Waziri Mkuu: Mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora Serikali iyauze kuliko kuyaacha yakiozea pale yard

Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Vyema pia hata Kama ni mabovu pia kuyakagua kabla ya kuyauza, unaweza pia kuta yapo Kama mabox tu vipuli vilishachomolewa na kupigwa bei
 
Huyu PM sijawahi mkubali kama "uwezo mdogo" hivi kwa mujibu wa Profesa.

prof anakwambia wasomi nchi hii ni viazi unamwamini wakati nayeye ni miongoni mwao[emoji3][emoji3][emoji3].

huoni tatizo lipo kwako wewe sasa pia!!!
 
Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Sasa kama hawapewi pesa ya service na fedha inaingia kwa control number au pos pamoja na sheria mbovu ya manunuzi ambayo inawataka kutangaza tender hata service hata wewe ungeweza? angalia hata TTCL inachehemea kila mwaka shauri ya sheria mbovu ya manunuzi + TEMESA
 
nimetoka kuposti kuhusu haya mabasi muda si mrefu kwenye thread nyingine!

aliyeshauri serikali iweke ile hub pale, bila kuboresha miundombinu ya eneo lile, alikuwa na lake!
 
Mardi wa mwendokasi siyo mzuri kwa sababu ni barabara inayoruhusu kutumiwa na gari za kampuni (mmiliki) moja pekee. Suluhisho ni kuwa na Barbara zisizo na makutano (highway) ambapo kila gari huweza kuzitumia. Kimsingi, hakuna gari ya mwendohafifu. Zote ni za mwendokasi isipokuwa tatizo kuwa na njia duni.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa ameshauri mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora yauzwe kuliko kuyaacha yakioza pale yard

Waziri mkuu amesema hayo baada ya kushuhudia mabasi takriban 50 yakiwa yamelala kabisa kwa ubovu na yakizidi kuchakaa.

Chanzo: ITV habari

Ramadhan Kareem!
Let's be serious yale magari yametengenezwa China na kwa technology ya General Motors. Yako computerized so yanahitaji advanced maintenance skills. Kama Serikali imeshindwa kuyatumia kwa kuharibika, utamuuzia nani?

Magari yalikuwa designed kwa ajili ya Mwendokasi, ndiyo maana mlango wakushukia uko kulia kadri ya barabara za Mwendokasi. Anayenunua itamlazimu kuoperate kwenye barabara ya Mwendokasi ?

Au itabidi afanye modification ya milango?

Kama kawaida PM Majaliwa ni mtu wa KUKURUPUKA
 
Kilichouwa hayo mabasi ni hapo jangwani...wasipojenga daraja LA juu hapo jangwani hata washushee miujiza magari yatakufa tuuu.
Yale mabasi mengi ameathiriwa na maji ya pale jangwani.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa ameshauri mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora yauzwe kuliko kuyaacha yakioza pale yard

Waziri mkuu amesema hayo baada ya kushuhudia mabasi takriban 50 yakiwa yamelala kabisa kwa ubovu na yakizidi kuchakaa.

Chanzo: ITV habari

Ramadhan Kareem!
Kutokana na mahesabu ya miradi UDART za 2013, gharama ya tiketi ya Mbezi- Kivukoni - Mbezi (round trip) ilipaswa kuwa Tsh 3,000 au Tsh kwa saffari ya kwenda tu.

Hiyo ndiyo bei inayoweza kulipa ghharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na riba za Benki.

Mradi ulipoanza ulianza kwa Serikali kuingiza Siasa ndipo UDART wakaambiwa wa charge Tsh 1,300 kwa round trip au Tsh 650/= kwa trip ya kwenda tu.

Gharama kubwa sana ya kuendesha UDART iko kwenye Workshop (Karakana). Karakana siyo revenue centre kama yalivyo mabasi, instead yenyewe ni cost centre. Inakula tu na haizalishi.

