Waziri Mkuu Majaliwa, pokea makadirio yangu kibanda cha VETA Tabora

Haujaweka gharama za tiles, za vitasa na bawaba, ulinzi wakati kinajengwa .

Amandla...
Ni kweli mkuu, hii estimate niliifanya kwa haraka haraka.
Na kwa kweli nashangazwa kwa Waziri Mkuu kushangazwa na bei ya hili jengo.
Gharama ambayo kiuhalisia na kwa viwango vyake gharma iko chini.
 
Ni kweli unaweza kujenga kibanda kama hicho hata kwa milion 100, ila kwanini ujenge kwa gharama kubwa wakati inawezekana kujenga kwa gharama ndogo na kwa ubora mzuri tu
Ubora unaendana na mkataba sio matakwa ya mjenzi. Hapo hajaweka gharama za kupima matofali, zege na nondo. Na kila hatua ikaguliwe na kupitishwa. Ndivyo inavyotakiwa katika miradi ya serikali. Weww ulifanya lini vyote hivi kwenye kibanda ulichojenga?

Amandla...
 
Naomba maelezo ya gharama za hapo juu, hicho kibanda ndio kinatumia 650,000 kwenye electrical wiring na kikatumia 445,000 kwenye rangi?
Inategemea waya za aina gani, hivyo vifaa vya umeme vimetoka wapi na kama fundi aliyefunga anatambulika na mamlaka husika. Rangi vile vile.

Amandla...
 
Mamamake, nani alikwambia hivyo vyote waliviweka? Halafu hako kakibanda kawe na mabati 38? Utakuwa pumbavu wewe!
 
Naomba maelezo ya gharama za hapo juu, hicho kibanda ndio kinatumia 650,000 kwenye electrical wiring na kikatumia 445,000 kwenye rangi?
Jidu La Mabambasi hoja yake ni kwamba Waziri Mkuu angelalamikia ubora kwa vigezo vya kitaalam na siyo gharama. Dukani unanunua Soda shilingi 600 lakini baa inauzwa shilingi 1,000 na kwenye zile Hoteli kubwa inaweza kufika hadi shilingi 2,000.

Kwa ivo ukiona mtu kaandika kanunua soda shilingi 2,000 usiseme haiwezekani. Uliza kainunua wapi?
 
Hapo bado ujaweka Armoured cable ya kueleta umeme kwenye hicho kibanda...chukulia ni mita 100 kutoka eneo ambayo main panel hipo.

Tukiona vitu vizuri ulaya tunadhani vinajengwa bure...tuwe serious wadau.
Kwanini uchukulie ni mita 100m wakati Kuna majengo makubwa yapo karibu na hicho kibanda.

Hicho kibanda hakiwezi kuchukua Armoured cable ya size ya ya zaidi ya 2.5sqmm aidha 3C au 4C. Chukulia hiyo Armoured cable per metre ni 5000 pamoja na VAT. Sawa tuchukulie ni mita 100, ukizidisha hapo hiyo Armoured Cable ya mita 100 gharama yake ni TSh 500,000/-. Au tufanye kabisa ni TSh 1,000,000/-.

Sasa ifikie hatua tuheshimiane hakuna kibanda kama hicho kina chojengwa Kwa gharama hizo.
 
Ni kweli mkuu, hii estimate niliifanya kwa haraka haraka.
Na kwa kweli nashangazwa kwa Waziri Mkuu kushangazwa na bei ya hili jengo.
Gharama ambayo kiuhalisia na kwa viwango vyake gharma iko chini.
Nimesikia choo cha Asian cha shilingi 40000. Hiyo bei ni ya choo cha kihindi. Kwenye miradi ya serikali vyoo ni Armitage Shank na hupati cha chini ya 300,000. Dar. Haujakisafirisha. Haujakifunga.

Amandla...
 
Na hiyo armoured cable inajileta yenyewe na inajifukia yenyewe?

Amandla...
 
Inategemea waya za aina gani, hivyo vifaa vya umeme vimetoka wapi na kama fundi aliyefunga anatambulika na mamlaka husika. Rangi vile vile.

Amandla...
Vifaa vya umeme huwa vinatoka wapi kwani hizi Tronic na wenzake si zipo maduka ya vifaa vya ujenzi. Na si zinatambulika na mamlaka za viwango. Kuna waya aina gani zinazotumika tofauti na majumbani, au serikali inanunua nyaya maalum kwa ajili yake.

Mafundi si walewale waliosoma vyuo vyetu na wana certificate au diploma in electrical installation. Si ndio haohao wanatumika na raia.

Ulicholenga hapa ni kwamba serikali ina watu na vifaa vyake special ambavyo ni classified ama nini
 

Ushatoka kwa zamana? Si aliagiza uwekwe ndani?
 
Na hiyo armoured cable inajileta yenyewe na inajifukia yenyewe?

Amandla...
Kijana vyovyote itakavyokuwa huwezi kutumia zaidi ya Milioni 2. Hapo kwanza hicho kibanda huwezi kutumia Cable ikafika 100m. Hilo kwanza weka akilini sababu umeme utafika hapo kwanza kwa ajili ya uwepo wa majengo hayo makubwa, kwenye kibanda kidogo cha mlinzi itakuwa tapping tu ya power kwenda hapo.

Chukulia Armoured Cable imetoka kiwandani Moja Kwa Moja sababu hizi Armoured Cable za 1.5sqmm mpaka 2.5 mara nyingi ni kwa Order ujue bei itapungua, huwezi kukodi semi au Fuso kubebea Armoured Cable ya mita 100 sababu ni mzigo mdogo huo. Usafiri wa hiyo Cable mpaka sehemu husika hauzidi laki 2. Mafundi wa mtaro na kufukia haizidi laki Moja, haya ni makadirio ya juu.
 
Tronic zimepitishwa na nani? Tangu lini umemtumia fundi mwenye diploma kukufungia umeme? Na hiyo diploma in electrical installation inatolewa na chuo gani?

Amandla...
 
Unapajua Uyui?

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…