Haya ndio matunda ya five years of HAPA KAZI TU! Tukiwaambia tuna mabingwa wa utapeli wa kisiasa, mnabisha! Kama angekwenda mwenyewe kitu cha kwanza angeuliza mbunge wa eneo hilo ni nani. Akiambiwa ni wa Upinzani, basi anawatukana wananchi kuwa hawapati maendeleo kwa sababu walichagua vibaya - walichagua mpinzani. Akiambiwa ni m-CCM, basi anafanya political gimmicks zake kwa kumtumbua mkurugenzi ili kuonesha kuwa ni mchapa kazi na amekasirika!! Uchapa kazi ni kufuatilia kila mwaka kwa kutaka uletewe ripoti kupitia channels za kiutawala na kuchukua hatua kiutawala. Kwa sababu mkuu wa nchi hawezi kwenda kila jimbo au halmashauri kuona nani anafanya nini. Kuna channels za kiutawala. Hiki alichofanya huyu WM ni mtindo ule ule wa bosi wake, political gimmick, tofauti ni kwamba hana mamlaka ya kutumbua!!! Tunasubiri miaka mingine mitano ya maendeleo hayana chama!! HAPA KAZI TU