Hiyo tofauti ya Tsh 3,000 ya kwenye upembuzi yakinifu na ile Tsh 1,300 ya Serikali ambayo imelazimisha ni Tsh 1,700.
Kwa hiyo kila abiria wa Mwendokasi anakokwenda Kariakoo na kurudi anatengeneza hasara ya Tsh 1,700.
Na hapo ndipo inaonekana mradi hauwezi kugomboa magari 70 ambayo yako TPA kuanzia mwaka 2019 yakisubiri yasamehewe Custom duty na Excise tax. Vile vile ndiyo chanzo cha kushindwa kununua magari mapya.

TUSITAFUTE MCHAWI, SERIKALI NDIYO CHANZO CHA KUDORORA KWA UDART
 
Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Tangu wachina wajitoe kwenye kuyatengeneza ndio hapo hapo yalifikia mwisho
 
Serikali inataka kuhamishia matatizo kwa wananchi wake wakope bank wanunue uchakavu huo...hapo vipuri ndio changamoto hapo wanaua gari moja kufufua lingine mngeweza mngewasiliana na makampuni yanayojitambua waweke engine na gear box hapo kwa hayo hayo mabodi yatafanya kazi acheni kulala...
 
Serikalini ni ngumu sana kufanya biashara.
Wasimamizi hawana uchungu na pesa ya umma.
Yule jamaa alituaminisha BORA APOTEE MTU LKN SIO PESA YA SERIKALI. Ajabu ndo ikapotea zaidi.
 
Kutokana na mahesabu ya miradi UDART za 2013, gharama ya tiketi ya Mbezi- Kivukoni - Mbezi (round trip) ilipaswa kuwa Tsh 3,000 au Tsh kwa saffari ya kwenda tu.

Hiyo ndiyo bei inayoweza kulipa ghharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na riba za Benki.

Mradi ulipoanza ulianza kwa Serikali kuingiza Siasa ndipo UDART wakaambiwa wa charge Tsh 1,300 kwa round trip au Tsh 650/= kwa trip ya kwenda tu.

Gharama kubwa sana ya kuendesha UDART iko kwenye Workshop (Karakana). Karakana siyo revenue centre kama yalivyo mabasi, instead yenyewe ni cost centre. Inakula tu na haizalishi.

Hiyo tofauti ya Tsh 3,000 ya kwenye upembuzi yakinifu na ile Tsh 1,300 ya Serikali ambayo imelazimisha ni Tsh 1,700.
Kwa hiyo kila abiria wa Mwendokasi anakokwenda Kariakoo na kurudi anatengeneza hasara ya Tsh 1,700.
Na hapo ndipo inaonekana mradi hauwezi kugomboa magari 70 ambayo yako TPA kuanzia mwaka 2019 yakisubiri yasamehewe Custom duty na Excise tax. Vile vile ndiyo chanzo cha kushindwa kununua magari mapya.

TUSITAFUTE MCHAWI, SERIKALI NDIYO CHANZO CHA KUDORORA KWA UDART
Usitetee kuna wizi wa tiketi pale zinapelekwa kwenye mabox wahunu tuu wale..
 
Uongozi wa mwendokasi unahitaji kusaidiwa
Wawekwe pembeni kidogo
Walioencourage privatization policy sio kwamba walikua vilaza hapana walifanya tathimini ya kina,taasis za serikali hakuna return on investment,ukosefu wa uwajibikaji wenye ufanisi sbb wanaamini hata ukipata hasara serikali itatoa ruzuku na mishahara watapata.Hata hii mindege mnayotetea hakuna ufanisi na usitarajie faida km itaendelea kuendeshwa na serikali kwa 100%.Tatizo Magufuli aliingia madarakan kwa mbwembwe akiamini wengine hawakua na akili kufufua baadhi ya mashirika,alikurupuka mwishowe taifa limepata hasara,vyovyote mtakavyomtetea lakin ameipa hasara nchi kwa kufanya maamuzi ya kukurupuka akiamini yeye ndo alikua na akili mingi kumbe maushuzi tupu
 
Back
Top Bottom