala zipo tangu enzi ya mkapa
 
Back
Top Bottom