Waziri mkuu Majaliwa aagiza hospital ya Uhuru mjini Dodoma iwe imekamilika ndani ya siku 15 ili Rais Magufuli aifungue 09/12/2020

Waziri mkuu Majaliwa aagiza hospital ya Uhuru mjini Dodoma iwe imekamilika ndani ya siku 15 ili Rais Magufuli aifungue 09/12/2020

Kwa hiyo iharakishwe kukamilika ili Rais aizindue tarehe 9/December!

Hizo ni akili au matope?

Hospitali inapaswa kujengwa kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi na sio kufikia matamanio ya kuzinduliwa na mtawala ili kumpa sifa.

Serikali itoe pesa, wakandarasi wa uhakika wawepo kazini na wataalamu wapewe nafasi ya kufanya kazi zao pasipo kukimbizwa.
Hii hospitali imechelewa kukamilika kwa sababu serikali iliyopita ilikuwa ya awamu ya tano, serikali makini ya awamu ya sita itaikamilisha haraka ndani ya siku kumi na tano tu.
 
nashauri kipindi hiki waziri mkuu awe mkali zaidi kuliko kipindi kilicho pita, tena awe mkali kwelikweli, yaaani asimchekee mtu yeyote aliye vurunda, awe mkali kweli kweli, awe mkali
hakuna kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa yaaani awe mkali haswaaaa, hiki ni kipindi cha lala salama, kamwe asikubali uozo ktk kipindi hiki, awasimimie bila kuwatazama usoni....yaaani kazi kazi.
 
Back
Top Bottom